Polisi: Lissu hatoki

Atanyooka tu.
Mara ngapi mmesema hivyo na bado yuko tu. simtetei lissu.. ila mahali wanaposhindwa polis ni kumkamata alaf wanashindwa kudhibitisha tuhuma dhidi yake. Ndio hapo mahakaman anawagaragaza..
 
Mkondya ni afisa mdogo sana kwa ngazi ya polisi , HANA UWEZO WA KUZUIA LISSU KUWA HURU , atashindwa mapema sana .

Awe Makini sana na kauli zake , huu upolisi una mwisho mbaya sana .

Omary Mahita aliyekuwa IGP wa Tanzania , baada ya kustaafu ALISHITAKIWA KWA KUMTIA MIMBA HOUSE GIRL WAKE NA KUKATAA MATUNZO YA MTOTO , haikufahamika kama ALIMBAKA KWA VITISHO VYA CHEO CHAKE AU WALIKUBALIANA KUFANYA ULE MCHEZO , Bali kinachofahamika ni kwamba Mahita kama kiongozi wa juu kabisa wa polisi , ALIJIDHALILISHA YEYE BINAFSI , ALIDHALILISHA NDUGU ZAKE , ALIDHALILISHA JESHI LA POLISI NA ALIDHALILISHA ALIYEMTEUA PAMOJA NA KUDHLILISHA NCHI YAKE .
 
Kesho jumatatu tarehe 24/7/2017, Tundu Lissu atatoka katika mahabusu za polisi, trust me !!

Labda huyu polisi na inawezekana alimaanisha kuwa hatatoka kwa siku hiyo ya ijumaa, j'mosi na leo j'pili jambo ambalo ni wazi linaeleweka ni kwa sbb gani....

Kwamba, wamezoea kuwakamata wakosoaji wa serikali na Magufuli wao siku za aidha alhamisi ama ijumaa ili wawashindishe katika mahabusu zao week-end yote kwa kusudi eti la kukomoa tu bila hata sababu za msingi....

Lakini anaposema hatumwachia, haeleweki na anajidhalilisha tu huyo polisi na inaonesha kuwa hakusoma somo la sheria ktk Chuo hicho alichosomea !!

Na by the way kwani yeye ni nani hata atoe hitimisho hilo ? Kwani yeye ni mahakama ?
 
kaiba haitoi haki ya kuzungumza?haitoi haki ya kuandamana?haitoi haki ya dhamana?haizungumzii kupeleleza kabla ya kukamata?
Kuminya haya yote ni nini kwa lugha ya kawaida?
Watu wengi wasio na majina wanapitia hizo shida kila siku Tanzania lakini kwasababu siyo mashuhuri tumekuwa tunawapuuza na sasa ni zamu ya waheshimiwa. Binafsi hata simuoni huruma TL , nimekuwa niking'unika ndani kwa ndani jinsi haki za watu wa chini zinavyominywa halafu hawa wapinzani uchwara wanatumia hasira zao kujinufaishia kupitia siasa. Jiulize kwa jinsi TL alivyotoa hotuba unamuona kama ni mtu anaetaka Serikali ijirudi na kuheshimu haki za wananchi wake au alikuwa anataka political mileage?
 

Mkuu, utaratibu wa kumshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano upo katika kila nchi.

Ila wanachofanya polisi wa Tanzania na katika nchi zingine zinazofuata sheria, ni kuomba kibali kutoka mahakamani cha kuendelea kumshikilia mtuhumiwa mpaka upelelezi utakapokamilika.

Tatizo ni kwamba hakuna anaesema kama polisi wamekuwa wakiomba kibali mahakamani cha kuendelea kumshikilia Tundu Lissu zaidi ya masaa 24.

Ingekuwa ni vema mawakili wake bwana Kibatala na Dada Fatma wakatanabaisha hilo.

Hivyo msipotoshe kuhusu hili la kushikiliwa na polisi khasa hili la uchochezi maana upelelezi wake unachukua muda, kutokana na nyenzo za kazi za kipolisi katika kudukua upelelezi.

Na haya yote yanatakiwa kuzingatiwa na Tundu Lissu pale anapozungumza na kutoa maneno ya uchochezi eti nchi inaendeshwa kikanda na kikabila.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…