Polisi kumulika CHADEMA kutokana na kupanga njama zenye mwelekeo wa ugaidi

Maigizo tu haya. Mbona taarifa za kuhusika Kwa Ikulu na kina Msangi na Ighondu kwenye kumteka , kumtesa na kujaribu kumuua Dr.Ulimboka hawakuzifanyia kazi.Wameishia kulifungia Gazeti Zalendo la Mwana.halisi.
Jeshi la polisi haliheshimiki wala haliaminiki.
 
Hivi nyie mnawaona watanzania kama wajinga sana siyo? Hawa wanaoua ni chadema? Tumia akili acha kutumika
attachment.php


naona Redbrigade kamnyooshea marehemu Mwangosi mtutu hapo.

R.I.P Mwangosi.
 
Mchange sio atoe maelezo ya kusaidia bali akamatwe na kuwekwa kizuizini kama mtuhumiwa aliyekiri kwa kinywa chake kuhusika na ugaidi na mauaji, kisha uchunguzi uendelee kwa wengine aliowataja ikithibitika waunganishwe naye akiwa ameshafikishwa mahakamani kwanza.
 
Nimetandwa na hofu kubwa na sintofahamu juu ya jeshi letu dhidi ya usalama wa raia wake.
Inawezekanaje kukawa na tuhuma nzito kiasi hiki za ugaidi na zisifahamike? mpaka ajitokeze mtu mmoja tu na kuaminiwa?
Hili jeshi linafanya kazi gani??? nahisi lazima kuna mchezo mchafu utakuwa unafanyika hapa...jeshi letu limejijengea sifa ya kutoaminika kwa wananchi wake kwa muda sasa, na hii ni kwa sababu wamesahau viapo vyao na kufuata maslahi yao binafsi, kwani kila mtu anaelewa kauli hii KUINGIA BURE , KUTOKA PESA.
Sasa kama vitendo hivi vitafanyika kwa mlipa kodi wa kawaida anayetumia chini ya dola moja kwa siku, inashindikana vipi kurubuniwa na vigogo ili kutekeleza azma zao binafsi??? niliwahi kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa kuna ofisa (Kombe)mmoja alifananishwa na jambazi na kuawa na jeshi huku akiwa ameinua mikono juu kujisalimisha. Kuna nini tena??? Vipi kuhusu Mauaji ya wafanyabiashara wa madini yaliyotekelezwa na jeshi msitu wa pande??? vipi kuhusu mauaji ya walipakodi wasiohatia wa Morogoro, yalitekelezwa na nani??? Mbona hili jeshi limeshindwa kusimamia amani na kujifanyia mambo yake lenyewe???
Hapa hakuna ubishi kuwa jeshi la polisi limekuwa ni bendera.
Kwa maoni yangu ningeshauri DCI ajimulike kuanzia miguuni kwake na ndipo aweze kumulika wengine, vinginevyo, tunadanganyana, na kwa jinsi hii, ipo siku kila mtu ataamua lake!
Naamini kwa kauli hii MAONI YA WENGI NI MUNGU, sasa laana hii ya wananchi jeshi la polisi litaibebea wapi??? maana ni laana ya Mungu. dhamana ya ya usalama wetu na mali zetu, ipo mashakani, tumekosa imani nao, je, ni nini kitafuata??? Maana kila mtu anajua ni nini jeshi la polisi linafanya, simply UONEVU, kila mtu anajua.
Mzimu huu wa uvunjifu wa amani unatengenezwa na jeshi la polisi lenyewe, utakapowarudia naomba wakae mkao wa kuukubali, maana wanaanzisha kisha wanakaa pembe kusikiliza.
Tunaona machafuko yalivyoitanda dunia, kwani sisi tuna nini mpaka Mungu atuepushie na janga la ukosefu wa amani? Hamjui ni kwa neema tu? narudia tena, DCI aanzie miguuni pake ndo amalizie na kiporo cha mchange.
 
chadema kila mtu anajua ni waharifu sana siyo watu wa kuchekea hata kidogo polisi wacheze nao wasiwaache hata kidogo wameuwa watu wengi sana.
mhuni tu ndiyo anaweza fikiri this way kwamba serikali ipo chadema inauwa watu wengi sana tena wengine mbele ya RPC,ie case ya mwangosi, kwamba CDM ilivalisha watu nguo za polisi ujinga wa hali ya juu, ccm itakuwa imeishiwa mikakati inatengeneza akina mchange ili ionewe huruma halafu B7 mnakuja kushangilia wakati kimsingi jambo hili ni aibu kwa serikali na ccm, lkn kwa ujinga wenu mnaona kama cdm imejulikana maovu yake, hivi nyie B7 njaa zenu haziwapi hata nafasi ya kutumia akili zenu?
 
Polisi watakuwa wana ujinga usioelezeka kama wanamwona aliyemwua Mwangosi lakini wanasema siyo huyu bali yupo mwingine. Rubbish.
 
Natamani sana jeshi lichukue madaraka. Kila uozo utakuwa hadharani na hapo ndipo huu usanii wa policcm na wajinga wengine utapata majibu sahihi. Jeshi letu tunawaamini kamateni nchi.
ndo kilicho bakia tu tz jeshi lishike nchi uozo wote uekwe hadharani
 
BARAZA LA VIJANA MKOA WA NJOMBE LIMEPINGA VIKALI TUHUMA ZINAZOENDELEA KUTOLEWA NA SERIKALI DHIDI YA CHADEMA KWA KUTUMIA VYOMBO VYA DOLA NA USALAMA WA TAIFA. AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA MKOA WA NJOMBE KWA NJIA YA SIMU kiongozi wa vijana WA CHADEMA MARA TU BAADA YA KUCHAGULIWA SIKU MBILI ZILIZOPITA ANASEMA HIZI NI NJAM ZA WAZI ZA CCM KUTAKA KUWAFANYA WATANZANIA WAKICHUKIE CHAMA CHAO KWA MINAJILI NI CHAMA CHA WAUAJI, LAKINI PIA LENGO LINGINE NI KUENDELEA KUPOTEZA LENGO NA KUTAKA KUFUTA AJENDA YA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA NA WATU WAJADILI MAUAJI NA KUDAI CHADEMA NDIO WAHUSIKA.
MWENYEKITI HUYO WA VIJANA ALIDAI HUU NI WAKATI WA UCHAGUZI NA WANACAHAMA WAJIKITE KATIKA MWASWALA YA UCHAGUZI KAMA CHAMA CHETU KINAHUSIKA NA SERIKALI PAMOJA NA VYOMBO VYAKE WANAO USHAHIDI BASI WACHUKUE HATUA NA SIO VINGINEVYO, LAKINI VEMA WAKAJUA KUWA WATANZANIA SIO WAJINGA WANAJUA NANI KAUA NANI ANASINGIZIWA, WITO KWA WANCHAMA NA WAPENZI WA CHADEMA TUZIDI KUUNGANA KATIKA KUPAMBANA NA CHAMA KISICHO NA NIA YA DHATI YA KULETA UKOMBOZI KATIKA NCHI HII.
 
Michezo ya bata kuku haiwezi,ccm wanataka kutumia style zile zile walizotumia kwa NCCR na Cuf kuididimiza chadema? Hii itabuma milele,asante kwa tamko la kiongozi wa Bavicha
 
Ni vyema wakafanya zoezi hili kwa kufuata misingi ya haki, sheria na utawala bora.


Ninategemea huyu DCI ana akili timamu za kuelewa hata wengine japo hawana magwanda ya polisi wanaelewa hata zaidi yake. Na hivyo sitegemei atatumia raslimali na muda wa taifa kuchunguza cdm waliwavalisha magwanda raia na kuwapa silaha wamuue mwangosi. Na akikubaliana na hilo, atakuwa mwehu.

La pili anapaswa aelewe, kuwa yeye ni mtumishi wa serikali na si wakala wa ccm. Uzito alioyapa maelezo ya mchange, alipaswa kuwa ameshautoa vile vile kwa maelezo ya madiwani wa shinyanga waliobainisha ugaidi na hujuma kama sera za mambo ya ndani ya ccm.

Akumbuke kwamba jeshi lake siku zote halina uwezo wa kudhibiti machafuko nchini na yanapotokea, polisi hukaa kando na kuwaachia JWTZ.

Njama zozote dhidi ya CDM, operation yoyote yenye picha ya uwakala wa ccm kudidimiza cDM, upendeleo wowote kwa ccm na ugaidi wake na ama uonevu wowote utakaofanywa kwa CDM, na kuonyesha kwamba ni katika michakato ya kutaka kudhoofisha CDM kuelekea uchaguzi mwakani, (kama walivyofanya kwa Rwakatare, na kumezea ugaidi wa akina masele), utapelekea machafuko makubwa sana na ya kihistoria Tanzania.


Haihitaji kutafuta kura za maoni ili kutambua ni kwa kiasi gani Watanzania wamechoshwa na uonevu unaofanywa na serikali kwa kutumia dola kwa vyama vya upinzania hasa vinavyodhihirisha nguvu ya kukubalika zaidi ya ccm.

Polisi ifahamu amani ya nchi hii inategemea sana uadilifu na ukwlei wao katika kushughulikia masuala yanayogusa siasa nchini.
Nakupongeza kwa mawazo yenye mtazamo mpana. Some folk wanashabikia bila kujali matokeo yajayo.
Kwenye platform, tunataka mawazo ya kujenga nchi siyo ushabiki unaopinga hata facts. POLISI WAWE MAKINI WASIWE CHANZO CHA VURUGU.
 
Mimi si mwanachama wa CHADEMA lakini ni Mtanzania mwenye kuelewa nini kizuri kwa maendeleo ya Watanzania. Ninaomba CDM, kuanzia wanachama wa kawaida, wapenzi na wafuasi, na viongozi wote wa chama hiki katika ngazi zote. Msikubali kuchepushwa na mizengwe inayotokea na itakayokuja. Kelele hizi zote zimebuniwa makusudi kuwatoa kwenye msingi na kuvuruga ufahamu wa Watanzania wa kawaida. Mkilijua hili msipoteze muda wenu kulumbana wala kushugulika na haya na mvumo huu, vinginevyo mtakuwa mmewapa adui zenu goli la wazi. Kikubwa kwa sasa kazaneni kuimarisha chama kwa kuandikisha wanachama wengi na kuwaimarisha katika ngazi za vijiji ama mashina. Tumieni muda huu vizuri katika uhamasishaji na mafunzo sahihi kwa wanachama wenu wa ngazi za chini. Tena mwende kwa mwendo wa kasi kuliko hapo awali maana muda ni mfupi. Mengine Mungu atawasimamieni na kuwapa maarifa na neema.

BARAZA LA VIJANA MKOA WA NJOMBE LIMEPINGA VIKALI TUHUMA ZINAZOENDELEA KUTOLEWA NA SERIKALI DHIDI YA CHADEMA KWA KUTUMIA VYOMBO VYA DOLA NA USALAMA WA TAIFA. AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA MKOA WA NJOMBE KWA NJIA YA SIMU kiongozi wa vijana WA CHADEMA MARA TU BAADA YA KUCHAGULIWA SIKU MBILI ZILIZOPITA ANASEMA HIZI NI NJAM ZA WAZI ZA CCM KUTAKA KUWAFANYA WATANZANIA WAKICHUKIE CHAMA CHAO KWA MINAJILI NI CHAMA CHA WAUAJI, LAKINI PIA LENGO LINGINE NI KUENDELEA KUPOTEZA LENGO NA KUTAKA KUFUTA AJENDA YA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA NA WATU WAJADILI MAUAJI NA KUDAI CHADEMA NDIO WAHUSIKA.
MWENYEKITI HUYO WA VIJANA ALIDAI HUU NI WAKATI WA UCHAGUZI NA WANACAHAMA WAJIKITE KATIKA MWASWALA YA UCHAGUZI KAMA CHAMA CHETU KINAHUSIKA NA SERIKALI PAMOJA NA VYOMBO VYAKE WANAO USHAHIDI BASI WACHUKUE HATUA NA SIO VINGINEVYO, LAKINI VEMA WAKAJUA KUWA WATANZANIA SIO WAJINGA WANAJUA NANI KAUA NANI ANASINGIZIWA, WITO KWA WANCHAMA NA WAPENZI WA CHADEMA TUZIDI KUUNGANA KATIKA KUPAMBANA NA CHAMA KISICHO NA NIA YA DHATI YA KULETA UKOMBOZI KATIKA NCHI HII.
 
MTU kama huyu ni hatari sana, na hafai kabisa
Yaani mfano. Unamwona MTU anamuua MTU mwingine na muuaji anakuona, hivi kirahisi tu atakuacha ukawe shahidi??
Umeona wapi movie Hii???
Jeshi la polisi lingepaswa limtie hatiani machange kwani tayari kajishuhudia na wamuulize tu kama hakushiriki, Je mbona hakutoa ripoti iyo mapema???
 
chadema siyo chama cha siasa ni genge la waharifu hakuna kiongozi aliyemsafi hata mmoja.

CCM wasafi sana yaani hakuna mharifu, unajua chama hiki ni wasafi wanapinga wizi, ufisadi, na chadema kila siku kazi yao kuisingizia ccm, Maisha mazuri sana kwa watz yaani tuko mbali kimaendeleo kwa 7bu ya ccm..aisee gsu acha tu 2015 ccm tu kwa 7bu wanajua uongozi we dvn one 300 mpka dvn one 4na ushee uko ccm wako vizuri acha gsu
 
Last edited by a moderator:
PolisiCCM kitengo cha MACCM cha kupambana na CHADEMA. Kazi ya kuhakikisha usalama wa Watanzania na mali zao imewashinda sasa wamebaki kutumika na Maintarahamwe ili kuwadhibiti Viongozi wa CHADEMA na ikiwezekana kuwabambikia kesi nzito katika juhudi za kuisambaratisha CHADEMA.


  1. Pamoja na Kikwete kudai anawajua wauza unga nchini, lakini polisiCCM imeshindwa kufanya uchunguzi wowote kuhusiana na wauza unga wanaofahamika na Kikwete.
  2. Pamoja na ushahidi wa kutosha wa wahusika waliomtesa na kutaka kumuua Dr Ulimboka, hakuna uchunguzi wowote uliofanywa kuhusiana na ushahidi huo.
  3. Hadi hii leo muuaji wa Askofu Augustino Shayo aliyeuawa Zanzibar polisiCCM imeshindwa kumtia mbaroni
  4. Mpaka leo hii aliyemuua Mwangosi bado hajatiwa mbaroni
  5. Hadi hii leo wahusika wa mauaji kule Arusha katika mkutano wa CHADEMA kwa kurusha mabomu bado hawajakamatwa.
  6. Katika kesi dhidi ya Lwakatare ambapo alibambikiwa kesi na gaidi maarufu wa MACCM, polisiCCM walishindwa kumtia hatiani mzushi wa ushahidi ule uliosemekana kwamba "ungekubalika hadi mbinguni"
  7. Kikwete pia alidai analijua genge la wauaji wa Tembo nchini ili kuvuna meno ya Tembo, lakini polisiCCM hawajafanya uchunguzi wowote hadi hii leo.
  8. Wabunge wa MACCM walipokea rushwa toka wizara ya nishati na madini wakati Ngeleja alipokuwa Waziri ili kusaidia kupitisha bajeti ya wizara, hakukufanyika uchunguzi wowote na polisiCCM dhidi ya watoa rushwa na wapokea rushwa katika sakata lile.
  9. Majambazi walivamia duka Kariakoo na kukwapua mfuko uliokuwa na shilingi 150 million, baada ya kukimbizwa na polisiCCM waliamua kuutupa na ukaokotwa na polisiCCM lakini pesa zile hazijulikani zilipo hadi leo. Wahusika walitiwa ndani kwa siku chache na kutolewa baada ya kuwekewa dhamana lakini kesi dhidi ya wahusika imekuwa ikipigwa kalenda.
  10. Pamoja na Watanzania wengi kuiona polisiCCM kama taasisi inayoongoza kwa rushwa nchini lakini Waziri wa Mambo ya ndani na IGP hawajachukua hatua zozote kupambana na hali hiyo na rushwa ndani ya taasisi hiyo inazidi kukithiri siku hadi siku.

PolisiCCM wameshakurupuka tena ili kuutumia ushahidi kutoka kwa mtu ambaye hana credibility yoyote hata kwa wale wanaomfahamu kwa karibu, katika juhudi nyingine za kuwabambikia kesi viongozi wa juu wa CHADEMA ili kukisambaratisha chama hicho.


Taasisi hii inabidi isafishwe kwa kiwango cha juu kabisa ili kurudisha heshima yake iliyopotea kwa miaka mingi sasa, lakini sioni hilo kama litafanywa na hii Serikali dhalimu ambayo imeifanya taasisi hiyo kama ni moja ya vitengo vyake.

Ukombozi wa pili wa Tanganyika ni lazima utapatikana

Alutta continua! continua!

:peace: :peace: :peace:

 
Back
Top Bottom