Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi watatu

Polisi wasio na weledi ndio wanakimbilia kutumia silaha, Polisi majambazi ndio wanaua watu na kuwabatiza ujambazi, Polisi wa mambosasa mwenye fremu za maduka 100 mabwepande ndio deal likibuma wanakuondosha usijewataja.

Kumbuka mnaowaua wana wategemezi wao ambao wataathirika maisha bila hatia, kumbuka laana mnayoitengeneza mpaka kizazi chenu cha tatu itawatafuna hata mkiwa kaburini.

Mh. Samiah badilisha uongozi wa polisi makao makuu, mpe mtu ambaye ni kweli analipenda jeshi na amefanya utafiti mpaka amepata PhD ya kazi za Polisi zinavyotakiwa kuendeshwa atarudisha heshima ya taasisi hii ambayo wananchi wanaichekea mdomoni moyoni wanalia, wanaiogopa hawaipendi, wanahofu nayo na wala hawaiheshimu.

Wapo polisi wamewekeza kwenye uhalifu wanafanya uhalifu ndio kitega uchumi wanashiriki moja kwa moja ujambazi nakisha rais ukiwalaumu hawafanyi kazi wanatafuta wa kuwatoa kafara wakuridhishe. Inauma sana.
 
Mmmhhh mara mmeanza kuua?
Msije mkawa mnatengeneza stori
Kwa nini kila siku huwa mnaua tu hamuwezi kuwakamata na kuwapeleka mahakamani?
Nyie haya
Kutulinda mpaka mshitukizwe mpange tukio weledi mmh mmh upo kweri au show?
Hili jeshi kwa kweri
Mambosasa katishiwa kuondolewa Dsm ataua sana hata kuloga ataloga ili mradi aonekane anafanyakazi! Ukweli mambosasa amekaa sana kanda maalumu atoke aletwe kamanda mwingine haraka sana.
 
Wake polisi wa patrol mafuta hiwa wanapata wapi,polisi wa defender??


Wakiingia sheli wanajichotea tu mafuta acha kutetea ujinga
 
Pongezi kwa jeshi, yule askari machachari wa kupambana na majambazi kisharudi?
Waongeze masnichi mtaani.

Everyday is Saturday...............................
Ni Mambosasa. Baada ya kuona kula yake inatikiswa. Ni hatari kwani wanaweza kuua na wasi na hatia ili kuonysha wako makini
 
Nakumbuka ile issue ya akina Zombie,ilianza kuripotiwa kama hii "eti polisi wamekuwa majambazi" Kila mtu akaamini,mwisho wa siku ukweli ukawekwa wazi,kumbe waliouwawa walikuwa ni wafanyabiashara ya madini tena Wana ndugu,very sad story.
 
Ulikuwepo ukaona anatupa risasi?? Polisi mwenye weledi hawezi kurushiwa risasi kwa sababu hafanyi confrontation ya mhalifu.
Weka hadithi ya kwako ambayo hawakutupa risasi tuijadili.
Hii iliyopo inasema walitupa risasi.
Kipimo cha weledi wakati wa vita si somo jepesi.
 
Tutaamini vipi kwamba hao majambazi hawakuwa wameshaiba tayari pesa nyingi, na hao polosi wakaamua kuwafanyia ujambazi hao majambazi kisha wakapoteza ushahidickwa kuwamaliza? Tutaamini vipi?! Maana Zombe alituondolea imani kabisa kwa jeshi la polisi, hiyo imani haitakaa iridi tena!!!
 
Safi sana.

Dawa ya moto ni moto.

safi sana na pongezi kwa Jeshi letu la polisi kwa kazi nzuri

kamwe msiwaache majambazi wavunje heshima ya Jeshi letu la polisi, hilo haliwezekani, tuwaahidi kutoa ushirikiano kuwafichua majambazi wote na wezi katika mitaa yetu.
 
Tulitoa tahadhari kwa majambazi baada ya kauli ya Mh SSH ,watakula vyuma sana wasipoacha ujambazi ,dawa ya jambazi hakuna kujadiliana nae ni kumlisha chuma tu na mtandao wao wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…