Polisi Kagera wamzuia James Mbatia kutembelea maeneo yaliyoathirika na kugawa misaada

Ben Saanane

JF-Expert Member
Jan 18, 2007
14,581
18,124
Angalizo: Post hii imeandikwa kwa Upole kabisa.
Jana Jioni Tukaondoka Bukoba kwenda Dodoma tukamuacha Mhe.Mbatia akiendelea kushirikiana na viongozi wengine eneo la Maafa

Polisi wakaanza kumtafuta na mwisho wa Siku wakamzuia kuendelea kutembelea maeneo hayo na kugawa misaada mbalimbali

Tuna habari tunazotafuta uthibitisho kuwa Hata maturubali yaliyotolewa na Viongozi Freeman Mbowe, Mhe.Mbatia, Mhe.Severina Mwijage, Mhe.Lwakatare kwa niaba ya viongozi wa UKAWA kwa wananchi kwa ajili ya kutengenezea mahema kama sehemu ya msaada wa Dharura kwa wananchi hao waliokuwa hawana msaada wowote, Polisi walipita na Kuanza kuyakusanya.Wanadai misaada yote ipite kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa tu.Urasimu usio na maana katika crisis hii.

Kwanini Polisi watumie muda na nguvu kufanya haya? Kwanini wasitumie nguvu hizo wao na jeshi kama sehemu ya Rapid Response kusaidia watu hawa waliokuwa stranded kwa zaidi ya saa 72?

Kwenye majanga haya tunahitaji Umoja wa Kitaifa zaidi. Waliothirika ni Watanzania wenzetu.

Leo Bungeni Mwenyekiti wa Bunge Mhe.Azzan Zungu ameomba radhi kwa Ubaguzi uliofanyika Bungeni leo baada ya mtoa taarifa ya Serikali kumbagua Kiongozi wa Kambi ya Upinzani wakati akitoa pongezi kwa viongozi wa kitaifa walio-respond haraka kuhusiana na maafa haya

Hata juzi polisi walitufuata Nyakato Sekondari wakiongozwa na OCD.

Maafa haya yametuvua nguo kama Taifa. Hata kwenye majanga bado watu wanataka kuleta siasa tena za kibaguzi.

Hali hii inatoa picha kwamba Taifa limegawanyika

Picha iliyojitokeza Bukoba ndio hali halisi ya Taifa letu

Taifa lisiloweza ku-respond haraka katika kuokoa maisha ya watu wake na kuendeleza lugha za "Tumepeleka wataalamu kufanya tathmini au Uhakiki" ni taifa lisilojua interest zake.

Primary interest(Maslahi ya Msingi Kabisa) za kulifanya taifa lolote kuwa taifa linaloheshimika ni kulinda watu na Ardhi(Mipaka) yake. Ndio maana taifa lolote lipo tayari kuingia vitani kwa ajili ya kulinda hata nchi moja ya Ardhi yake au Mtu wake. Ndivyo nadharia za Diplomasia na siasa za kimataifa zinavyoelekeza.

Sasa kwa hapa kuna kitengo chini ya Waziri Mkuu nilidhani kitengo hiki cha Maaafa ni kwa ajili ya kulinda Interest hizi .Kina wataalamu na kila kitu standby

Serikali inashibdwaje kutoa hata Milioni 300 za dharura ili watu wasilale nje na kukosa vyakula?

Kwa kuwa kuna kambi za majeshi kanda ya Ziwa ambako tumepakana na nchi Tatu ilishindikana nini kufunga mahema haraka na kutoa msaada ?

Mungu Epushia Mbali,tungekua tumevamiwa na Adui kijeshi tukapigwa mabomu ingekuaje?

Nawapongeza wafanyabiashara waliojitolea jana

Walionesha Utaifa bila Ubaguzi ingawa Rais Magufuli mara nyingi amekua akitumia lugha za kuwagawa watu

Mara nyingi amekua akisema alichaguliwa na Watanzania Maskini

Jana Matajiri wamejitolea kuwasaidia Watanzania waliokumbwa na maafa bila kujali ni Tajiri au maskini aliyeathirika

Tetemeko hili limetu-expose

Mungu wape wepesi watu wa Kagera

Mungu ibariki Tanzania

Aluta Continua,Victory Ascerta....

Ben Saanane

xxxxxxxxxx
UPDATES:

Mhe.James Mbatia ameendelea na Ziara Misenye
 
Unajua hii inamaanisha nini?
Hii inamaanisha kitu chochote kutoka kwa wapinzani, iwe mradi wa maendeleo au wazo au mapendekezo yoyote mazuri ni haramu tu kwa serikali ya Magufuli

Hata bungeni wapinzani wanaenda kuchukua posho za bure tu, maana serikali hii sikivu haitakaa ichukue mchango wowote hata uwe wa maana kiasi gani

Ndio maana hata wakazuia meya wa kinondoni kupokea mashine ya kuchakata taka kwa kuipandishia kodi wakati ni ya msaada, wakakataa madawati ya Bulaya, msaada wa Lwakatare n.k

Nadhani watawazuia hata waandishi wa habari kuandika habari za wapinzani siku za karibuni

Halafu kuna mtu anakaa jukwaani na kujinasibu maendeleo hayana chama,

Nadhani ile hotuba aliyotoa Magufuli kule Unguja na Pemba ndio hotuba za kutoka moyoni mwake kweli, hotuba zilizojaa chuki, visasi na kukomoana,
 
Kuna mambo mengine yanatia fehdeha. Kuna ubaya gani kwa UKAWA kuwasaidia manusura wa tetemeko. Hivi Polisi wanapowanyang'anya manusura vifaa vya kujikimu wanategemea wataishije? Tulipofika ni pabaya sana na kama kweli hili limejitokeza litakuwa limeitia doa kubwa serikali.
 
Ni kweli turubai zote zimekusanywa!!Wanasema ni maagizo kutoka juu kuwa misaada yote waliotoa upinzani iondolewa kwa Wananchi wasubilie ile ya Serikali.
Agizo ni kuwa hata Viongozi wa vyama vya upinzani wanaozunguka kuwapa pole wananchi wanatakiwa kuzuiliwa.Nimehuzunika,nimesikitika...Sikutegemea hili kutokea ktk kujenga umoja wa Kitaifa

Katika hili nafsi yangu inanisuta...Siwezi kuwa upande wa Serikali ninayoipenda!!Nitakuwa upande wa huzuni ya nafsi yangu!!Wakati mwingine kutii mwitiko wa nafsi na dhamira,ni afya kwa mwili na Roho.Visilani havijengi
 
Kama ni hivyo kuna haja gani sisi wafanyabiashara wakubwa tunaounga mkono upinzani kuendelea kutoa misaada ?

Ubaguzi ni laana mbaya sana , wakitubagua sisi hawataishia hapo , wataanza kubaguana wenyewe .

Haya yote yanatokana na kauli ya Simbachawene bungeni , lakini nakuhakikishia kwamba Mungu hatowabakisha wanafiki , ni suala la muda tu .
 
Ni kweli turubai zote zimekusanywa!!Wanasema ni maagizo kutoka juu kuwa misaada yote waliotoa upinzani iondolewa kwa Wananchi wasubilie ile ya Serikali.
Agizo ni kuwa hata Viongozi wa vyama vya upinzani wanaozunguka kuwapa pole wananchi wanatakiwa kuzuiliwa.Nimehuzunika,nimesikitika...Sikutegemea hili kutokea ktk kujenga umoja wa Kitaifa

Katika hili nafsi yangu inanisuta...Siwezi kuwa upande wa Serikali ninayoipenda!!Nitakuwa upande wa huzuni ya nafsi yangu!!Wakati mwingine kutii mwitiko wa nafsi na dhamira,ni afya kwa mwili na Roho.Visilani havijengi
Viongozi wa UKAWA angalieni uwezekano wa kuratibu haya mambo kivyenu , hili ni jimbo lenu , msikubali kupangiwa namna ya kutoa misaada.
 
Mbatia alisema hakuna kinachofanyika, wakati huo Mabilioni yameshachangwa .... HUO NI UCHOCHEZI
Uchochezi ni kukaa bungeni kila mwaka,na kutenga mabilioni kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu,ambayo ndani yake kuna Kitengo Cha Maaafa!!Halafu miaka mingine maafa hayatokei na pesa hazijulikani zimeenda wapi.

Halafu Majanga yanatokea miezi mitatu baada ya bajeti kupitishwa,Serikali inalalamika na kupitisha mabakuli kwa watu huku Kitengo cha Maafa kikibaki "bubu wa misaada" katika maeneo yaliyoathirika.Tetemeko limetuumbua kuwa bajeti iliyopitishwa kwa ajili ya Kitengo cha Maafa ni bajeti hewa.Kumbe sasa si tu tuna wafanyakazi hewa,Bali tuna bajeti hewa ndani ya Ofisi kubwa ya Shughuli za kila siku za Serikali.

Hii ni aibu ya sharti moja kubwa!!Kuchutamana bila kugeuka nyuma!!
 
Mbatia alisema hakuna kinachofanyika, wakati huo Mabilioni yameshachangwa .... HUO NI UCHOCHEZI

Ukweli unauma.Serikali iko tayari kugharamia mabilioni kuwaweka polisi mitaani kufanya mazoezi,lakini imeshindwa kutoa msaada wakati wa dharura ya kibinadamu.Na bado wamewanyang'anya wahanga misaada waliyopata toka pande ya pili sijui kama ndiyo ubinadamu au ndiyo sera za CCM inashangaza sana.
 
Back
Top Bottom