Polisi jamii wanalipwa na nani?

Mkuu The Boss hawa watu wanaojiita polisi jamii sijui wako kwenye sheria ipi maana afadhali ya sungusungu wana sheria yao na wale Auxiliary Police nao wana sheria yao ila hawa ambao wamejaa kariakoo kama utitiri sijui wanalipwa na nani au ndo ile mbuzi hula urefu wa kamba yake
 
Last edited by a moderator:
Hawa wanakula faini ya papo kwa papo mfano anakufuma unakunya kichochoroni faini Tsh.50,000/= anakula yeye

mamlaka hayo anapewa na nani? na kwa qualification zipi?
Ama huu upolisi jamii pia ni ujasiriamali?
 
Wamemaliza mafunzo flani hivi pale chuo cha bandari Tandika kwa manispaa ya Temeke, kweli hawalipwi. Wanasaidia kuweka usalama kwa mambo madogomadogo kama kukojoa ovyo, uzururaji usiku nk. ukikamatwa na hawa `Polsi Jamii` unalo faini Elf 50. au uende nao mbele.....
 
we Mamndenyi weweeee?

elfu kumi?

mnalipa???

khaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!

aisee mi wangeisikia kwenye bomba, la wanipe sheria inayoruhusu kukusanya mapato ya namna hiyo kwa wananchi

then najizatiti kiulinzi maana ndo vibaka wenyewe, huku nikimpiga biti mwenyekiti ole wako niibiwe hata kijiko...



 

There are things in life that are very difficult to explain....
Nadhani ndio wahalifu wenyewe hao.
 
BADILI TABIA
mambo ya bongo ni wizi mtupu,
tena wanazo na risiti feki zile
halafu kwa hasira wala sijawahi kuzipitia nione
ni za wapi.
 
Last edited by a moderator:
sasa hivi polisi hawafanyi kazi za ulinzi kisa polisi jamii ukienda kwenye polisi posti ukiripoti tukio utakuta ama polisi mmoja unaambiwa subiri polisi jamii ingawa polisi kila mwisho wa mwezi wanapokea mshahara wengi wao ni vibaka hawana mafunzo stahiki wakikamata mtuhumiwa ama wanampora au kuomba rushwa
 
Mimi ni polisi lakini mpaka sasa nashangaa siku moja nikawauliza sikupata jibu la maana zaidi ya mazingira ya Rushwa tu.
 
Haya jamaa ukikamatwa nao ni sawa umekamatwa na vibaka.Kama mnabisha niulizeni nini kilinikuta.
 
Katika mikoa mikubwa kma dsm kamati za ulinzi na usalama mkoa huwa wanaomba misaada kwa makampuni na wafanyabiashara wakubwa kila mwezi kuchangia mfuko wa pj

na hao wafanyabiashara wakiwa ndo wahalifu wenyewe lakini wanachangia pesa?
 
Utawala mmbovu na maamuzi mabovu, Wale jamaa ni vibaka wazoefu wamevunja dhana ya police jamii,

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 


hili ni janga hili
 
Mimi ni polisi lakini mpaka sasa nashangaa siku moja nikawauliza sikupata jibu la maana zaidi ya mazingira ya Rushwa tu.

Yaani wewe polisi na unashangaa na sisi je?
 


Yaani wanawachangia vibaka
 


yaani polisi wenyewe ni tatizo
na hawa nao wanazidisha tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…