Polisi jamii wanalipwa na nani?

Polisi jamii wanalipwa na nani?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,611
Kila mtu anajua kuwa mishahara ni midogo mno
kwa polisi wa Tanzania hadi wengine kudai rushwa
na hata kushiriki uhalifu ili wapate kipato

Sasa ghafla bin vuuu kuna wimbi la watu ambao wanaitwa
'polisi jamii' wanavaa uniform na wamesambaa jiji zima
kwa Daresalaam....
nasikia kwamba hawa watu hawalipwi ni wanajitolea

haingii akilini mtu kujitolea siku nzima au wiki nzima
kufanya kazi ya kujitolea bila malipo
je hawa watu wanalipwa?
na kama hawalipwi wanaishije?
na hatari za kuwa na hili jeshi lisilo rasmi ni zipi?

sasa naona wameanza kukamata magari barabarani pia
what next huko mbeleni?
 
Kama mtu aliweza kujivalia uniform za askari wa barabarani na kula vichwa sidhani kama itashindikana kwenye polisi jamii.

na hili ndo haswaa naliona
na wanakamata magari na kuchukua rushwa tayari now
 
na hili ndo haswaa naliona
na wanakamata magari na kuchukua rushwa tayari now

"Rushwa imeenea kila mahali, katika sekta na nyanja zote (horizontal) na kwa ngazi zote, kuanzia Ikulu hadi ofisi ya kitongoji, balozi, kaya na mtu binafsi" - per Mbunge wa Magu, Dk Festus Limbu.
 
yaani hawa ndo vinara wa uhalifu, ukienda temeke wale vibaka ndo wamevalishwa uniform, buguruni pia, mwenge, ubungo, wanafahamika kuwa ndo wale wale vibaka lakini ndo wamepanda cheo wanaitwa polisi jamii, ukipita bara bara ya Tandare ni balaa tupu kila kituo wapo ni mateja ndo wamepewa uniform za polisi jamii. The Boss hata mimi nilikuwa na maswali kama yako, nitafurahi tukijibiwa wote
 
Last edited by a moderator:
Mwema atakumbukwa sana kwa kumaliza era ya ngunguri kwny polisi sasa ule wimbo wa polisi kamata kidevu kinawasha kirahiisiii unawaimbia polisi......
 
je, hao polisi jamii ni kama sungusungu? au tofauti?

Nadhani sungusungu is more of a neighborhood watching groups.

Shughuli za sungusungu zinatambuliwa kisheria na People's Militia Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 1989).

Hawa polisi jamii wanatambuliwa chini ya sheria ipi? Wana powers zipi?

Inasemekana kuwa sababu za kuanzisha polisi jamii zilikuwa ni pamoja na kutatua baadhi ya matatizo ambayo sungusungu walikuwa walikuwa wanakabiliana nayo hasa katika interventions zao. Sungusungu ilikuwa very effective mpaka pale ilipoanza kuhusishwa na itikadi za CCM katika miaka ya 1990s baada ya kuanzishwa siasa za vyama vingi.

Tofauti na Sungusungu, nadhani polisi jamii ilianzishwa kupitia muundo wa sasa wa kipolisi na wanafanya kazi kama Dar es Salaam City Auxiliary Police kwenye ngazi za chini kabisa kama kata, vitongoji.

Sungusungu walikuwa siyo professionals. Polisi jamii ni, au wanatakiwa kuwa, professional.

Pia nadhani sungusungu walikuwa wa kujitolea, lakini hawa polisi jamii wanatakiwa walipwe kutokana na kazi zao.
 
Katika mikoa mikubwa kma dsm kamati za ulinzi na usalama mkoa huwa wanaomba misaada kwa makampuni na wafanyabiashara wakubwa kila mwezi kuchangia mfuko wa pj
 
yaani hawa ndo vinara wa uhalifu, ukienda temeke wale vibaka ndo wamevalishwa uniform, buguruni pia, mwenge, ubungo, wanafahamika kuwa ndo wale wale vibaka lakini ndo wamepanda cheo wanaitwa polisi jamii, ukipita bara bara ya Tandare ni balaa tupu kila kituo wapo ni mateja ndo wamepewa uniform za polisi jamii. The Boss hata mimi nilikuwa na maswali kama yako, nitafurahi tukijibiwa wote

Wakati huo huo imeripotiwa leo kuwa

ULINZI SHIRIKISHI MKOANI SINGIGA WAMEWAKAMATA WATOTO 11 WAKISHIRIKI NGONO usiku wa kuamkia jana. watoto hao wana miaka kati ya 12 mpaka 15. Walikutwa wakifanya mapenzi katika chumba kimoja chenye kitanda kimoja kama ilivyoonekana katika television.

https://www.jamiiforums.com/mahusia...kwa-kufanya-mapenzi-katika-chumba-kimoja.html
 
Back
Top Bottom