Polisi Iweke wazi picha za majambazi wanaokamatwa

Sele Mkonje

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
643
844
Habari za Jumapili ndugu zangu.

Tumekuwa tukishuhudia katika vyombo vya habari vya kimataifa pale linapotokea tukio la kigaidi ama uhalifu ya aina yoyote ile basi wale wanaohusika picha zao huwekwa hadharani ili watu wawatambue. Hii husaidia sana Kurahisisha Kazi ya polisi kuwakamata.

Picha zinapowekwa wazi watu wanaowafahamu huweza kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kurahisisha ukamatwaji wa wahalifu hao. Haitoshi kusikia tu kwamba polisi imekamata majambazi kadhaa ama magaidi kadhaa ila itakuwa ni vizuri zaidi zikaoneshwa picha zao na majina zao pia.

Hii itakuwa msaada kwa Mimi kama raia mwema nikiona kuna taarifa naweza kutoa kwa polisi kwa sababu namfahamu Jambazi huyo. Kutuonesha silaha tu haitoshi inatakiwa watuoneshe na Sura za wahusika ili tulisaidie jeshi letu kupambana na uhalifu...

Note: Sifahamu kanuni za jeshi ya Polisi kama zinakataza ama kuruhusu kuoneshwa kwa sura za waalifu,hivyo mwenye ujuzi wa jambo hii tafadhali anielimishe.

Asante Sana na Nawasilisha.

[HASHTAG]#mckonjetv[/HASHTAG]
 
Kuna mtu wako humuoni, au katika walio uwawa hujui ni yupi kauwawa na yupi amekamatwa. Sidhani kama inaumuhimu kwako kukuonyesha watuhumiwa.
 
Wakishakamatwa picha haikusadii chochote.. polisi wanaweka wazi ya mtuhumiwa wa uharifu endapo anatafutwa
kama tunakata matawi ya mti hakuna tatizo ila kama tunataka kung'oa hadi mizizi ya matukio kama haya lazma majambazi wafahamike ili wanancbi wawareport na makundi ambayo jambazi alikuwa anajihusisha nayo sana.
 
Ajabu kuwa picha za askari wetu zilizagaa mitandaoni, picha za majambazi mpaka sasa hata 1 hakuna,
Hapa naona maigizo ya KDF yanakuja mpaka kwetu, huwa wanatoa namba tu za al shababu waliokufa bila ushahidi,
 
Kwenye ile nyumba police waliozingira sii waliwakamata majambazi yote unafkri waliweza kuwatoroka police wetu Imara?
 
Kuna mtu wako humuoni, au katika walio uwawa hujui ni yupi kauwawa na yupi amekamatwa. Sidhani kama inaumuhimu kwako kukuonyesha watuhumiwa.
Kama haina umuhim hakuna sababu ya wao kuwa na utaratibu wa kuonyesha watuhumiwa kama wanavyofanya
 
Ni kinyume cha misingi ya utawala wa sheria na haki za kijinai kuonyesha sura za watuhumiwa kwani hiyo inawahukumu kabla ya mahakama kufanya hivyo.
Ila polisi wanapaswa kutoa picha za washukiwa ambao bado wanasakwa.
 
Nu kinyume cha misingi ya utawala wa sheria na haki za kijinai kuonyesha sura za watuhumiwa kwani hiyo inawahukumu kabla ya mahakama kufanya hivyo.
Ila polisi wanapaswa kutoa picha za washukiwa ambao bado wanasakwa.
Miaka yote huwa wanatuonesha,na naamini ushawah kuwaona kupitia magazeti na T.V si majambazi tu hata watu wa rushwa na watuhumiwa wengine....ndo maana mdau ameuliza kwenye hili la Vikindu,na kwa ukubwa wa tatizo unaona wanaanzaje kutowaonesha kwa mfano?
 
Kuna mtu wako humuoni, au katika walio uwawa hujui ni yupi kauwawa na yupi amekamatwa. Sidhani kama inaumuhimu kwako kukuonyesha watuhumiwa.

Khasante mkuu....umemjibu kwa usahihi zaidi mana tiyari washakatwa hizo picha za nini?
 
Back
Top Bottom