IGP Wambura naomba tumia Mamlaka yako kuchunguza Utendaji Kazi wa Mkuu wa Kituo cha Polisi Tegeta

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Moja ya Sheria ya Jeshi la Polisi ni kuwa ikibainika Askari Polisi ametembea au ameingilia uhusiano wa mke wa mtu iwe ni Askari mwenzake au raia na uthibitisho ukapatikana bila kupepesa macho ajira yake ndio inakuwa imeishia hapohapo.

Kuna kesi kadhaa nyingi ambazo zimetokea siku za nyuma na hatua kali zikachukuliwa, nasema hayo kwa kuwa ninajua ninachokisema kwa sababu ni mmoja wa washiriki katika Idara hiyo ya Ulinzi (nadhani utakuwa umenielewa).

Kuna huyu bwana ni Mkuu wa Kituo cha Polisi – Tegeta ndani ya Dar es Salaam.

Kwa muda mrefu amekuwa ni mmoja wa watu ambao wamekuwa wasumbufu katika majukumu yao, ananyanyasa Watumishi walio chini yake kwa kutumia cheo chake.

Amekuwa akitumia vibaya madaraka yake, mfano amekuwa akiwatuma Askari wake kwa lazima kwenda kwenye mambo yake binafsi, wakikataa anaanza kuwafanyia figisu au anakuja juu.

Askari hawapendi na hawafurahishwi na kinachofanywa na bosi wao lakini kwa kuwa Sheria ya Jeshi ni kutii amri, hawana jinsi.

Kibaya zaidi ambacho kinatuuma ni tabia yake ya kutengeneza mazingira ya kutongoza na kuwa na uhusiano na wake za watu, hili linaweza kuonekana ni jambo binafsi au majungu lakini kwa kuwa lipo kinyume na Maadili ya kazi yake nimeamua kulisema.

Namuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura atumie watu wake au mbinu zake amchunguze huyu Mkuu wa Kituo, ili kama haya ninayoandika hapa ni majungu basi ayapotezee na kama ni kweli hatua zichukuliwe.

Kuna mengi ambayo anayafanya huyu Afande na yapo kinyume kabisa na suala la Utawala Bora.

Kama hatua hazitachukuliwa dhidi ya Kiongozi huyu nitarejea na kuweka picha na jina lake wazi ili Watanzania wamjue, japo najua kwa wasifu huo nilioutaja tayari mamlaka zitakuwa zimeshamjua ni nani.

Lengo langu si kumchafua bali ni kutaka Mamlaka zichukue hatua ili kuwa na utawala bora na uwajibikaji kwenye Jeshi letu la Polisi, sio kama huyu bwana anavyofanya, nimeamua kumstahi japo kidogo kuhusu kuweka wazi sura na jina lake.
 
Bwana Mohamed Mzelengi ndio mkuu wa Kituo hicho sio siri jamaa ni mzinzi sana tena na wake za watu. Huwatishia raia kwamba atawafungulia kesi ya jinai.

Huyo jamaa ni bora Serikali ichunguze suala lake ni baya na hatari. Mwanaume yeyote akilalama kuchukuliwa mke huwambia atamfungulia Jinai na kama mjuavyo yeye ndio mkuu wa kituo anaweza akakumaliza. AFANDE IGP tafadhali chukua hili suala.Tunafahamu pia huyu mtu anatumia majina ya Viongozi kutamba kwamba ana urafiki nao hakuna wa kumchukulia hatua.
 
Hii nchi ni shithole country, lalamiko hili very serious linalalama humu na sio wahanga kufanya push back, katiba mpya tuipiganie wote regardless utofauti wa itikadi zetu, katiba mpya itatuletea vyombo viwili hapa, IPID (hawa ni police wa police, hii issue inawahusu), PP huyu ana mamlaka ya kijudge,maagizo yake ni court binding, issue hii pia ingemhusu, ujinga, na upumbavu wa watanzania ndio kiini cha yote haya, one man manage to silence 5000 people's.
 
Hii nchi ni shithole country, lalamiko hili very serious linalalama humu na sio wahanga kufanya push back, katiba mpya tuipiganie wote regardless utofauti wa itikadi zetu, katiba mpya itatuletea vyombo viwili hapa, IPID (hawa ni police wa police, hii issue inawahusu),PP huyu ana mamlaka ya kijudge,maagizo yake ni court binding, issue hii pia ingemhusu, ujinga, na upumbavu wa watanzania ndio kiini cha yote haya,one man manage to silence 5000 people's

....manages.....siyo .....manage....
Jifunze sana grammar kijana.
 
Hii nchi ni shithole country, lalamiko hili very serious linalalama humu na sio wahanga kufanya push back, katiba mpya tuipiganie wote regardless utofauti wa itikadi zetu, katiba mpya itatuletea vyombo viwili hapa, IPID (hawa ni police wa police, hii issue inawahusu),PP huyu ana mamlaka ya kijudge,maagizo yake ni court binding, issue hii pia ingemhusu, ujinga, na upumbavu wa watanzania ndio kiini cha yote haya,one man manage to silence 5000 people's

And what is people’s?
 
Ukiwaambia hivyo hawakuelewi. Huyo analalamika kitu ambacho nina uhakika hata hao wanaopelekewa malalamiko wanafanya na si ajabu hata huyo amiri mkuu wa majeshi anaweza kuwa anafanya. Bila kubadilisha mfumo wetu na kuwa na viongozi wanaowajibika kwa wananchi ni bure.
 
Soma kuelewa SIO kuuliza maswali, matokeo ya shule za kata

Wewe kweli umesoma shule? Nisome kwa kuelewa nini kiingereza kichafu kama hiki? Tena unaweza kushambuliwa humu hadi unakimbia kama kenge! Kubali kufundishwa wewe, siyo unatuandikia takataka kama hizi na kujiita umeandika kiingereza!
 
Moja ya Sheria ya Jeshi la Polisi ni kuwa ikibainika Askari Polisi ametembea au ameingilia uhusiano wa mke wa mtu iwe ni a zichukue hatua ili kuwa na utawala bora na uwajibikaji kwenye Jeshi letu la Polisi, sio kama huyu bwana anavyofanya, nimeamua kumstahi japo kidogo kuhusu kuweka wazi sura na jina lake.
Kituo kile ambacho unapita Bar ya Lexus kwa mbele!? Kesho kutwa ntaenda pale kumtegeshea halima mishepu wangu, ngojea nirudi dar, atajifanya ana kesi fulani
 
Bwana Mohamed Mzelengi ndio mkuu wa Kituo hicho sio siri jamaa ni mzinzi sana tena na wake za watu. Huwatishia raia kwamba atawafungulia kesi ya jinai.
Huyo jamaa ni bora Serikali ichunguze suala lake ni baya na hatari.
Mwanaume yeyote akilalama kuchukuliwa mke huwambia atamfungulia Jinai na kama mjuavyo yeye ndio mkuu wa kituo anaweza akakumaliza. AFANDE IGP tafadhali chukua hili suala
AnawatombeRea wajinga tuh,mke anavyouma
 
Nyoosha taarifa, andiko limekaa kiroho mbaya tu! Yaani kweli kiongozi Mkubwa apokee na kuifanyia kazi taarifa kama hii.

Hapana HAKUNA mfanyakazi atakayebakia ofisini au sehemu yoyote katika utendaji.

Kwa ufupi kama ujumbe wako huu una ukweli wa wazi wenye nia ya kujenga.

Taja eneo, mfano wa vitendo vibaya, matukio kwa mifano aliyotenda, watu walioathirika na nk.

Isije ikawa ni kizingiti kwenu katika kufanya uhalifu.
 
Back
Top Bottom