Wana JF polisi mmoja akiwa katika uniform amepigwa risasi hadi kufa maeneo ya Arusha chini ya mti karibu na stand ya magari ya kwenda Kisongo, Kwamrombo.
Ilikuja gari aina ya RA4 ikiwa imewasha taa kisha baadhi ya magari yakapisha wakijua labda ilikuwa na dharura, lakini walipofika alipokuwa askari huyo alipokaa basi alishuka jamaa mmoja na kumpiga risasi kwa bastola kisha kuingia ndani ya gari na kutokomea kusikojulikana.
Hadi napost thread hakuna habari za kukamatwa kwa jamaa hao ambao haikujulikana walikuwa majambazi au walikuwa na visasi nae marehemu.
wakuu....hii story ya kupigwa risasi polisi nilivyosikia ni kwamba kuna majambazi yamemliza mfanyabiashara kiasi cha pesa ambacho mpaka sasa hakijajulikana.....mfanyabiashara huyo alikuwa anaenda kuweka pesa hizo CRDB bank pale uhuru road, wachizi wakamtokea, walipokuwa wapo njiani kukimbia wakakutana na huyo polisi hana hili wala lile katoka duka la hardware kununua anachojua mwenyewe.....wanaume wakajua huyu ni nuksi wakamuwahi.....kwa hiyo polisi amekufa bila kujua kilichomuua ni nini.....huku nyuma majambazi hao wakimuacha yule baba mfanyabiashara akilia barabarani kama mtoto mdogo.....kweli pesa ni maua....hunyauka na kuchanua
When a system in equilibrium is subjected to a change,the system will also try to change so as to halt the effect of that changes until stability is re-attained.Tazama Iraq,Afghanistan etc
Mambo ya kawaida binadamu kufa, mungu ndiyo kampangia afe kwa njia hiyo, nimeona kuna watu fulani humu wanataka kulikuza hili suala na kulifanya la kisiasa zaidi, mimi naomba tusiende huko. huwezi kujua sababu ya kuuliwa, labda alikuwa akichukua mke wa mtu, labda alikuwa akishirikiana kwenye biashara za magendo, labda labda, labda!...hakuna jibu hapa jibu lililobaki ni labda tu, hili suala tuwaachie wahusika.
ndo hivyo mkuu cdm wasiiingizwe tusiendelee kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu!
Umegundua eeeh! Afadhali hela yangu nikainywe sasa hivi kuliko kufikiri itajaa halafu watu wakaichukua kama yao siku moja.wakuu....hii story ya kupigwa risasi polisi nilivyosikia ni kwamba kuna majambazi yamemliza mfanyabiashara kiasi cha pesa ambacho mpaka sasa hakijajulikana.....mfanyabiashara huyo alikuwa anaenda kuweka pesa hizo CRDB bank pale uhuru road, wachizi wakamtokea, walipokuwa wapo njiani kukimbia wakakutana na huyo polisi hana hili wala lile katoka duka la hardware kununua anachojua mwenyewe.....wanaume wakajua huyu ni nuksi wakamuwahi.....kwa hiyo polisi amekufa bila kujua kilichomuua ni nini.....huku nyuma majambazi hao wakimuacha yule baba mfanyabiashara akilia barabarani kama mtoto mdogo.....kweli pesa ni maua....hunyauka na kuchanua
Mimi niko Arusha, habari tulizozipata ni kwamba wale walikuwa ni majambazi na wameiba kwenye duka la jirani na pale idara ya maji. Wakiwa wanaondoka wakamwona askari na wakahisi anaweza kuwadhuru, kujiwahi wakaamua kumpiga risasi. Yule askari alikuwa akisubili wenzake ambao pia walikuwa wapo ndani ya duka jirani na hapo.