Polisi angalieni haya maeneo

MAGARI7

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
2,401
1,303
Habari wana-jamii forums,

Nimeona kuanzisha uzi huu kwa ajili ya kupeana taarifa ya maeneo hatarishi nyakati za jioni/Usiku ilikuwa na tahadhari.

Mimi nianze na ile barabara ya 'mawasiliano tower'

(ile service road baada ya mawasiliano towers)

Eneo lile ni moja ya miongoni mwa maeneo hatari sana nyakati za usiku., kuna vibaka. Nimewahi kukuta tukio la mtu kagongwa na gari hadi kufa kwenye pulukushani za kupambana na vibaka waliokua wamekwapua pochi ya mwanamke aliekua nae.

Kwa kifupi ni eneo ambalo sio zuri.

Naomba mchukue tahadhari mnaopita kwa miguu eneo hilo nyakati za usiku.

Pia,

Tujuzane maeneo mengine ambayo ni hatari nyakati za usiku.

Nawasilisha.
 
Baada ya mawasiliano tower kuelekea wapi sasa mwenge au kuja ubungo..??
 
Baada ya mawasiliano tower kuelekea wapi sasa mwenge au kuja ubungo..??
Yaani ukishaumaliza ule ukuta wa mawasiliano towers tu, ukiwa unaenda mwenge (sana sana sana) ... na hata ule upnde wa wauza maua pia., nasikia sio pazuri kwa watembea kwa miguu nyakati za usiku.
 
mie ushauri wangu kwa maafisa polisi au mkuu wa mkoa waende kwa wenyeviti wa serikali za mitaa wanawajua vibaka wote wakwenye mitaa yao,waorodheshwe wote kwa majina wakamatwe hakika raia tutakaa kwa amani kabisa cc Mwigulu Nchemba
 
Mbona mmekaa kimya,? hamuwezi jua mchango wenu unaweza kuokoa maisha ya mtu kiasi gani.

Tuonyeshe upendo, tuonyeshe uzalendo kwa kupeana taarifa muhimu za maeneo hatari iliwatu kuchukua tahadhari napia hata vyombo vya usalama kuyaangalia maeneo husika ...
 
Acha uongo wenyeviti wa mtaa wanawajua vibaka kwani wanaendaga kuiba wote wewe na mimi twapasa kusaidia polisi pia uwezi kamata mtu bira ushaidi harafu usisahau kuwaumbua mashoga
 
Yaani ukishaumaliza ule ukuta wa mawasiliano towers tu, ukiwa unaenda mwenge (sana sana sana) ... na hata ule upnde wa wauza maua pia., nasikia sio pazuri kwa watembea kwa miguu nyakati za usiku.
Na kwanini utembee mwenyewe tu bila kujihami usiku huo
 
Na kwanini utembee mwenyewe tu bila kujihami usiku huo
Mazingira yake huonyesha kua ni sehemu salama, hivyo humuondoa hofu mtembea kwa miguu kupita. Lakini nimoja ya sehemu hatarishi sana.

Unajua kuna wanaokua wanatoka makazini kwao usiku,

Wauza bar etc, wengi ndiio hua nadhani wanatembea kubana matumizi (wakishuka ubungo)
 
Acha uongo wenyeviti wa mtaa wanawajua vibaka kwani wanaendaga kuiba wote wewe na mimi twapasa kusaidia polisi pia uwezi kamata mtu bira ushaidi harafu usisahau kuwaumbua mashoga
Kwanza, niambie huo uongo ni upi hapo.?!
 
Wana-jamii.

Naomba

Tushirikiane sote, kuorodhesha maeneo yote hatarishi hapa!
 
Back
Top Bottom