Usinunue kiwanja au kujenga maeneo haya

Annunaki

JF-Expert Member
Dec 30, 2021
1,911
3,171
Katika harakati za kujitafuta kimaisha na kuanzisha makazi ya kuishi kwa ajili ya yako mwenyewe/familia ni vyema kuepuka kuishi au kujenga makazi karibu na maeneo haya nitakayoyataja hapa kwani kuishi karibu na maeneo haya ni kujitafutia matatizo.

Usijenge au kuishi karibu na maeneo haya.

1. Hifadhi za wanyama, misitu.

Ikiwa unatafuta eneo la kuishi au kujenga eneo lolote lile ambalo linapakana na hifadhi ya wanyama au misitu siyo sahihi kwani unaweza kuhamishwa muda wowote ule kutoka katika maeneo ya hifadhi.

2. Kambi ya jeshi.

Usijaribu kabisa kuishi au kujenga karibu na eneo lenye kambi ya jeshi, ikiwa umejenga karibu na kambi ya jeshi, jeshi linaweza kuwataka muhame eneo hilo kutokana na shughuli zake. Usijenge karibu na kambi ya jeshi ni hatari kwa usalama.

3. Hifadhi ya Barabara
Kuna watu upenda kununua maeneo bila kutafiti, ikiwa utauziwa eneo lilipo kwenye hifadhi ya Barabara na Serikali ikaja na mkakati wa kupanua Barabara, utatakiwa kuhama na hutolipwa fidia yeyote ile.

4. Maeneo yanayopakana na migodi ya madini.

Usiwekeze sana katika maeneo hayo hata kama ni eneo lako, Ardhi yote ni mali ya Rais ,kwahiyo ikiwa Serikali itaona kuna uhitaji wa wewe kuhama ili kupisha shughuli za uchimbaji ni utahama tu iwe kwa kulipwa fidia au kutokulipwa. Ikubukwe kuna maeneo ambayo yameshapimwa kabisa, kwahiyo usinunue ardhi au kujenga katika maeneo hayo.

5. Mabondeni na kwenye miteremko mikali.

Kama unataka kujenga au kuanzisha makazi hakikisha eneo husika halipo kwenye bonde au mteremko mkali ili kuepuka athari za maporomoko ya udongo pamaja na mafuriko. Ni vyema kabla hujanunua eneo ktk maeneo ya hivi, upate historia yake kuhusu mafuriko n.k kwenye eneo husiki, ikiwa eneo hilo lipo bondeni.

6. Karibu na Mto, Bahari au Ziwa.

Usiweke makazi kabisa ktk mwambao wa meneo haya ili kuepuka athari za vimbunga, kupwa na kujaa kwa bahari, mito au maziwa. Kina cha mto, bahari au ziwa uongezeka na kupungua kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, unaweza kujenga leo then baada ya hata miaka 20 n.k nyumba ikasombwa na maji. Hapa wale waliowahi kuishi haya maeneo wanaelewa vyema.

7. Viwanja vya Ndege.

Usijenge au kununua kiwanja karibu na eneo lenye kiwanja cha Ndege chochote. Kuishi karibu na eneo hili ni kujitafutia matatizo kwana shughuli za uwanja wa Ndege husika uweza kubadilika muda wowote.

8. Maeneo yenye migogoro ya kiraia/Serikali.

Usijenge na kuishi katika maeneo haya utakaa uishi kwa amani na muda wowote unaweza kulazimika kuhama eneo husika kwa kulazimishwa au hata kwa hiyari.

Imeandikwa na Annunaki.

Niwatakie utekelezeji mwema wasomaji wote.
 
Usijenge na kuishi ktk maeneo haya utakaa uishi kwa amani na muda wowote unaweza kulazimika kuhama eneo husika kwa kulazimishwa au hata kwa hiyari.

Muki, hili ni jambo la wazi kabisa kama kusema leo usiku hapa Dar jua litakuwa limezama. Kwa kifupi ni hivi: watu wanaonunua maeneo kama haya wakati wa kununua, kwa sababu hii au ile, huwa hawajui kama ni ya shughuli hizo.
 
Kimsingi unapotaka kununue ardhi maeneo haya ni vyema ukatifiti vya kutosha hasa kuhusiana na baadhi ya niliyoyabainisha hapa.
 
Muki, hili ni jambo la wazi kabisa kama kusema leo usiku hapa Dar jua litakuwa limezama. Kwa kifupi ni hivi: watu wanaonunua maeneo kama haya wakati wa kununua, kwa sababu hii au ile, huwa hawajui kama ni ya shughuli hizo.
Hapo ndio kweny tatizo, yaani viwanja vimekuwa na migogoro bado watu wanauziwa sehemu za watu kama kambi za jeshi na wawekezaji.
 
Katika harakati za kujitafuta kimaisha na kuanzisha makazi ya kuishi kwa ajili ya yako mwenyewe/familia ni vyema kuepuka kuishi au kujenga makazi karibu na maeneo haya nitakayoyataja hapa kwani kuishi karibu na maeneo haya ni kujitafutia matatizo.

Usijenge au kuishi karibu na maeneo haya.

1. Hifadhi za wanyama, misitu.

Ikiwa unatafuta eneo la kuishi au kujenga eneo lolote lile ambalo linapakana na hifadhi ya wanyama au misitu siyo sahihi kwani unaweza kuhamishwa muda wowote ule kutoka katika maeneo ya hifadhi.

2. Kambi ya jeshi.

Usijaribu kabisa kuishi au kujenga karibu na eneo lenye kambi ya jeshi, ikiwa umejenga karibu na kambi ya jeshi, jeshi linaweza kuwataka muhame eneo hilo kutokana na shughuli zake. Usijenge karibu na kambi ya jeshi ni hatari kwa usalama.

3. Hifadhi ya Barabara
Kuna watu upenda kununua maeneo bila kutafiti, ikiwa utauziwa eneo lilipo kwenye hifadhi ya Barabara na Serikali ikaja na mkakati wa kupanua Barabara, utatakiwa kuhama na hutolipwa fidia yeyote ile.

4. Maeneo yanayopakana na migodi ya madini.

Usiwekeze sana katika maeneo hayo hata kama ni eneo lako, Ardhi yote ni mali ya Rais ,kwahiyo ikiwa Serikali itaona kuna uhitaji wa wewe kuhama ili kupisha shughuli za uchimbaji ni utahama tu iwe kwa kulipwa fidia au kutokulipwa. Ikubukwe kuna maeneo ambayo yameshapimwa kabisa, kwahiyo usinunue ardhi au kujenga katika maeneo hayo.

5. Mabondeni na kwenye miteremko mikali.

Kama unataka kujenga au kuanzisha makazi hakikisha eneo husika halipo kwenye bonde au mteremko mkali ili kuepuka athari za maporomoko ya udongo pamaja na mafuriko. Ni vyema kabla hujanunua eneo ktk maeneo ya hivi, upate historia yake kuhusu mafuriko n.k kwenye eneo husiki, ikiwa eneo hilo lipo bondeni.

6. Karibu na Mto, Bahari au Ziwa.

Usiweke makazi kabisa ktk mwambao wa meneo haya ili kuepuka athari za vimbunga, kupwa na kujaa kwa bahari, mito au maziwa. Kina cha mto, bahari au ziwa uongezeka na kupungua kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi, unaweza kujenga leo then baada ya hata miaka 20 n.k nyumba ikasombwa na maji. Hapa wale waliowahi kuishi haya maeneo wanaelewa vyema.

7. Viwanja vya Ndege.

Usijenge au kununua kiwanja karibu na eneo lenye kiwanja cha Ndege chochote. Kuishi karibu na eneo hili ni kujitafutia matatizo kwana shughuli za uwanja wa Ndege husika uweza kubadilika muda wowote.

8. Maeneo yenye migogoro ya kiraia/Serikali.

Usijenge na kuishi ktk maeneo haya utakaa uishi kwa amani na muda wowote unaweza kulazimika kuhama eneo husika kwa kulazimishwa au hata kwa hiyari.

Imeandikwa na Annunaki.

Niwatakie utekelezeji mwema wasomaji wote.
Duh nimejenga bondeni,karibu na kambi ya jeshi & Airport.

Itabidi niuze chap.
 
Back
Top Bottom