Polisi akataa hela yangu asema ni rushwa

Polisi akataa hela yangu asema ni rushwa

Manstone

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2013
Posts
516
Reaction score
315
Nikiwa natokea zangu asubuhi kutoka maili moja nikiwa kwenye IST yangu na kamvua kananyesha kwenda viwanja, kufika maeneo ya Kwa Yusufu Mbezi nikakutana na barrier ya trafic wakikagua magari yalikuwa yakipita.

Ilinipa mawazo kwa kuwa taa ya mkono wa kushoto mwa gari yangu imevunjika, baada ya trafic kukagua gari akagundua hilo kosa.

Basi nikashuka nikaongee asiniandikie faini,
nikatoa elfu 5 nikamwambia mkuu shika hii ya kubrashia viatu, acha acharuke unanipa rushwa!

Nikamwambia hapana hata mh. mtukufu Rais alisha sema elfu 5 hizi si mbaya mchukue za kuburashia viatu, kwa hasira ameamua kuniandikia faini.
 
Rushwa huwa wanaanza kuchukua baada ya kutimiza Masharti ya Makosa wanayotakiwa ku rekodi Kwa Siku

Kama unabisha pita jion then Chepuka eneo lake Halafu akukamate uone Kama hachukui Kwa kuwa tayari kishakamilisha idadi
 
...Kuna bosi wake mnoko hapo karibu pengine, maana si kawaida..
 
Uwe makini sana sio kila traffic officer anahitaji hiyo ya kiwi( kubrashia). Wengine ni walokole au wasabato wenye nia ya kwenda mbinguni hawanaga masihara, ni wabaya kweli kweli.
Wasabato na Walokole hawachukui Rushwa? Wanaochukua Rushwa ni wapi?
 
labda kama ni polisi wa Marekani au Uingereza....... kama ni poliCCM wetu waliojawa na njaa mwili mzima hiyo hela haiahwi.
 
Alikuwa hajakamilisha hesabu yake ya siku ndo mana akakutolea mkeka wa 30k
 
Ela yako mbuzi. Ukiona trafik anapokea pesa ndogo ujue ana njaa au ni dala dala. Kwenye dala dala huchukua hadi buku mbili.
 
Back
Top Bottom