Police Tanzania rushwa kinguvu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Police Tanzania rushwa kinguvu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kiby, Sep 10, 2012.

 1. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi ni wazi kwamba police wa Tanzania hawaombi tena rushwa bali wanawanyang'anya raia kila sent walio nao. Kuna police traffic wa Mbeya mjini wakiongozwa na mwenye jina la Siza huchukua gari ya polisi na kuenda kutega nje ya mji. Hasa hupenda kukaa eneo linaloitwa Kirongo. Kibaya zaidi huyu Siza huwanyanganya madreva leseni zao na kutokomea nazo. Jambo hili huwafanya madereva kuahirisha safari zao na kuenda kumtafuta. Mara nyingi hapatikani kituoni na hupigiwa simu kujua yuko wapi. Madreva humfuata na kutoa rushwa ya kuanzia elfu ishirini na tano na kuenda juu. Mwema fuatilia askari wako watatukausha hata damu miilini mwetu. Kwa IGP Mwema amelishika jeshi likaharibika hivyo? Mara lipige raia wasio hatia risasi, mara lipore watu pesa zao kinguvu tutakimbilia wapi? Source ya habari hii ni jamaa yangu aliyeko safarini huko Mbeya. Yamemtokea leo hayo ya Traffic Siza na amemtafuta baada ya kunyanganywa leseni yake kwa kutumia piki piki iliyomtoza sh. 10,000 na Siza alipopatikana kamdai jamaa rushwa ya sh. 25.000. Ambayo imebidi ampe kujiokoa asife njaa.
  Dereva mwenyewe analipwa sh laki moja tu kwenda safari yake ya Tunduma na kurudi halafu ndio anakumbana na zoruba kama hizo. Nauliza tena jamani tutafika? Nini basi kifanyike?.
   
 2. e

  emalau JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 273
  Trophy Points: 180
  Si Mbeya tu, hata hapa Arusha ndo hivyo. wametanda kila sehemu wakikuta huna kosa wanaomba kwa nguvu. Nilipofanya utafiti kidogo niliambiwa Mkuu Said Mwema anajenga apartment zake hapa Ars, kwa hiyo pesa inatafuta by hooks and crooks!
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Traffic nao wamepewa target ya makusanyo daily so ndo pressure iyo
  So wanapiga kama laki 2 kwa siku robo inaenda kwa serikali inayobaki ninyake pamoja na waliomtuma kuvaa ilo gwanda.
   
Loading...