kikurajembe Original 2015
Senior Member
- Feb 27, 2016
- 109
- 138
Wapendwa wana JF, habari za majukumu na poleni sana kwa majukumu ya ujenz wa taifa letu.
Leo nimeamua kuandika uzi huu kwa Mh.Rais JPM na Mh.Waziri Mkuu mchapakazi MKM. wana JF
Najua mambo mengi sana serikali yetu inategemea askari polisi kuyafanya ikiwemo jukumu kubwa la kulinda usalama wa raia na mali zao. Japo wakati mwingine askari wetu wanatumika kisiasa lakini basically leo sio concern yangu.
Tunajua sana pamoja na makosa wanayofanya polisi wetu kama binadamu.mengine kwa kuamriwa kufanya,mengine kwa kufuata sheria za kikoloni PGO-Police General Order ambazo tunalia nazo siku zote zibadilishwe ili wafunguliwe kwenye vifungu vya kuwabana sana lakini ni wazi kuwa askari wetu hawa wanateseka sana.
UPANDISHWAJI WA VYEO:
1.Askari amemaliza depo moja na wenzake wanaelimu sawa na pia hana mashitaka yoyote ama ya kijeshi ama ya kiraia kwenye faili lakini mmoja anapendekezwa cheo mmoja anaendelea kubaki constebo wa kudumu over five to ten years.
2.Askari mwingine ana masters na mwingine ana certificate ya vehicle inspectors anatokea traffic na usajent au hata umeja wanateuliwa wote kwenda kozi ya nyota moja,baada ya mwaka mmoja yule mwenye certificate ya vehicle inspetors kwa kuwa anajuana na wakubwa wengi anapelekwa GO akawe gazette officer-(afisa wa nyota tatu) na yule mwenye masters yake aliyesoma kwa shida na tabu nyingi mototo wa mkulima maskini anabaki na kanyota kake kamoja mkaguzi msaidizi au mkaguzi. mwenye certificate anakuwa bosi wake hata miaka haijapita.
Tena anawasifia wenzake hawa wazee bhana bila kuwaona hufanikiwi utasota na kanyota kako kusubiri utaratibu wa miaka mi3.wakati huo mwenzake hana nguvu ya kuwaona wakubwa kwakuwa hayupo kitengo cha traffic au chenye maslahi.Sasa huyo mwenye certificate anaenda kuwa OCS yani mkuu wa kituo cha polisi mahali anaongoza askari wa vyeo vya chini wenye elimu zaidi yake.
Matokeo yake tunaona wanapokea order kutoka kwa viongozi wa juu wanatekeleza "differently" hana leadership skills,management skills na pia ana lack knowledge ya how to manage people at work. Strategic management.hivyo anashindwa kutekeleza majukumu yake anaongoza watu kwa cheo tu.
Wakati mwingine wanakamata watu kwa amri ya ocs wanafikishwa mahakamani halafu watuhumiwa wakiweka wakili askari wetu,wanakosa ushahidi,wanashindwa kujenga hoja mahakamani serikali inashindwa kesi.
Tumetumia magari ya polisi kupeleka watu mahakamani,mbwembwe,vitisho kesi wanashindwa kwenye"hearing" askari anafanyiwa "cross examination" na wakili,haji mahakamani mpaka hakimu au jaji anaondoa jalada mahakamani.kila siku upelelezi unaendelea.Pengine mtuhumiwa alikamtwa kwa kupigwa,kuteswa,kudhalilishwa mbele ya familia yake,ama marafiki na hata kuumia sana. Hiii inatia doa serikali yako Mh.na askari wetu wanajenga uadui mkubwa na raia.
KUTOLIPWA STAHIKI ZAO KULINGANA NA VYEO WALIVYOPANDISHWA:HILI NI JIPU KUBWA:
Msione kimya mkazani ni salama,hao askari wetu wanaofanya doria usiku kucha na mchana na pia tunaojivunia nao kwa kutoa kauli "uchaguzi utakuwa huru na haki askari wetu wako timamu watalinda usalama kwenye vituo vyetu",je mmewalipa stahiki zao?
Askari alikuwa na cheo cha sajent au meja anapandishwa cheo cha mkaguzi msaidizi tangu mwaka 2008 analipwa mshahara wa meja na yeye ni mkaguzi. Mwingine alikuwa constable akaenda (PSI) mkaguzi msaidizi tangu 2010.akapandishwa tena mkaguzi kamili analipwa mshahara wa conteble mwenye degree,ama wa meja au RSM mpaka leo 2016.
Mwingine alikuwa mkaguzi amepelekwa GO kawa officer tangu 2009 mpaka sasa 2016 analipwa mshahara wa inspector-mkaguzi.Viongozi wote wa jeshi la polisi mpo kimya.business as usual.Jambo hili lilikuwepo tangu kipindi cha IGP Mahita,Mwema na sasa kwa IGP Mangu.
Hawa askari ni nani atakae wasemea matatizo yao na wao wamefumbwa midomo na PGO ya kikoloni wasiweze kuhoji hatakama wanakandamizwa? Askari anakwenda makao makuu ya polisi kuulizia mbona alipandishwa cheo mika mitatu iliyopita akiwa rank & file sasa ni mkaguzi msaidizi au mkaguzi analipwa mshahara wa constable.Hata wa bachelor degree yake hapati.
MAJIBU: Nenda kasajili vyeti vyako huko kwa OC-CID/OCS/OCD/RPC au Mkuu wako wa chuo kama ni wale wa mavyuoni.Ukumbuke waliomruhusu kwenda chuo ni wao,na aliporudi alisajili vyeti tayari anaambiwa vyeti vyako hatuvioni kwenye faili.
Ama barua yako ya kupandishwa cheo hatuioni kwenye faili lako.hapo yupo masijala.PHQ.anayetoa majibu anachezea simu yake ya smart phone wala hamuangalii usoni.mwenzie katoka pengine vituoni au mkoani kufuatilia maslahi na kapewa muda anamajukumu kama yeye tena ya huyu wa kituoni au mikoa ya kipolisi yupo busy sana. Au "nenda kule hazina kafuatilie mwenyewe watakupandishia mshahara wako" Mwingine anasema "aah mimi nilimuona fulani nikampa nanihii kidogo yaani mwezi huohuo mshahara wangu wa uofficer nimelipwa".what is this?
Sasa kama mtu ni OCS bado analipwa mshahara wa A/Insp. miaka zaidi ya mitatu kwa nini asiwaambie askari wake fungeni watu kumi mashati leteni kituo,wanapewa charge ya uzembe na uzurulaji,halafu wanapewa nafasi ya mwisho kuongea na ndg zao kwaajili ya zamana,wanakuja kudhaminiwa kwa 30,000 alfu kila mmoja,hiyo utaita ni rushwa au ni ubunifu? na huko barabarani is the same.kweli tunasema tutapunguza ama kuondoa rushwa ndani ya jeshi la polisi wakati viongozi wapokimya makamishina na mkuu analipwa vizuri bila kuangalia maslahi ya askari wetu ambao ndiyo watendaji na wanao muweka mkuu pale juu?
MAPENDEKEZO YA UTATUZI WA MATATIZO HAYA YA ASKARI WETU:
Plan"A" kwa upandishwaji wa vyeo:
Katika upandishwaji wa vyeo kama viongozi wataamua kuwapa watu wao vyeo kwa kufuata umri mkubwa kazini lakini elimu haitoshelezi au kidugu ama kujuana.Muishie vyeo vya RANK & FILE lakini kwa majukumu ya kuwa kiongozi wa kitaifa ambao barua inatoka kwa amiri jeshi mkuu,wapendekezeni/wapeni wasomi,nchi hii kwa sasa imebadilika sana wananchi hawaburuzwi kama zamani.
Plan"B"
Kama ni lazima kuwapa vyeo vya juu mfano uofficer walikuwa na elimu iliyopelea kwa kigezo cha miaka mingi jeshini,basi msiwape majukumu ya kufanya maamuzi
Plan"A" kwa ulipwaji wa stahiki zao haraka:
Askari anapopendekezwa cheo cha ngazi ya ukaguzi au gazette officer-GO,majina yanatoka kazini kwake na kwenda makao makuu ya polisi na kufikia wizarani,na mchakato kufikia utumish na mwisho kwa Rais na kisha kusainiwa na kurudishwa kwa katibu mkuu na kurudi kwa IGP.
Hapo askari husomewa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania amewapandisha vyeo askari wafuatao.......Kwanini kopi au nakala ya majina ya wale waliopandishwa vyeo isiende hazina waandaliwe mishahara mipya? ili wakimaliza mafunzo tu wapate mishahara yao mipya kuliko kuwaambia wafuatilie mishahara mipya kama vyeo walijipandisha wenyewe?
Plan"B"
Hivi kweli kwa muda wa miezi sita wakiwa mafunzoni na wengine huwa wanaenda kozi ya miezi tisa second-commander.muda huo office ya Inspector General PHQ mishahara wakishirikiana na hazina wanashindwa kuwaandalia hawa askari mishahara mipya pamoja na muda wote wa mafunzo huo,mpaka wanarudi na kupangiwa new post na pia wanakaa miaka mitatu mpaka mitano huu kweli ni ubinadamu sio unyama?
Kinadharia amiri jeshi mkuu anapopandisha watumishi wa umma mwezi huohuo anatakiwa kupata mshahara mpya.Hayo mafunzo ni mbwembwe tu jins ya kwenda kufanyakazi katikanafasi yako mpya.Tumeona mawaziri alisema nimewapandisha vyeo kwa kuwateua kuwa mawaziri lakini hamna semina elekezi mtajifunza humohumo.Je na wao wangepaswa kucheweleshewa stahiki zao?
NB: Tusikimbilie kuwapa vitendea kazi vizuri magari ya doria,virungu,silaha,na ya maji ya kuwasha na kila kitu wakati hawana makazi mazuri,na pia wanalipwa mishahara kidogo.madeni kibao,kukopa mkopo wa nyumba za nssf au pspf au watumish housing ile sijui ma ya tatu,kiwango cha makato ya bot hakidhi.mkopo wake anaishia kununua chaser old model mil.3,mwingineananunua kiwanja hawezi kujenga akiishiwa anakiuza anakwenda kulewa pombe basi yaishe..TUACHE LAWAMA NA MANENO YASIYOKUWA NA UZALENDO KWA ASILIMIA KUBWA POLICE HAVE DONE EVERYTHING IN THIS COUNTRY (source polisi wenyewe) nawakilisha,
Tuchangie kwa hoja bila vyama na maneno matupu na lugha za kuuzi