Traffic police officers wa Arusha mnalidhalilisha jeshi, mnaomba mno rushwa

mandella

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2011
Messages
2,905
Points
2,000

mandella

JF-Expert Member
Joined Oct 29, 2011
2,905 2,000
Aisee inakera bana. Hii ni too much, nasema tena hii ni TOO MUCH. Ni experience mbaya sana ndani ya mkoa huu.

Juzi nimeombwa Elfu tano na Traffic zaidi ya Mara tatu kwa Siku moja,na hapo ni ndani ya mji, nikawa nawagomea wote, sasa mmoja akang'ang'ania leseni yangu katika mabishano akabadili kesi kuwa eti nimevuka Zebra.

Nikamuuliza mbona ulivyonikamata hukuniambia kuwa nina kosa, kwanza nikamcheka kwa dharau, na mimi nikamuuliza pale nilisimama au sikusimama embu kuwa mkweli?

Akajibu ulisimama Ila kuna watu walikuwepo hapo, nikamuuliza kama nilisimama na hawajaruka je lilikuwa ni jukumu langu kushuka na kwenda kuwavusha. Akasema kwa hilo Utajua wewe ngoja uichangie serikali, akanipiga fine.

Kumbuka hapo kulikuwa na watu wamesimama wanapiga zao story hata hawana habari ya kuruka. Nilimlaani tu na kumwambia mafanikio yako ni machache mno kwenye maisha ya baadae.

Nikaondoka, ila sababu ya yote ni kumnyima anachookiita hela ya lunch.

Wakikusimamisha wanakutupia Kijitabu au Note Book, wanakuambia Weka Chochote huko.

Najiuliza Hivi vitabu na Note books wanazishika za kazi gani? Hivyo ndio vikapu vyao vya Kuwekea Rushwa.

Halafu wapo wengi mno ndani ya mji! Wasambazeni embu ikiwezekana wasambazeni huko Kigoma Mtwara na miji mipya mingine.
 

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Messages
4,501
Points
2,000

Mad Max

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2010
4,501 2,000
Mjini Dar tunaelewana maisha yanaenda. Sometimes bora kutoa 5,000 kuliko kuandikiwa 30,000 ambayo ukijisahau inafika hadi 60,000
 

mkorinto

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Messages
14,183
Points
2,000

mkorinto

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2014
14,183 2,000
Usitoe wala kupokea rushwa.

Lipa malipo halali upate risiti halali ya serikali.

Usitishwe na kuomba kwao,lipia 30 chukua zako risiti sepa.
 

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
52,879
Points
2,000

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
52,879 2,000
Ukishakuwa umeajiri watu waliochukua tu kazi vile wamekosa options nyingine za kazi hayo ndio matokeo yake
 

evonik

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2015
Messages
2,249
Points
2,000

evonik

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2015
2,249 2,000
Wajomba wanasaka hela wale hatari, hata kama huna kosa wanaweza kwambia hata hujapasi Nguo toa faini
 

molwe

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2015
Messages
253
Points
250

molwe

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2015
253 250
Yaani hawa wanatakiwa wapewe pesa za chuma ulete!! Anapokea elf 5!! Anapoteza laki na kuanzia hapo hell zoote anazokusanya zinageuka makaratasi!!
 

mkorinto

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Messages
14,183
Points
2,000

mkorinto

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2014
14,183 2,000
Unafikiri kwa mtindo unatakuwa unamkomoa nani? wale jamaa hawakosi kosa kabisa
Kumbe sasa kosa linakuwepo sio la kubambikiwa.

Unajua tunashindwa kukubali kwamba ni kweli vifaa vyetu vina matatizo kila siku, basi traffic police watumie busara na utu.ila tunalazimisha ionekane wanatafuta makosa ili wapewe kitu kidogo.


Sasa kwa sisi watu wa kufikiri kwa namna tofauti,tunawaza iwapo tatizo ni traffic kukusanya elfu 5 5 zetu kila siku kwa makosa ya kutafuta,basi ni vyema tusiwape hizo elfu 5,nali 30 kwa kosa hilo na kudai risiti,tutakuwa tumewakomoa kabisa ,watakufa njaa.
 

Forum statistics

Threads 1,381,430
Members 526,097
Posts 33,800,008
Top