George Jinasa
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 399
- 58
Mimi sidhani hata kidogo kwamba kama kuna polisi wangapi au raia wangapui wameuwawa ni jambo la kushabikia. Watanzania naona tumeanza kuwa na fikra ambazo hatufanani nazo. Mambo yaliyotokea Arusha ni ya kusikitisha bila kujali kama amekufa polisi au raia. Polisi na raia wote ni wanaadamu na wanahaki ya kuishi.
Siwezi kusema kwamba Chadema hawakuwa na makosa wala polisi hawakuwa na makosa maana haisaidii sana maana kama damu imeshamwagika. Cha msingi ni kujadili namna ya kuzuia yasitokee tena. Ili tuweze kuwa kwenye nafasi ya kujadili hili lazima tusikitike kwa yaliyo tokea Arusha. Kama tutachekelea kwakuwa polisi mmoja alikufa au raia watatu walikufa hatutakuwa kwenye nafasi ya kukomesha hilo. Kwa maoni yangu, hamna polisi anayependa yatokee kama yaliyotokea.
Ni mhimu kwa raia na polisi tukazingatia sheria. Ni mhimu pia raia tukaheshimu vyombo vya dola. Ni kweli kwamba hamna aliye juu ya sheria. Hata hivyo, sheria zetu licha ya mapungufu yote zina taratibu ya kuwashughulikia wanaovunja sheria hata kama ni askari. Kesi ya Zombe imetoa fundisho kubwa na imeandika historia. Haki ya kukusanyika na kufanya maandamano ni ya msingi. Na haki ya wananchi wengine wasio na maslahi na maandamano kutopata usumbufu na madhara yatokanayo na maandamano ni ya msingi pia. Kati ya haki hizi kinzani sheria inajaribu kuweka mizani ili kurinda haki zote kwa busara. Ni kutokana na ukweli huu ndio maana kwa wakati mwingine kila upande unapaswa kuvumilia pale ambapo ni lazima haki ya wengine ikatekelezwa licha ya madhara madogo madogo wanayoweza kuyapata. Bila vyombo vya dola kama vile Mahakama, polisi na magereza haki kama hizi haziwezi kupatikana. Siamini kama kulikuwa na uharaka sana wa Chadema kuandamna siku hiyo hiyo. Kama polisi walikuwa na wasiwasi wa usalama katika siku hiyo pengine amani ingekuwepo kama viongozi wa Chadema wangeyaahirisha maandamano kuwapa nafasi polisi wajiandae kiusalama na kuyafanya siku nyingine. Kama mwenyekiti au katibu angetoa maelekezo hayo sidhani kama yangepingwa na wanachama. (I stand to be correcte)