Police Central Dsm, Kwanini watuhumiwa wakae shimoni zaidi ya miezi miwili!?

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,519
7,556
Ndugu yangu ametoka shimoni (mahabusu) muda si mrefu.
Cha ajabu kuna watu nilikuwa siwaoni mtaani na ikawa inasemwa wamekamatwa na wako shimoni. Yaani hawajapelekwa mahakamani tangu wakamatwe.


Mmoja wa Ndugu hao anaitwa Paskali( sio Mayalla). Ingekuwa ana kesi na amekosa dhamana mahakamani wala sio tatizo lakini miezi zaidi ya miwili yupo huko na hakuna kupelekwa mahakamani.

Huu ni ukatili uliopitiliza.
 
Kuna watu humu kwa uwezo wao mdogo wa kufikir watawatetea polisi kwa vitendo vya ajabu wafanyavyo
 
Wananchi wanapenda kunyanyaswa ndo maana wacha wafanye wanavotaka sisi ni wapuuzi kupita dunia nzima ndo maana mungu katukusanya tanzania tuteswe huku tunashangilia " a dead nation"
 
Mhh pole yake Paskali haya mambo yanakuaga na kukomoana...unakuta aliyekamatwa hana kesi ya msingi kumbuka kisa cha LEMA, Mbunge wa Arusha.
 
Polisi wa nchi hii ndio maana huwa staki hata urafiki nao, jamaa wamelishwa roho mbaya ajabu na watawala!
 
Hawa watu ni waonevu sana yaani huwezi ukawa polisi halafu utende haki lazima udhulumu tu ni kazi ya laana ukiona mwanao anataka kuwa polisi mwambie aache mara moja siyo kazi
 
Nenda mwone mwenye fail mwambie kuna m1 hapa uone kama mchana huu hautakua na ndugu yako sinza
 
Halafu naskia hapo shimoni wanachanganywa wakiume na wakike, ndugu yangu aliwekwa hapo, inauma saana
 
Mmoja wa watu hao ni Paskali.

Mmoja wa Ndugu hao anaitwa Paskali

Kama huyo Paskali ni huyu wa JF basi wacha aonje joto ya jiwe. Nafikili kuanzia sasa tutaongea Lugha moja. Maana amekua mstari ya mbele kutetea mpaka visivyostahili.
 
Ndio maana Paskali Mayala nilikuwa simuoni huku jf kumbe yuko shimoni
Una uhakika ndiye yeye.... Kwa jinsi anavyopenda kulamba niguu YA wakubwa askari wanaweza kumrukia kweli au yule na yeye ujanja wake upo nyuma ya keyboard
Polisi wa nchi hii ndio maana huwa staki hata urafiki nao, jamaa wamelishwa roho mbaya ajabu na watawala!
Mm kuna siku natokea dodoma Kufika maeneo YA kibaigwa askari wakanisimamisha walikuwa wanamuombea mwenzao lifti ahaaaa niliwakataaa..... Askari hawana ubinadamu mm siwez weka urafika na askari never ever..... Dakika moja anakukana Alafu wanapenda mteremko Sana....... Mm askari hapandi kwenye gari yangu labda niwe na pick up nitamuweka nyuma mbele Aslan akai
 
Back
Top Bottom