Nusrat Hanje na Twaha Mwaipaya wapo gerezani zaidi ya miezi miwili kwa kinachodaiwa ‘Kuharibu wimbo wa Taifa’

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Katibu Mkuu wa BAVICHA, Nusrat Hanje na mratibu wa uhamasishaji taifa, Twaha Mwaipaya wapo gerezani zaidi ya miezi miwili kwa kile kinachodaiwa kuharibu wimbo wa taifa kwa kusema "Mungu ibariki CHADEMA, wabariki viongozi wake"
_
Pamoja na kwamba kesi yao inadhaminika lakini mahakama mkoani Singida imewanyima dhamana. Yani watu wanateswa miezi miwili gerezani without any serious offence. Hawajaua, hawajaiba, hawajahujumu uchumi, hawajatakatisha fedha. Eti wamesema "Mungu ibariki CHADEMA, wabariki viongozi wake". Hilo ndio kosa linalowafanya wasote gerezani hadi leo.

Waliokamatwa na nyara za serikali na silaha za kivita huko Shinyanga wanapeta uraiani, lakini waliosema "Mungu ibariki CHADEMA" wanasota gerezani eti wameharibu wimbo wa taifa.

Mbaya zaidi Jamhuri inadai upelelezi haujakamilika. Kwahiyo watuhumiwa wanapandishwa mahakamani kesi inatajwa na kurudishwa gerezani (kesi haijaanza kusikilizwa). Hawapewi hata nafasi ya kujitetea kwa sababu eti upelelezi haujakamilika. Kwahiyo "uzembe" wa Jamhuri kushindwa kukamilisha upelelezi mapema, unawafanya watuhumiwa kuendelea kusota gerezani. Very unfair.!

Kwanini kama upelelezi haujakamilika wasiachiwe kwa dhamana, ili Jamhuri iendelee na upelelezi wake watuhumiwa wakiwa nje? Na kwanini Polisi ikamate watu bila kuwa na ushahidi wa kutosha? Miezi miwili mnapeleleza nini, wakati video yenye maneno waliyosema mnayo? Huu ni UONEVU unaopaswa kupingwa na kila mtu anayependa HAKI.

Leo siku ya 62, mmoja wa watuhumiwa Twaha Mwaipaya amempoteza baba yake mzazi akiwa gerezani. Kwa uchungu mkubwa ameandika ujumbe huu;

"Salaam, Kwa masikitiko makubwa nawatangazia kifo cha Baba yangu mpendwa, Yassin Abdallah AH. Mwaipaya. Taarifa niliyosoma kwenye Gazeti nikiwa Gerezani, nimeumia sana kukosa kushiriki msiba huu, najua ndugu zangu wameumia zaidi, ila Mungu ana mapenzi yake.

Nimeshindwa hata kuona mwili wake kwa mara ya mwisho, Gereza limenitenganisha na mpendwa wangu. Ningekuwepo ningeweka hata mchanga kwenye kaburi lake, ningeshiriki kubeba jeneza lake lakini hila za watawala zimenikosesha ibada hii ya mazishi ya Baba yangu. Nashindwa kuandika zaidi, machozi yanaloanisha karatasi.

Twaha Mwaipaya
Mahabusu siku 62"
 
Nchambi kafanya kosa kakiri kalipa fine,na hao wahuni wa chadomo wamefanya makosa hawataki kukiri sasa wanamlilia nani? Mwanakulitafuta mwanakulipata
Kama mimi nina undugu na hao wanaoteswa,unadhani nikipewa means ya kulipa kisasi nitasita kufanya hivyo?Hapa sina undugu nao lakini nimeumia na kuguswa hivi,nawaza kwa ndugu wapendwa wao ikoje!

Ugaidi huanza hivi hivi,unapandikizwa chuki halafu anatokea mtu anakuwezesha ili ulipe kisasi,unajiondoa na vichwa hata 30 vya watesaji au wapendwa wao!!

Haki huinua taifa!
 
Back
Top Bottom