Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to know!

Kweli karne hii Bado binadamu tunafanyiana haya utadhani enzi ya utumwa kumbe waafrika wenyewe tunaumizana na kuuana kama punda ndio tunaita nchi ya amani sisiemu wauaji wakubwa kabisa..
 
Ndugu Tumaini Makeni!! Usiweke chumvi katika kidonda ambacho kingali kibichi ,Hivi Unajisahaulisha kwa makusudi au ni kwa bahati mabaya ?matokeo hayo ni madogo sana ukilinganisha na yale yaliyobarikiwa na Rais Benjaman Mkapa alipoamrisha mauwaji ya raia kule Zenj na kutamka bila huruma kwa kusema hata kama kuna uwezekano wa kuliwa nyamazao zao basi zilewe , wanajeshi hao hao ndiwo walipewa hiyo amri na kukamilisha magizo ya Rais mkapa ,baada ya kufanya mauwaji na Ubakaji walipandishwa Vyeo kwa mbwebwe na Rais mkapa ,haikumalizikia hapo kuna baadhi ya Ndugu zetu kutoka Tanganyika iliwauma sana lakini pia kuna wale ambao udugu wao ni wa kitu na sio wa utu walifurahishwa sana na magizo ya Rais mkapa kwa jeshi zidi ya wananchi wa Zenj ,hatutasahau hilo Rais mkapa alikumbuke tumepoteza baba zetu wajomba zetu ,kuna wanawake hadi leo ni wajane na watoto ni yatima mkumbusheni Mpaka (mtaka Unda haneni)

Sonara

Unyama wa serikali ya CCM ni mwingi. Sijasahau huo unyama waliofanyiwa Watanzania wa Zanzibar! Ndiyo maana tunasema serikali hii ilipaswa kuwa imeng'oka!
 
Vipi ingekuwa ni wewe au mzazi wako ungeyasema haya????? Au kwa wengine ni sawa maumivu ambayo wameyapata watu si ya kuyasema ukiona mtu anaunga mkono anafikiri siku moja hayatampata. Ukiyaona kwa mwenzio kemea ukifikiri ni kwa wengine tu subiri siku yako


Nani kaunga mkono mh? tunataka tuone video za huo unyama tulioambiwa, vinginevyo hii tuliyo iona hapa kwa wanajeshi hayo ni mambo ya kawaida huko kwao, kurushwa kichura!!
 
Nani aliruhusu jeshi kufanya operesheni ya kiraia? Je Jeshi la Wananchi liliamuriwa kwenda kupambana na wananchi? Je Jeshi linaweza kuingia kwenye operesheni au vitani bila maagizo ya Amri Jeshi Mkuu? Je ni kweli vijana waliokwenda kwenye operesheni hawakuwa wamelipwa fedha zao (walikopwa?), wakawa na hasira?

Je ni kweli wamekuwa na manung'uniko mengi hivyo wakaamua kumalizia hasira zao kwa wananchi? Je ni kweli kwamba hakukuwa na mkakati wowote wa ku-manage hili suala, hivyo lilifanywa kwa kukurupuka?

Kuna maswali mengi mnastahili kuwajibu Watanzania kabla hamjatumia kisingizo chochote kile kuhalalisha mauaji na unyama huu.

mwenye majibu mazuri kwa maswali haya ni rais wa jamhuri ya tanzania, mheshimiwa dr mrisho khalfan jakaya kikwete! si yeye ndiye amiri jeshi mkuu wa majeshi ya tanzania? alishasema mtakatwa mapembe!
 

Like Sabibo Camp like Operesheni Tokomeza. Na hii ni just a drop of ice berg...unaweza kupata wakati mgumu kujiuliza kwa nini hadi sasa serikali haijawajibika kikamilifu katika unyama huu waliofanyiwa Watanzania.

Hivi unaweza kujiuliza kwenye hizo kambi vingapi hatujavijua vilifanyika? Kama hadi sasa, kwa mujibu wa Tundu Lissu akihutubia mkutano wa Shelui na Gervas Mbasa akihutubia Nanga, wapo watu tena akina mama walipigwa misumari ya nchi sita masikioni, wanaume walilazimishwa kufanya mapenzi na miti hadi wamalize haja zao, wengine wakatiwa chupa na misumari sehemu za siri. OMG! Mangapi hatuyajui!

Shameful condition...but they should know exactly, no condition is permanent (The State of Africa; A History of Fifty Years of Independence [Martin Meredith].
Mhe. Hebu angalia hii na itasaidia wanasiasa wetu (BOFYA) kuanzia kwako MKUU
 
Sema na wewe Victoire tukisema siye wengine tunaambiwa aahhh! CHADEMA hao hawaoni bora lolote nchini, sasa kama hakuna kitu bora nchini tukisema ni kosa!?

Dah,jamani hao ni binadamu au?
 
Last edited by a moderator:
kiukweli inaumiza sana. kabla ya kuchangia chochote inabidi tujiulize maswali kadhaa, la sivyo tunaweza kuwalaumu watenda na watendewa kimakosa. Ndugu zangu Tanzania ya leo inaongozwa kisiasa zaidi ndio maana haya yote yanatokea. kama kweli watendwa katika video imethibitishwa wamehusika na ujangili basi adhabu waliyopewa wamestahili. swali la kujiuliza, je adhabu waliyopewa inawahusu wao moja kwa moja au kuna wakubwa nyuma ya pazia?!
 
Wacheni fitna, hayo si mazoezi tu hata mgambo wanafanya. Watu mmekaa kupiga siasa lakini hamna nia ya kufanikisha chochote zaidi ya kutafuta madaraka. Kila siku kusifia rwanda mnadhani kagame amekalia kupiga siasa? Kama tumesema ni operation maaluum sasa mlifikiri nini kinafanyika ili kubaini mtandao wa majangili.
 
Hii inanikumbusha wakati nikiwa JKT!.

Serikali ya CCM imeishanawa mikono ya kisiasa kwa sasa kwa kuyatenda mapendekezo ya tume ndogo ya bunge kama ilivyoshauri katika mapendekezo yake.

Hizi hoja zingine za kisiasa kwa sasa zinajibika kwenye majukwaa ya siasa.

CCM na serikali yake utawasikia kwa sasa wanasema "Rais amefanya kama wabunge walivyoshauri na serikali inaendelea na uchunguzi ili iwawajibishe na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria wale wote walifanya uharifu kisheria" Finito.

Nilipatwa na mshangao kwa nini tume ya bunge haikumpa Rais wetu food for thought kwa kutoa mapendekezo na kumshauri ili Mkuu wa polisi, Mkuu wa majeshi na wakuu wa kitengo cha TANAPA awawajishe badala yake wakaja na option ambayo kwa Rais kutoa uamuzi kwake ni cup of tea.

Huu ni upepo na utapita-kauli mbiu ya serikali.
 
Maudhui ya operation si mabaya,ila utekelezaji Ulikuwa kinyume chake.Hapa kuna tatizo kubwa la ukosefu wa mbinu za kuhoji watuhumiwa,hali hii hupelekea askari wetu kufanya kazi ki analogically zaidi kuliko ki digitally..AMA kwa lugha nyingine wapo too political and not scientific. Something must be done,hata wabunge wetu wanayumba tu,hawalitambui hili,watafute solution na si kupiga Keller tu mawaziri waondoke,wataondoka wangapi Kama hakuna mbinu za kupambana na mbovu ya Wana jamii? Wahalifu wamepata loope hole ya kuendelea na uovu wao,hakuna mbadala wa kuwazuia maana kelele za haki za binadamu zingali zinatawala.
 
Wacheni fitna, hayo si mazoezi tu hata mgambo wanafanya. Watu mmekaa kupiga siasa lakini hamna nia ya kufanikisha chochote zaidi ya kutafuta madaraka. Kila siku kusifia rwanda mnadhani kagame amekalia kupiga siasa? Kama tumesema ni operation maaluum sasa mlifikiri nini kinafanyika ili kubaini mtandao wa majangili.

Kwa hiyo kwa ujinga huu wa kufikiri kwako, wale mawaziri waliojiuzulu kwa shinikizo la siasa za watafuta madaraka? Ulisoma ripoti ya bunge inayohusu kampeni hii ya tokomeza? Kula ugali wako ukalale, usiandike ujinga kwenye jambo ambalo linahuzunisha taifa zima! Shame on you!
 
Ni kama nchi isiyokuwa na central Government!

Mara nyingi watoto wakimlilia baba yao kwamba mama wa kambo anawatesa hawezi amini kwa sababu mara nyingi baba anazurura kwenye vilabu vya pombe hashindi nyumbani na watoto akajua wanaishije
 
Mara nyingi watoto wakimlilia baba yao kwamba mama wa kambo anawatesa hawezi amini kwa sababu mara nyingi baba anazurura kwenye vilabu vya pombe hashindi nyumbani na watoto akajua wanaishije
Yaani wewe acha,watu waliteseka sana!
 
Nimesoma comments wee ila sielewi kinachoendelea, kila mtu na lake, hiyo video nayoona, Si wanafundishwa ukakamavu jeshini kweli? hivo viboko mi naona kama tizi tu jeshini, tena tizi majeshi mengine ziipo hiyo cha mtoto, Ila kama ni wana makosa wanachapwa inategemea na kosa, mfano mtu kama gaidi unadhani hilo lina mtosha? hilo kidogo sana, hilo labda wenye makosa madogo madogo kama mwizi vile... Hata jambazi anastahili kikubwa zaidi ya hicho, ka unadhani hastahili ngoja siku uingiliwe wakukate mkono na miguu au wamchome kisu mzazi wako mbele yako ndio utaona kama. wanastahili hivho au zaidi..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom