Kidamva
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,578
- 1,984
Nimemsikia Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akisema kuwa mchakato wa Katiba utakuja baada ya Rais Magufuli kuinyoosha nchi. Hata muda huu anaongea kwenye kipindi cha Sema kweli (Chanel 10). Hivi lini Rais Magufuli aliahidi kuleta Katiba mpya?
Mwenyewe alishasema suala hilo halikuwepo kwenye ahadi zake za uchaguzi. Sasa wewe Polepole umeteuliwa juzijuzi unawaahidi Watanzania kuwa wakishanyooshwa ndiyo katiba italetwa, je Rais akikataa?
Wakati Polepole akiwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, alikuwa akisisitiza madai ya Katiba mpya, hakujua kama kuna kunyooshwa? Mabilioni ya fedha yametumika ya nini kama mlikuwa mnajua nchi inatakiwa kunyooshwa kwanza? Huu ni unafiki tu.
Eti warejeshe kwanza nidhamu, aliyeiharibu ni nani? Amechukuliwa hatua gani?
Polepole aache kuwa kigeugeu.