TLS waendesha Zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi wa jiji la Dar es salaam juu ya Katiba mpya

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
398
648
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) waendesha Zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi wa jiji la Dar es salaam juu ya katiba mpya
20240615_184312.jpg

Kipekee napenda kuwakaribisha katika mdahalo wetu wa mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya #KatibaMpyaNiSasa

Mariam Othuman, Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)Nchi zingine zina mfumo ambapo Rais anaweza dhibitiwa na Mamlaka mengine ili kuchochea uwajibikaji na ufanisi wa utendaji wa serikali: Iddy Mandi

"Muundo wa Muungano umekuwa na malalamiko Mara nyingi malalamiko huanzia Tanzania Visiwani ambapo husema Tanzania Bara imejivika koti la Muungano na kwa muda mrefu wanaharakati wametaka uboreshwe" - Iddy Mandi
20240615_183811.jpg

"Vifungu vya Uraia Watu wengi wanaopenda Uraia wa Tanzania hupendelea kuwa na uraia pacha ipo haja ya kuliangazia hili jambo kama lina mashiko na manufaa kwa kila mmoja" - Iddy Mandi

"Katiba 1977 ni katiba nzuri na imetuongoza kwa muda mrefu lakini kutokana na mazingira ya sasa ipo haja ifanyiwe maboresho" - Iddy Mandi

Kuna haja ya kuangalia upya
1 Uhuru wa Mahakama
2 Mfumo wa Uchaguzi
3 Mamlaka ya uteuzi
4 Mwingiliano wa Mihimili
Dkt Mande

Hakukuwa na uwakilishi sawa kwenye bunge maalum, na ikasababisha makundi mengine kutokukubaliana
20240616_002335.jpg
20240616_002339.jpg

20240616_002526.jpg
20240616_002530.jpg
20240616_002554.jpg
20240616_002556.jpg
20240616_002558.jpg

Baadhi ya wananchi kutoka makundi mbalimbali wa mkoa wa DSM wamefanikiwa kutoa maoni kwenye mjadala wa wazi juu ya 'Upatikanaji wa Katiba Mpya ambao umeandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanganyika.

Mjadala huo umefanyika leo 15 Juni 2024 makao makuu ya TLS Wakili house Mkoani Dar

Hakukuwa na uwakilishi sawa kwenye bunge maalum, na ikasababisha makundi mengine kutokukubaliana
@TanganyikaLaw #KatibaMpyaNisasa

Dkt Mandi anasema “ Kuna misingi ya Katiba”
1 Mgawanyo wa Madaraka (separation of Power)
2 Uhuru wa Mahakama
3 Utawala wa Sheria
Mgawanyo wa Mamlaka bado unapoteza msingi kwa sababu Executive inakuwa na mamlaka makubwa na kuimeza mihimili mingine
#KatibaMpyaNiSasa

Katibu wa Baraza la Wazee wa chama cha @ChademaTz Rodrick Rutembeka amekiri nia ya dhati ya Rais Samia kuleta Katiba Mpya lakini mkwamo ukarudi kwa @ccm_tanzania , amesema hayo leo wakati wa kuchangia mjadala wa wazi juu ya Upatikanaji wa Katiba Mpya ulioandaliwa na TLS.
 
Back
Top Bottom