Polepole unampoteza Zenda

Mondoros

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
629
472
Kwa muda mrefu sasa zenda amekua akisadikiwa kuisema vibaya uvccm kwa polepole na baadhi ya maofisa wa ccm Lumumba. Sababu ya kufanya hivyo iko wazi; (1) shirikisho kuondolewa na kuwekwa chini ya uvccm kama idara (2) kutopewa cheo kikubwa (unaibu katibu Mkuu au ukatibu mkuu) (3) kupenda kufanya kazi bila kufuata taratibu na mipango.

Kwasababu ya hayo yote hivyo ameamua kumtumia polepole kama mtu wa kumuhakikishia kuwa anaivuruga uvccm na hatimaye kuukwaa ukuu wa jumuiya hii adhimu ya ccm, hivyo polepole amekua akifanya kila analoliweza kuhakikisha kuwa anaviza utendaji kazi wa uvccm, anaingilia majukumu ya jumuiya, na pindi anapojishughulisha na kazi za vijana kiungo anayemtumia ni zenda pekee kwani anataka kumfanya yeye ndio aonekane kama mtu pekee anayeweza kufanya shughuli za jumuiya na za vijana kwa ujumla.

Kwanini nasema Polepole anampoteza zenda?

(1) CCM na Jumuiya zake inayo utaratibu wa kufanya kazi. Polepole anamshughulisha Zenda kuuvunja utaratibu wa CCM na Jumuiya zake kwenye uhusiano wa kikatiba na Kikanuni wa kufanya kazi.

(2) Msimamizi Mkuu wa shughuli za UVCCM ni Katibu Mkuu, lakini Polepole akadandia majukumu ya mwenye nayo kwa kupitia Zenda na kuyahodhi mamlaka hayo kwa lengo lao la msingi la kuivuruga UVCCM.

(3) Polepole anyemgombea wake wa uwenyekiti UVCCM (ninamuhifadh jina kwa awamu hii) Hivyo kiungo mchezeshaji kwenye harakati hizo ni Zenda, na Zenda kaamua kuwa mwendawazimu zaidi ya uwendawazimu wake unaofahamika.

(4) Polepole amemuhakikishia Zenda na washirika wake kuwa yeye ndiye Katibu mkuu wa CCM ajaye kwasababu kinana ataondoshwa katika nafasi hiyo na kukikalia kiti, pia amemfahamisha zenda kuwa atampambania awe katibu mkuu uvccm ajaye ili wafanye kazi pamoja.

(5) Polepole anamremote control Zenda kuandaa mambo yasiyo ya ukweli mfano kupanga safu na kupokea rushwa na kutafuta namna ya kuzipenyesha kwa rais. Na hii imedhibitika juzi jumamosi siku ambayo rais alikwenda kigamboni.

Mwisho Ningependa kumshauri Polepole ajiheshimu na atulizane, maana tabia mbaya anoyoonyesha sio njema kwa afya ya CCM.

Pia Zenda ni mdhaifu sana kiuongozi na hana nasaba zozote za uongozi, anafanya kulazimisha mambo.

Usipopigwa na radi kutoka kwa MUNGU ukapotea, utapigwa kwa namna yeyote na wanadamu.

USIPOZIBA UFA, UTAJENGA UKUTA
 
nimecheka ulivyosema zenda kaamua kuwa mwendawazimu zaidi ya uwendawazimu wake unaojulikana...


huyo zenda ni kichaaa kwa kweli nimesoma nae primary namjua ...... huyo zenda kabla hujamvuruga anakuvurugaaaa mara 100 ... hanaga aibu hata uchi anaweza akatembea.... uvccm kweli kazi mnayoooo kama viongozi wenu ni kina daniel zendaaa
 
Siasa ni fitina, ila ukijibu fitina kizwazwa unapotezwa. Hivi ulivyofanya jiandae kukimbilia Akiba ya Chama Tawala.
 
nimecheka ulivyosema zenda kaamua kuwa mwendawazimu zaidi ya uwendawazimu wake unaojulikana...


huyo zenda ni kichaaa kwa kweli nimesoma nae primary namjua ...... huyo zenda kabla hujamvuruga anakuvurugaaaa mara 100 ... hanaga aibu hata uchi anaweza akatembea.... uvccm kweli kazi mnayoooo kama viongozi wenu ni kina daniel zendaaa
Huyu jamaa ni mwendawazimu kweli,sasa kama amekuwa zaidi ya ile kawaida...Itakuwa balaa
Kwa sasa hakuna tena UVCCM ya maana,wapo kwa ajili ya kusaka vyeo na wengine kuuza papa wapate nafasi.UVCCM hii sio hata kama ile ya kina Nchimbi...Hiivijana wapo kama mikuku ya boila

Wanawaza vyeo na ukuu tu,hakuna ubunifu wala harakati za siasa,wanajazana Lumumba kuitana komredi bila maana,kupigana mizinga na ndio maana unaona wameshaanza kuparuana wanagombea uongozi
 
Ungetaja basi jina la huyo mtu kama wewe hauko nyuma yake kutaka awe mwenyekiti... kazi mnayo.. kumbe mna drama hata awamu hii na amuogopi kabisaaa.. DUH!!!
 
Nani amekutuma wewe kwanini usitumie vikao vya chama aidha uvccm au vyovyote vile lakini viwe ni vikao vya chama kuzungumza madukuduku yako kama kweli unazo hoja za msingi na hukutumwa na mtu yoyote yule? Hii sio njia sahihi.
 
Back
Top Bottom