Polepole: Tanzania tuna kaya 14,152,803 kwa bei ya Cuba mtungi wa gesi wa 10Kgm tunahitaji tzs 28.3B

Polepole: Tanzania tuna kaya 14,152,803 kwa bei ya Cuba mtungi wa gesi wa 10Kgm tunahitaji tzs 28.3B

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
2,091
Reaction score
1,915
Team,
Salaam!

Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 inaonesha Tanzania ina kaya 14,152,803. Sasa kama tungekuwa na bei ya kununua mtungi wa gesi wa 10kgm kwa tzs 2,000 kama ilivyo nchini Cuba basi kaya zote hapa nchini tungetumia tzs 28,305,606,000/=.

Sasa kwa kuwa na gesi inayouzwa takribani tzs 56,000 hii imepelekea kuhitajika kwa tzs 792,255,698,000/=.

Sasa kwa nini Serikali haijajikita ktk ugawaji wa mitungi ya gesi kwa kaya nyingi nchini - huenda ni moja ya sababu zifuatazo:-

1. Baadhi ya Halmashauri za wilaya kutegemea shughuli za uvunaji mkaa kama sehemu ya pato kuu - hivyo Serikali inaona kwamba jamii kubwa ikitumia gesi basi mapato yatapungua;

2. Elimu ndogo ya utunzaji mazingira kwa viongozi wengi nchini - kwamba hawajui athari za ukaji ovyo wa miti na athari za baadae;

3. Huenda viongozi wengi ni wabia wa wafanyabiashara wa gesi au huenda hupata 10% kutoka kwa wafanyabiashara wa mitungi ya gesi na gesi;

4. Huenda jamii haijahamasika kuhusu umuhimu wa kutumia gesi kwa shughuli nyingi za kaya.

Mwisho, Balozi HP asibezwe - hoja zake zisibezwe - na Taifa msijenge chuki kwa wanaowakosoa.
 
Back
Top Bottom