Polepole na Katiba Mpya ni Sawa na Mtu anayeogopa kivuli chake

Ethos

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
2,293
2,000
... Leo nimemsikiliza Kwa makini sana Ndugu Polepole katika kipindi cha asubuhi maarufu kama 360 cha Clouds tv
... Kwanza nampongeza Kwa kujibu maswali mengi vizuri sana na kwa facts kama kawaida yake

.. Kuhusu Chama cha mapinduzi kumiliki Mali nyingi kuliko vingine nimemuelewa baada ya kusema Mali hizo mlizitafuta na mna haki ya kuwa nazo... Hii ni changamoto Kwa vyama vingine

... Lilipokuja swala la katiba mpya amelikwepa kabisa. Ameulizwa mara zaidi ya mbili na watazamaji Lakini amelikwepa na kuishia kututaka tuangalie muelekeo wa Rais Magufuli ili tupate hitimisho la msimamo wake..

.. Polepole kwanini usiseme tu wazi kuwa tunahitaji katiba mpya ili na nchi ipate mapinduzi ya kimfumo kama mnavyofanya ndani ya Chama chenu? Unaogopa nini? Itikadi na Uenezi ndio inasababisha uvae gamba lingine?
 
PRINCE CROWN

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,987
2,000
huyu kijana wangu Mimi namkubali sana kwa Ukweli ni Mtu timamu sana hata ukimsikiliza.

Lakini kosa alilofanya ni kukubali kuwa Mkuu wa wilaya na hatimae kuteuliwa kuwa Mwenezi wa chama.

Hapa ajue walio waerevu zaidi yake wamempatia nafasi hiyo ili wamdhibiti juu ya misimamo yake iliyokuwa inakinzana na chama chake.

Sote tunajua jinsi huyu ndugu alivyoipigania rasimu yao iliyokanyagwa kule bungeni na kuibuliwa ile ya mzee samweli sita ambayo tunasubiria iletwe tuipigie kura hapo ndipo alipozibwa mdomo.

Siasa ni mahesabu na ujanja ujanja hivyo kijana wangu pole pole, habari yake kwishiney.

Amebaki Mzee wangu Butiku. Sijui na Mzee wangu Warioba kama atakuwa na Ubavu wa Kuisimamia Kazi yake Aliyoipigania sana.
 
Nov 21, 2016
53
95
Watanzania wengi ujiangalizia masirah yao binafsi tu na c ya nchi atapiga kelele akiwa hayupo kwenye systeam akiwekwa basi kazibwa mdomo na apganii tena kile alichkua anakiamni ndo Tanzania yetu watu wake walivyo
 
MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
9,467
2,000
Mpaka atakapoondolewa kwenye hiyo nafasi aliyo nayo ndio ataweza tena kuizumgumzia Katiba mpya..

Kwa sasa tusitegemee lolote linalohusiana na Katiba mpya kutoka kwa Polepole.

Unafiki uliotukuka..!!
 
Ethos

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
2,293
2,000
huyu kijana wangu Mimi namkubali sana kwa Ukweli ni Mtu timamu sana hata ukimsikiliza.

Lakini kosa alilofanya ni kukubali kuwa Mkuu wa wilaya na hatimae kuteuliwa kuwa Mwenezi wa chama.

Hapa ajue walio waerevu zaidi yake wamempatia nafasi hiyo ili wamdhibiti juu ya misimamo yake iliyokuwa inakinzana na chama chake.

Sote tunajua jinsi huyu ndugu alivyoipigania rasimu yao iliyokanyagwa kule bungeni na kuibuliwa ile ya mzee samweli sita ambayo tunasubiria iletwe tuipigie kura hapo ndipo alipozibwa mdomo.

Siasa ni mahesabu na ujanja ujanja hivyo kijana wangu pole pole, habari yake kwishiney.

Amebaki Mzee wangu Butiku. Sijui na Mzee wangu Warioba kama atakuwa na Ubavu wa Kuisimamia Kazi yake Aliyoipigania sana.
Kipindi cha katiba nilikuwa namuelewa sana.. Ila kwasasa nadhani uhuru wake wa kazungumza unamezwa na matakwa ya Chama..
 
mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,451
2,000
Kuna siku nilimsikia mmama mmoja somebody Semakafu akisema bila aibu wala haya kwamba eti hatuhitaji tena katiba mpya kwa sababu Magufuli anafanya yale tuliyotaka kwenye katiba mpya. Sikuamini masikio yangu! Eti Magufuli ndio katiba mpya? Nilijisikia kufa? Very sad indeed. Tens huyo mama ni msomi eti Dr Avemaria, Pumbavu kabisa! Msgufuli akifa leo je?
 
Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
1,950
2,000
We ulitaka mpaka atamke kwamba watarudi kwa Rasimu katiba ya Warioba? Kawaambieni kwamba CCM wanafanya mageuzi makubwa ya kurudisha Chama kwa Watu, na kwamba Chama kitasikiliza watu wanataka nini, na kwamba katiba ni takwa la watu na wataheshimu watu wanataka nini! Yaani hapo hujaona kwamba Rasimu ya Katiba ya Warioba ndio iko mezani?

Kweli unashindwa kuunganisha dots za kwanini Chama cha Mapinduzi kinachoamini ktk serikali MBILI kinampa mtu nafasi kubwa ya uongozi mtu menye msimamo wa serikali TATU? Hukumsikia akisema kuteuliwa kwake nayeye kukubali kunamaana mbili, kwanza ama ame-compromise na Msimamo wa CCM na kuachana na wakwake aaouamini mpaka kufa au anaenda kusaidia CCM ku-adopt matakwa ya serikali TATU ambayo WATU ambao CCM inawatumikia wanataka. Unataka jibu la vipi ndungu, mbona kajibu vizuri saaaaaaana kwamba RASIMU ya WARIOBA itafuatwa.
 
Huyo AVEMARIA SEMAKAFU hakuna kitu kabisa! Huwa hana hoja sijui ni (Dr) mganga wa kienyeji? Juzi pia nilimsikia ktk DIRA ya DUNIA ya DW akibwabwaja kuhusu marais wa Africa kung'ang'ania madaraka, eti anasema hiyo ndiyo demokrasia ya kiafrika, ya machifu n.k. Mara kakimbilia viongozi wa vyama vya upinzani kukaa muda mrefu, wala hakuzungumzia katiba za vyama vyao, yaani wachangiaji wengine wote walitofautiana naye. Nakumbuka alivyokuwa akisema katiba pendekezwa ni nzuri sana imezingatia usawa wa jinsia, blablabla. Sasa inaenda kuibuliwa ya Warioba sijui atasemaje. Huyu vyeti vyake vihakikiwe, huenda ni vya kughushi au ni hewa!
 
shige2

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
7,899
2,000
UKWELI usio KANUKIKA. Nchi nyingi zilizoweka mifumo ya FEDERAL/ KUSOGEZEA Watu TAWALA nchi hizo zimepiga hatua kubwa sana.
Miaka ya 1961tulipopata uhuru, watu walikuwa ni millioni ndogo sana. Na hivyo CENTRAL government/Serikali kuu ilikuwa ni LAZIMA itawale na IAMUE mkoa gani UTAPATA nini na Mkoa upi HAUTAPATA.

Na matokeo yake kukawa na IMBALANCE/KUTO UWIYANA kimaendeleo. Mikoa mingine IKAPENDELEWA zaidi.
Na Mikoa mingine IKANYIMWA maendeleo maksudi.
Na matokeo yake TUNAYAONA=UMASKINI kila mahali.

Nchi nyingi za ULAYA na Marekani zilizo BADILI miundo ya KATIBA zao na kusema.
"SERIKALI KUU haiwezi kuwaamulia watu ni Barabara ipi ijengwe ama ni Visima vingapi vya maji vichimbwe ama ni NINI KIPAU MBELE cha eneo husika"
Hivyo basi MAENDELEO yakaWAKARIBIA wananchi.

Na wenzetu WAKO MBELE sana kimaendeleo sababu ya hio sisitimu!
Tanzania hatuna namna ni LAZIMA system ya FEDERAL/KUSOGEZEA WATU TAWALA iweze kuwepo.
Ni AIBU sana miaka zaidi ya 50 ya kujitawala HAKUNA Barabara za LAMI zinazounganisha WILAYA na WILAYA. Hakuna MAJI vijijini, AJIRA ni SHIDA nk.

Sababu kuu ya impediment hii/ Zuio hili la maendeleo ni kuwa WATU WACHACHE wanakaa kwenye boardroom wanakuamlia
UAJIRIWE ama USIAJIRIWE,
UJENGEWE HOSPITALI ama LA.
Serikali KUU ina mambo mengi sana ni VIGUMU kutatua SHIDA ZOTE za Watanzania bila ku DEVOLVE kabisa na wala si PIECE MEAL devolvement/Mamlaka ya VIPANDE VIPANDE.

Kama kuna shida katika katiba turekebishe LAKINI KATIBA MPYA HAIEPUKIKI! Maana si ya MTU ni ya WATANZANIA na watanzania wanataka HAKI yao ya MAENDELEO!!!
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,045
2,000
Huyo AVEMARIA SEMAKAFU hakuna kitu kabisa! Huwa hana hoja sijui ni (Dr) mganga wa kienyeji? Juzi pia nilimsikia ktk DIRA ya DUNIA ya DW akibwabwaja kuhusu marais wa Africa kung'ang'ania madaraka, eti anasema hiyo ndiyo demokrasia ya kiafrika, ya machifu n.k. Mara kakimbilia viongozi wa vyama vya upinzani kukaa muda mrefu, wala hakuzungumzia katiba za vyama vyao, yaani wachangiaji wengine wote walitofautiana naye. Nakumbuka alivyokuwa akisema katiba pendekezwa ni nzuri sana imezingatia usawa wa jinsia, blablabla. Sasa inaenda kuibuliwa ya Warioba sijui atasemaje. Huyu vyeti vyake vihakikiwe, huenda ni vya kughushi au ni hewa!
Tumbo limepiga dafrau kichwa-na kwa wasomi hii ni kawaida sana.
 
Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,000
We ulitaka mpaka atamke kwamba watarudi kwa Rasimu katiba ya Warioba? Kawaambieni kwamba CCM wanafanya mageuzi makubwa ya kurudisha Chama kwa Watu, na kwamba Chama kitasikiliza watu wanataka nini, na kwamba katiba ni takwa la watu na wataheshimu watu wanataka nini! Yaani hapo hujaona kwamba Rasimu ya Katiba ya Warioba ndio iko mezani?

Kweli unashindwa kuunganisha dots za kwanini Chama cha Mapinduzi kinachoamini ktk serikali MBILI kinampa mtu nafasi kubwa ya uongozi mtu menye msimamo wa serikali TATU? Hukumsikia akisema kuteuliwa kwake nayeye kukubali kunamaana mbili, kwanza ama ame-compromise na Msimamo wa CCM na kuachana na wakwake aaouamini mpaka kufa au anaenda kusaidia CCM ku-adopt matakwa ya serikali TATU ambayo WATU ambao CCM inawatumikia wanataka. Unataka jibu la vipi ndungu, mbona kajibu vizuri saaaaaaana kwamba RASIMU ya WARIOBA itafuatwa.
Ni lini CCM ilikua chama cha wanyama ,mbona hamkutangaza? Eti ile rasimu ya Warioba ,kwani hii iliyopendekezwa lini CCM walisema hatufai? CCM haiwezi kukubali kua chama cha kinacho ongozwa na maskini maana hawana tija zaidi ya kutupigia kura basi
 
Ethos

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
2,293
2,000
We ulitaka mpaka atamke kwamba watarudi kwa Rasimu katiba ya Warioba? Kawaambieni kwamba CCM wanafanya mageuzi makubwa ya kurudisha Chama kwa Watu, na kwamba Chama kitasikiliza watu wanataka nini, na kwamba katiba ni takwa la watu na wataheshimu watu wanataka nini! Yaani hapo hujaona kwamba Rasimu ya Katiba ya Warioba ndio iko mezani?

Kweli unashindwa kuunganisha dots za kwanini Chama cha Mapinduzi kinachoamini ktk serikali MBILI kinampa mtu nafasi kubwa ya uongozi mtu menye msimamo wa serikali TATU? Hukumsikia akisema kuteuliwa kwake nayeye kukubali kunamaana mbili, kwanza ama ame-compromise na Msimamo wa CCM na kuachana na wakwake aaouamini mpaka kufa au anaenda kusaidia CCM ku-adopt matakwa ya serikali TATU ambayo WATU ambao CCM inawatumikia wanataka. Unataka jibu la vipi ndungu, mbona kajibu vizuri saaaaaaana kwamba RASIMU ya WARIOBA itafuatwa.
Angesema wazi wazi... Kwanini angolee Kwa kificho?
 
clet 8

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
1,126
1,500
Pole pole hana alishaishiwa uhai wa kauli, ni ngumu kumeza matapishi.
 
Shuleless

JF-Expert Member
Aug 12, 2015
4,909
2,000
Qualifications za kua mwanaccm
1-kua mnafiki
2-tendea haki unafiki wako
3-rejea qualification namba moja na mbili
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom