Polepole, Mangula na wengine; wakati ndio huu

Joshua justine

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
792
1,007
Nawasalimu wadau wote wa jukwaa hili; ninaomba tushirikiane kwa pamoja kuangalia jambo hili kutoka pande mbalimbali na kuona kama linaweza kuwa ni uamuzi sahihi kwa majira haya ambayo taifa letu limefikia sasa.

Wote tunakubaliana kuwa kila jambo huwa na mwisho wake na historia inajengwa na matukio. Huwezi kupingana na uhalisia halisi pale matukio yanapokuwa yakijenga historia, tumeona falme zilivyoinuka zikafika kileleni zikang'ara na zikaporomoka muda wake ulipoisha, na ni matukio ndio yamesababisha, cause and effect. Uingereza iliwika ikaja marekani na sasa mchina anatake over mbele ya macho ya ulimwengu mzima na hakuna awezaye kuzuia hata mmarekani mwenyewe anafurukuta tu, kwa sababu yameshafanywa matukio na mmarekani mwenyewe na wenzzie yanayosababisha hayo, hivyo hawezi tena kuzuia.

Tanzania tunapotimiza miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika kuna mambo mengi yametokea katika historia ya siasa yetu. Ni kitabu kizima unaweza kujaza matukio hayo yakiwemo ya ufisadi, vifo vya viongozi wema kama hayati sokoine, n.k na hayajaacha kutokea mpk kesho! Wote tunakumbuka viongozi kama Nyerere alipokuwepo alivyolazimika kuwa anakemea mpaka watawala kama watoto wadogo wasiojua nin wanafanya, tumeona hayati Magufuli nae alijaribu kukemea na kuwaadhibu pia, leo hii watu hao wa kukemea na kuwafunga kengele viongozi waovu wote wamekwenda zao, je taifa litaelekea wapi wale mbwa wakifunguliwa?

Tunaona watu kama Polepole wanavyojaribu kuongea lakini wote tunajua na hata yy mwenyewe amekiri mara nyingi kujaribu kutishwa na wengine ndani yachama ili asiongee, je ameongea lipi baya la kutaka kumfunga mdomo?

Ni wazi chama cha mapinduzi sasa kimepoteza legitimacy ya kutawala nchi rasmi! Kwani yote yanayofanyika humo ni kinyume na misingi ya siasa za nchi yetu na siasa za chama hicho chenyewe ambavyo vyote pamoja viliwekwa na waasisi wa taifa letu mwanzoni kabisa. Ni matukio mengi yametokea na leo ni ukomavu wa matukio hayo tu, huwezi kusema eti bado tukipe nafasi utakuwa hujuihistoria vizuri wewe, maaana ikifika ukomavu wa matukio historia inadai mabadiriko na utake usitake yatakuja tu hata ulie, ugalegale , no way!

Chama cha mapinduzi ndani yake chembe za watu wasafi zimebaki chache kuliko walio waovu, na tunaona wanavyokuja kwa nguvu mpaka raia wote wamejikatia tamaa kabisa. Sasa kuibuka tena mtu mzalendo na kufanya miujiza aliyofanya hayati Magufuli ndani ya chama hicho ni ndoto isiyowezekana.

TUFANYAJE
Wazalendo waliobaki ndani ya chama hicho mkubali matokeo, (ngumu kumeza), lakini ni wakati wa nyinyi kuja na CHAMA KIPYA CHA SIASA NCHI HII.

Najua mtasema kuwa kuna vyama vingi vimeshindwa, lakini napenda kuwakumbusha kuwa kila tukio lina right timing yake, umri wa CCM ulikuwa haujaisha wakati Mkapa, Magufuli na wengine bado wapo hai, maana chama kilifikia hatua waatu hawaiogopi katiba yao bali wanaogopa viongozi wakali waliopo, sasa hawapo, je niambie nani ni , "BABA NDANI YA CHAMA HICHO SASA, NA ANA SIFA GANI?"

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa CCM sio mama yake, je nyie mlioikuta tu mnajifanya CCM ni zaidi ya mama zenu?
NI UKWELI KUWA UPINZANI SAHIHI UTAKAOSHIKA NCHI HII UNAPASWA UTOKEE NDANI YA CCM KWA SABABU ZIFUATAZO:
  • Viongozi watakaounda chama kipya watakuwa wana uzoefu mzuri wa siasa ya nchi yetu na misingi yake iliyowekwa na waasisi hivyo wataanzisha chama kinachokuja kurudisha uzalendo upya bila kuiasi misingi ya taifa (ni lazima wakubali kutoka na yale mema CCM, maana hayo ni ya waasisi na wananchi sio ya hao mafisadi watakaobaki humo)
  • Kwakuwa watakuwa ni watu walewale (ila wazalendo), hawatakuwa na kazi kubwa kufikia matawi yote na mashina yote nchi nzima kwani CCM itapasuka juu mpaka chini kama pazia la hekalu, hii itawarahisiahia kuwa tayari wakati uchaguzi utakapofika 2025, jambo hilo ni tofauti iliyosababisha vyama kama Chadema kushindwa kuchukua madaraka kwa urahisi.
  • Ni chama kipya ndio kutoka CCM ndio kitawezesha kuwe na power check na power balance ya ukweli katika taifa hili itakayorudisha nguvu ya kura ya raia na hivyo kuimarisha ama kurudisha demokrasia ya ukweli kwenye taifa letu.
  • Ni chama kipya kutoka CCM ndio kitawezesha kuandikwa katiba mpya ya wananchi katika taifa hili( kubotesha katiba iwe ya wananchi zaidi)

JE, hakuna mpasuko humo ndani ya chama hata sasa watu wanagombaniana vyeo na mali humo?

Historia hakuna wa kushindana nayo, mkiogopa kuanzisha chama jambo ambalo sio dhambi kikatiba ipo siku raia watachoka na risasi ya kwanza itakaporushwa katika tukio lolote lile hapohapo ndipo mafuriko yatakapopasulia njia (MARK MY WORDS)

SUGGESTED READINGS;
*Mwili umekosa kichwa ( jukwaa la siasa)
*Hili liwe funzo: tudai katiba bora zaidi (maboresho) - jukwaa la katiba mpya.
  • Serikali na mwarobaini wa matatizo yetu (Jukwaa la siasa)
  • Ukweli mchungu, ngumu lakini ndivyo ilivo ( jukwaa la siasa)
NB: wazalendo mliopo humu JF naomba uzi huu kwa vyovyote uwafikie Polepole, Mangula et al.
Tuepuke mawazo mgando, CCM milele, sio Mungu CCM, inaweza anguka pia kama marekani, kama zambia!
 
Mkuu hivi huioni chadema Kama Ni strong party to take over after the death of ccm? Mikutano inakatazwa kwa mabomu na he unahisi hicho chama kipya ndo mikutano yake itaruhusiwa na hawahawa polisi.

Shida siyo chama shida Ni watu kujitoa muhanga ikitokea polisi wakakataa mikutano mnafanya hivyohivyo polisi wanawaua wote siku nyingine wanafanya wengine polisi wanaua wote, siku nyine Tena wanafanya wengine mpaka polisi watakapochoka kuua
 
Nakubaliana na ww, chadema ndio wameshafanya hivyo unavyosema na sasa polisi wamewafanya hivyo unavyosema Lissu hayupo nchini , Mbowe hatujui hatima yake na pengine wakatumia mwanya huo kumchelewesha kuja kujipanga na 2025, sasa niambie tunategemea nn tena na 2025 , Mungu atupe uzima, sio mbali mkuu, dawa ni kupata nguvu mpya tu,
 
Chama kipya ambacho waanzilishi wake ni kutoka CCM iliyomezwa na mawakala wa wezi wa raslimali za taifa ( kuna watu wenye historia ya utumishi uliotukuka kila mtanzania anawafahamu) kianzishwe haraka. Msisubiri kampeni za uchaguzi zianze. Msisubiri mapinduzi aliyoyaanzisha JPM mioyoni mwetu yanyauke!
 
Binadamu bana, wakati mnakula mnafaidi kwenye ma-vieiteee mlikuwa kimya hamkutaka tusaidiane kupiga makelele mapungufu, sasa hvi mambo yamebadilika mnataka tujiunge nanyi kukemea maovu - hii siyo sahihi - sasa ni hivi kila mtu apambane na hali yake.

Sisi wananchi priority yetu kwa sasa ni katiba mpya, sasa yeyote asiyetaka katiba mpya ni adui yetu - over.
 
Ahahaaaa...
●Tumeamua kuwa wakweli basi acha tuseme bila kupepesa, Rais wa sasa anamalizia Awamu ya 5 ya hayati JPM, ambaye kwa mapenzi ya MUNGU aliishia njiani.

●Kinachofanyika sasa ni usanii wa kisiasa wakulazimisha wananchi wamtambue Rais wa sasa kama Rais wa awamu ya 6.
 
Binadamu bana, wakati mnakula mnafaidi mlikuwa kimya hamkutaka tusaidiane kupiga makelele mapungufu, sasa hvi mambo yamebadilika mnataka tujiunge nanyi kukemea maovu - hii siyo sahihi - sasa ni hivi kila mtu apambane na hali yake.

Sisi watanzania priority yetu kwa sasa ni katiba mpya, sasa yeyote asiyetaka katiba mpya ni adui yetu - over.
Halafu Chama kipya kitokane na CCM ile ile!! Kweli??? Hajui "Mtoto wa Nyoka ni Nyoka??"
 
Nawasalimu wadau wote wa jukwaa hili; ninaomba tushirikiane kwa pamoja kuangalia jambo hili kutoka pande mbalimbali na kuona kama linaweza kuwa ni uamuzi sahihi kwa majira haya ambayo taifa letu limefikia sasa...
Mtakisajili wapi? Burundi?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Chama kipya ambacho waanzilishi wake ni kutoka CCM iliyomezwa na mawakala wa wezi wa raslimali za taifa ( kuna watu wenye historia ya utumishi uliotukuka kila mtanzania anawafahamu) kianzishwe haraka. Msisubiri kampeni za uchaguzi zianze. Msisubiri mapinduzi aliyoyaanzisha JPM mioyoni mwetu yanyauke!
Mkuu tupaze sauti tu , wananchi ndio wenye nchi , tukikubali upuuzi ndio basi tena,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom