Polepole: Makonda hakupaswa kufanya sherehe na Polisi

Polepole: Makonda hakupaswa kufanya sherehe na Polisi

Polisi walikua kwenye zoezi la kuhakikisha jamaa anashinda na wamefanikisha hivyo lazima wapongezwe bwana polepole acha nongwa
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hakupaswa kufanya sherehe na Polisi kwa sababu kuna mahali hali haikuwa shwari na wao walikaa kimya.

Polepole ameyasema hayo leo Septemba 18,2018 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam akielezea sababu za ushindi wa majimbo mawili ya Monduli na Ukonga.

Amesema Chadema wanasema Jeshi la Polisi linawasaidia CCM ilihali aliyekuwa mgombea ubunge wa chama chao kwenye Jimbo la Ukonga Asia Msangi alimkwida msimamizi wa uchaguzi mbele ya Polisi na walikuwa wametulia.

"Makonda hakupaswa kufanya sherehe nao kwa sababu kuna mahali sheria ya tume ilikuwa inakiukwa na wao wapo wametulia" amesema Polepole.

Amesema pamoja na yote CCM inathamini uwepo wa vyama vya upinzani na wanataka wakosolewe na kupewa mawazo mbadala.

"Kwa bahati mbaya hawa wenzetu kazi yao ni kukosoa tu" amesema

Pia, Katibu huyo aliutaka upinzani utambulike kwa itikadi za vyama vyao badala ya kuonekana mtu zaidi ya chama.

"Kama chama kinachojinasibu kuwa ni mpinzanii mkuu na ninachelea kukiita mpinzani na ninashukuru wameshindwa vibaya, ukimtoa yule kiongozi wao na wapambe wake wa karibu Kinabaki nini, ACT Wazalendo ukimtoa mjomba kinabaki nini.”

"Wajenge kwanza itikadi ya vyama vyao itambulike, CCM ni taasisi inayotambulika kiitikadi" amejinasibu Polepole.
IMG_20180918_165822.jpeg
IMG_20180918_165757.jpeg
IMG_20180918_165727.jpeg
 
Mbona hana mpambe hata mmoja pembeni, ndo kusema mwanzo wa ngoma ni.......???! Anyway, tutafika tu
 
Hakukua na anayehamia safari hii... Hiyo siti ya Pembeni inakaliwa na kina Kalanga, waitara, yule wa liwale n. K
Mbona hana mpambe hata mmoja pembeni, ndo kusema mwanzo wa ngoma ni.......???! Anyway, tutafika tu
 
Anapinga kama nani?kwa mfano.Wakati bosi wa polisi atawafanyia family day sasa yeye ni nani au ni drama ionekane wao hawako behind all these drama! Nacheka mwenyewe kwa kujitekenya kwa sinema isiyo na stelingi!
 
Vipi mawakala waliotolewa nje ya vituo ili mpate nafasi ya kupindua matokeo..?
Pole pole hupaswi kushadidia mambo haya ya aibu.
Chama Kikongwe bado kinahitaji msaada wa Tume na Polisi ili kupata ridhaa ya kuongoza..?
 
wananchi hatuna shida na nyie tunajifunza kuvumilia
 
Funika Kombe Mwanaharamu apite ,tunajua mliiba endeeni kusherehekea Ushindi .
 
Kwa nyuzi kama hizi za chakubanga.
ccm haitatoka madarakani kamwe.
 
Angemalizia kwa kutaja "idadi" ya watu wa "vyama vya upinzani" na wa "ccm" waliokamatwa.

Tujue idadi ya wangapi ambao wapo ndani bado kwa pande zote mbili.
 
Back
Top Bottom