Polepole: Makonda hakupaswa kufanya sherehe na Polisi

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hakupaswa kufanya sherehe na Polisi kwa sababu kuna mahali hali haikuwa shwari na wao walikaa kimya.

Polepole ameyasema hayo leo Septemba 18,2018 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam akielezea sababu za ushindi wa majimbo mawili ya Monduli na Ukonga.

Amesema Chadema wanasema Jeshi la Polisi linawasaidia CCM ilihali aliyekuwa mgombea ubunge wa chama chao kwenye Jimbo la Ukonga Asia Msangi alimkwida msimamizi wa uchaguzi mbele ya Polisi na walikuwa wametulia.

"Makonda hakupaswa kufanya sherehe nao kwa sababu kuna mahali sheria ya tume ilikuwa inakiukwa na wao wapo wametulia" amesema Polepole.

Amesema pamoja na yote CCM inathamini uwepo wa vyama vya upinzani na wanataka wakosolewe na kupewa mawazo mbadala.

"Kwa bahati mbaya hawa wenzetu kazi yao ni kukosoa tu" amesema
Pia, Katibu huyo aliutaka upinzani utambulike kwa itikadi za vyama vyao badala ya kuonekana mtu zaidi ya chama.

"Kama chama kinachojinasibu kuwa ni mpinzanii mkuu na ninachelea kukiita mpinzani na ninashukuru wameshindwa vibaya, ukimtoa yule kiongozi wao na wapambe wake wa karibu Kinabaki nini, ACT Wazalendo ukimtoa mjomba kinabaki nini.”

"Wajenge kwanza itikadi ya vyama vyao itambulike, CCM ni taasisi inayotambulika kiitikadi" amejinasibu Polepole.

Chanzo: Mwananchi
Mhh!
 
View attachment 870101

Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole amemkosoa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kitendo chake cha kuwafanyia sherehe Askari Polisi walikuwa katika jukumu la kulinda usalama wakati wa zoezi la Uchaguzi wa marudio.
Polepole amekosoa pia kitendo cha Askari Polisi kushindwa kuingilia kati pale Mgombea ubunge wa CCM, Asiah Msangi alipomdhalilidha mmoja wa wasimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ukonga huku yeye akishindwa kuingilia kati.

View attachment 870112

POLEPOLE AKOSOA NIA YA RC DAR KUWAFANYIA SHEREHE POLISI

View attachment 870102
Waanzisha fujo hao
 
Hivo huwa mnakuwa na mda wa kumsikiliza slow slow! Ni kijana aliyesema ukweli katika maswala ya kitaifa akajijusanyia mashabiki.... Baada katiba kukwama kachagua kuwa Mwongo na mnafiki wa kiwango cha juu. Ni wa kupuuza tu.....
 
Ndo uzuri wa chama cha mapinduzi, wanatofautiana mitizamo wakiwa chama kimoja na maisha yanaendelea, hebu jaribu chagadema umpinge Mbowe kama utasavaivu, thubutu!,utaishia kuitwa msaliti tu, Mbowe ni chairman wa maisha
Kwa hiyo mambo sasa na DAB walinengua sababu ni CCM???
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hakupaswa kufanya sherehe na Polisi kwa sababu kuna mahali hali haikuwa shwari na wao walikaa kimya.

Polepole ameyasema hayo leo Septemba 18,2018 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam akielezea sababu za ushindi wa majimbo mawili ya Monduli na Ukonga.

Amesema Chadema wanasema Jeshi la Polisi linawasaidia CCM ilihali aliyekuwa mgombea ubunge wa chama chao kwenye Jimbo la Ukonga Asia Msangi alimkwida msimamizi wa uchaguzi mbele ya Polisi na walikuwa wametulia.

"Makonda hakupaswa kufanya sherehe nao kwa sababu kuna mahali sheria ya tume ilikuwa inakiukwa na wao wapo wametulia" amesema Polepole.

Amesema pamoja na yote CCM inathamini uwepo wa vyama vya upinzani na wanataka wakosolewe na kupewa mawazo mbadala.

"Kwa bahati mbaya hawa wenzetu kazi yao ni kukosoa tu" amesema
Pia, Katibu huyo aliutaka upinzani utambulike kwa itikadi za vyama vyao badala ya kuonekana mtu zaidi ya chama.

"Kama chama kinachojinasibu kuwa ni mpinzanii mkuu na ninachelea kukiita mpinzani na ninashukuru wameshindwa vibaya, ukimtoa yule kiongozi wao na wapambe wake wa karibu Kinabaki nini, ACT Wazalendo ukimtoa mjomba kinabaki nini.”

"Wajenge kwanza itikadi ya vyama vyao itambulike, CCM ni taasisi inayotambulika kiitikadi" amejinasibu Polepole.

Chanzo: Mwananchi
Katika mfumo wa vyama vingi naomba kujua kuwa ccm ilipata usajili tarehe ngapi?
 
Tatizo la umasikini wa Tanzania na Afrika si rasilimali au ni viongozi na uwezo wa kupambunua mambo.Tupitie hoja
"Hivi punde, post: 28420500, member: 426068"]Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hakupaswa kufanya sherehe na Polisi kwa sababu kuna mahali hali haikuwa shwari na wao walikaa kimya.
Mwenezi analiona tatizo kwa jicho la chama, kwamba, kuna mahali hali haikuwa nzuri hivyo sherehe haikupaswa kufanywa

Pengine angekemea tabia ya viongozi kuhusisha vyombo vya usalama ktk shughuli za kisiasa
Aliyechukua video ndani ya '' police barracks' ni mtu wa ''ndani '' ni kwanini alitoa kwa jamii?
Kwamba, askari walikuwa na kiongozi wa mkoa wakisherehekea, muda mfupi baada ya matokeo ya uchaguzi!

Ni jambo la hatari. Ndani ya Polisi kuna wenye mitazamo tofauti ya kisiasa.
Kinachowazuia ni sheria. Inapotokea hivi, ipo siku tutasikia makundi mengine katika chombo, ndicho tunachopanda?

Kwa upande mwingine, Pole pole alipaswa kukemea sherehe ndani ya ofisi za dola
Kwa maneno yake tatizo si askari kusherehekea bali walifanya kukiwa na hali isiyo shwari !!

Ndipo Tume ya uchaguzi na Msajili wa vyama wanapojikuta na maswali magumu
Amesema Chadema wanasema Jeshi la Polisi linawasaidia CCM ilihali aliyekuwa mgombea ubunge wa chama chao kwenye Jimbo la Ukonga Asia Msangi alimkwida msimamizi wa uchaguzi mbele ya Polisi na walikuwa wametulia.
Alitoa taarifa kunakohusika kama inavyosemwa kila siku?

Polepole anaweza kuwa sahihi, pengine eneo hilo lilikuwa na polisi walioona tatizo. Pengine walikuwa na hisia zao kama zile za wale walioangusha 'bash' la nguvu
"Makonda hakupaswa kufanya sherehe nao kwa sababu kuna mahali sheria ya tume ilikuwa inakiukwa na wao wapo wametulia" amesema Polepole.
Kama si kukiukwa anakosema sherehe ilikuwa sahihi.Haoni tatizo RC akiwa na Police wanatumbuika ndani ya kambi
Amesema pamoja na yote CCM inathamini uwepo wa vyama vya upinzani na wanataka wakosolewe na kupewa mawazo mbadala.
Vema ,neno 'WAKOSOLEWE' na MAWAZO MBADALA
"Kwa bahati mbaya hawa wenzetu kazi yao ni kukosoa tu" amesema
Sijui alimaanisha nini kuhusu 'wanataka wakosolewe' halafu analaumu wakikosoa hivi hajui kuwa mawazo mbadala ndiko kukosoa kwenyewe
Pia, Katibu huyo aliutaka upinzani utambulike kwa itikadi za vyama vyao badala ya kuonekana mtu zaidi ya chama.
Haelewi unapomchukua mbunge wa upinzan aliyechaguliwa kwa itikadi ya CDM, akahamia CCM na ''kushinda' hapo hakuna itikadi ya CCM.
Huyu aliyehama ndiye itikadi siyo chama.Wenye itikadi za CCM wanaimba na kuvaa kofia. Hawa wanaokuja na kupewa ubunge hawana itikadi, lini wameelewa itikadi ya CCM?
"Kama chama kinachojinasibu kuwa ni mpinzanii mkuu na ninachelea kukiita mpinzani na ninashukuru wameshindwa vibaya, ukimtoa yule kiongozi wao na wapambe wake wa karibu Kinabaki nini, ACT Wazalendo ukimtoa mjomba kinabaki nini.”
Wameshindwa vibaya! Watashindaje ikiwa kuna sherehe!! mamlaka zinazohusu vyama na uchaguzi zikiwa kimya!
"Wajenge kwanza itikadi ya vyama vyao itambulike, CCM ni taasisi inayotambulika kiitikadi" amejinasibu Polepole.
CCM ina itikadi gani ?Hivi yanayoendelea ni itikadi? Leo mtu analala CDM na ACT kesho CCM,ana itikadi gani?
Kama itikadi ni kitu rahisi kama hicho, kuna tatizo kubwa kuliko itikadi

Ukimsikiliza huyu ni kiongozi yupo makini na ushindi, hana habari ya kugeuza vituo vya Polisi kuwa maeneo ya sherehe na kwamba hilo lina ujumbe mbaya kwa jamii

Polepole ajiulize kwanza, video imetokaje nje ya kituo cha Polisi?
Nani kaitoa na kwa maana gani?

Pascal Mayalla JokaKuu Mag3
 
Bashite, police na polepole wote 3 uelewa wao wa wastani, what do you expect!
 
Back
Top Bottom