Polepole: Makonda hakupaswa kufanya sherehe na Polisi

I said it, Makonda anaipotezea CCM kwa kiki binafsi.
Ni suala la kushangaza, kama si la kukera, mkuu wa Mkoa wa Dsm, Paul Makonda kushangiliwa na kubebwa juu kwa juu na POLISI!!

ANGEBEBWA NA WANA CCM hilo ni suala lingeeleweka na kuonekana kuwa chama kimeshinda.

Sasa Mtu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa, akipongezwa na vyombo vya usalama, kwa ushindi wa CCM!

Nategemea hapa IGP, Kamanda Sirro atawachukulia hatua askari wake kwa kuingilia mambo ya siasa katika nchi ya demokrasia.

MIMI MWANA CCM, na sioni mantiki ya kuipongeza serikali badala ya kuipongeza CCM.

Bashiru Ally, Katibu Mkuu CCM, na hata Polepole, mko wapi kukemea uozo huu.

Waswahili husema ukimwendekeza sana mtoto, atachezea shilingi chooni.

Makonda anachezea Shilingi ya CCM chooni.View attachment 869509
 
Hivi uchaguzi ungekwenda vizuri Na polisi wakalinda amani ipasavyo,mbunge wa upinzani akaibuka kidedea!!!Je,mkuu wa mkoa angeagiza sherehe ifanyike kushangilia amani kipindi cha uchaguzi?
Kinachosherehekewa ni amani kulindwa au ni ccm kushinda?????
Amani kulindwa...
 
Kama kahujumu uchumi wa nchi na bado yuko ofisini sembuse kula bata na police
 
Polisi tenda wema nenda zako. Hata ccm isipowashukuru Leo mbingu na nchi zinashuhudia kazi nzuri mnazowafanyia. Msivunjike moyo, maana wakati mwingine shukrani ya punda mateke lakini haiwezi kuwa mwisho wa kumtumia punda. Mnafanya kazi nzuri sana kwa kukibeba Chama chetu na Watanzania wanaona na Dunia nzima inaona. Haya maneno mengine ya kupindisha ukweli huku yakionesha dharau dhidi ya kazi yenu nzuri iliyopelekea mkapongezwa na Kada Mkuu wa Chama hicho Mkoa wa Dsm ni ya kupuuza tu. Hata aliyeyaongea anajua alikuwa hasemi ukweli, anajua anatania, lakini hawezi kusema hadharani anatania. Endeleeni kukibeba Chama maana hamna namna nyingine isipokuwa kutekeleza amri toka juu. Polepole si msemaji wa mwisho kwenye chama , wa mwisho yupo na mnamjua, na huyu mliyeaherehekea naye ni mtoto mkubwa wa huyo Bwana Mkubwa. Sasa Polepole ni nani hadi apingane na Prince Paul?
Mkuu umeandika
 
Jamani hivi itikadi ya ccm ni nini, maana ,mimi ninayoifahamu ni ya ununuzi wa wabiunge na madiwani
 
Inashangaza sana, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa dar, mheshimiwa Makonda kupongeza vijana wake kwa kazi nzuri ya kulinda amani kipindi cha kampeni mpaka uchaguzi kumalizika kwa amani ,limepewa sura ya kisiasa na baadhi ya wajuvi.kipi cha ajabu?,jeshi letu la polisi tusilikatishe tamaa kwa mitizamo ya baadhi yetu ,yenye lengo la kupotosha jamii kwa maslahi binafsi.
jeshi hili hubebeshwa lawama kila uchao hata kama baadhi ya kazia hizo hawahusiki moja kwa moja,licha ya uchache wao na changamoto ya vitendea kazi.
Leo wameweza kuleta utulivu nayo imekua nongwa kupongezwa?hamfahamu kwamba lawama zisizo na msingi zikizidi zinaua morally ya mtumishi yoyote yule ?

Mfano mwingine ,hapo nyuma ujambazi mkoa wa dar kila siku ilikua ni mauaji na wizi wa fedha,wafanyabiashara amani ilitoweka,panya road,dhulma,utapeli,kusambaa kwa dawa za kulevya mitaani,lakini angalau ahueni kwa sasa,kwa nini mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama asijipongeze na vijana wake kutambua kazi yao?,mnyonge mnyongeni ,haki yake mpatieni.
Imekua nongwa kila afanyalo Makonda tena in a positive way ,lakini kelele zisizo na msingi ndo huvurumuka toka vichakani,au hua jiwe limewapata?
Namaliza kwa kusema kitendo alichokifanya Makonda ni sahihi na hakiitaji mjadala,sifa ya Makonda ni ubunifu na uwajibikaji ,tejenge taasisi zetu,zinaporomoka kila kukicha,
 
Back
Top Bottom