Polepole: Makonda hakupaswa kufanya sherehe na Polisi

Polepole: Makonda hakupaswa kufanya sherehe na Polisi

Ndo uzuri wa chama cha mapinduzi, wanatofautiana mitizamo wakiwa chama kimoja na maisha yanaendelea, hebu jaribu chagadema umpinge Mbowe kama utasavaivu, thubutu!,utaishia kuitwa msaliti tu, Mbowe ni chairman wa maisha

Mkuu umemezeshwa code, muda wote unazirudia hizo hizo kama vile vispika vidogo vya wamachinga wauza dawa za mende.
 
CCM na ikulu wana propaganda too local
Kwamba mkuu wewe nenda utasimamishwa Mkata utatoa fungu la kusaidia ABC utapoint mtu aeleze shida zake utoe order ikiwezekana mnyooshe mtumishi jukwaani

Serikali iseme hivi atokee huyu chamani apinge kuonesha hajaenda sawia na mabosi waliokipa chama kira
Pathetic 😎😎😎
 
Mungu uko wapi?
Bwana ee bwana kwa nini wasimama mbali

kwa nini kujificha na kujificha nyakati hizi


Hakika Mwenye enzi Mungu atasikia kilio chako na atakujibu kwa wakti usiotarajiwa na Wanadamu. God is still saying something to Tanzania. Just stay tuned!!!.
 
Huyu nae ni _ichaa Kama yule Mkuu, Anaongelea nini sasa...Polisi,Msimamizi,Makonda,Viongozi upinzani au Anawapa ushauri kuhusu itikadi za Vyama vyao?
Maana kama ni Wimbo Mmoja Ameanza Mchiriku ikafuata Jazz akamaliza na Reggae..
 
Mwacheni BWANA MUNGU aitwe MUNGU maana kama angelikuonyesha mwisho wako utakuwaje ungelimwomba kama una ujasiri huo ufe leo lakini ameuficha kusudi kupitia huo mwisho wako watu wajue kuwa yupo. Mtakuja kuyajutia hayo matumbo.
 
Hivi Polepole anatuona kama vile wote tumekuwa wajinga wao kuwa ccm kweli inashinda Monduli na Dar?
Acheni wizi wenu 🙂 🙂 🙂!!
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hakupaswa kufanya sherehe na Polisi kwa sababu kuna mahali hali haikuwa shwari na wao walikaa kimya.

Polepole ameyasema hayo leo Septemba 18,2018 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam akielezea sababu za ushindi wa majimbo mawili ya Monduli na Ukonga.

Amesema Chadema wanasema Jeshi la Polisi linawasaidia CCM ilihali aliyekuwa mgombea ubunge wa chama chao kwenye Jimbo la Ukonga Asia Msangi alimkwida msimamizi wa uchaguzi mbele ya Polisi na walikuwa wametulia.

"Makonda hakupaswa kufanya sherehe nao kwa sababu kuna mahali sheria ya tume ilikuwa inakiukwa na wao wapo wametulia" amesema Polepole.

Amesema pamoja na yote CCM inathamini uwepo wa vyama vya upinzani na wanataka wakosolewe na kupewa mawazo mbadala.

"Kwa bahati mbaya hawa wenzetu kazi yao ni kukosoa tu" amesema
Pia, Katibu huyo aliutaka upinzani utambulike kwa itikadi za vyama vyao badala ya kuonekana mtu zaidi ya chama.

"Kama chama kinachojinasibu kuwa ni mpinzanii mkuu na ninachelea kukiita mpinzani na ninashukuru wameshindwa vibaya, ukimtoa yule kiongozi wao na wapambe wake wa karibu Kinabaki nini, ACT Wazalendo ukimtoa mjomba kinabaki nini.”

"Wajenge kwanza itikadi ya vyama vyao itambulike, CCM ni taasisi inayotambulika kiitikadi" amejinasibu Polepole.

Chanzo: Mwananchi
Huyo tangu alipo msaliti na kuisaliti ripoti aliyo shiriki kuiandaa ya katiba mpya pendekezwa alisha jizaraulisha
 
Hivi uchaguzi ungekwenda vizuri Na polisi wakalinda amani ipasavyo,mbunge wa upinzani akaibuka kidedea!!!Je,mkuu wa mkoa angeagiza sherehe ifanyike kushangilia amani kipindi cha uchaguzi?
Kinachosherehekewa ni amani kulindwa au ni ccm kushinda?????
Ccm kushinda
 
Hii tungo ni tata.......mkuu was itikadi was chama anathibitisha RC kuwafanyia sherehe polisi waliokuwa wanatimiza majukumu yao ya kazi!........nasubiri kumsikia mjamaa Bashiru atalisemeaje hili.
Wewe subiri upandoshwe kwenye tipa kama mchanga ukashangilie
FB_IMG_1536771315632.jpeg
 
Ndo uzuri wa chama cha mapinduzi, wanatofautiana mitizamo wakiwa chama kimoja na maisha yanaendelea, hebu jaribu chagadema umpinge Mbowe kama utasavaivu, thubutu!,utaishia kuitwa msaliti tu, Mbowe ni chairman wa maisha
Nakuona Nakuona hapo mnatoka kwenye kampeini
FB_IMG_1536771315632.jpeg
 
Back
Top Bottom