Na: Idara ya itikadi na uenezi CCM Taifa.
12 May 2018
Dodoma.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole amefafanua kwa kina mahusiano yaliyopo kati ya maendeleo ya vitu na maendeleo ya watu katika mahafali ya Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu ambapo wanachama zaidi ya 1000 wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dodoma wamepatiwa vyeti vya heshima kwa kuwa wanachama wa CCM Kipindi chochote walichokuwepo chuoni.
Katika Sherehe hiyo iliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dodoma wakishirikiana na Seneti ya Vyuo na Vyuo vikuu Ndg. Polepole amewaeleza kwa kina wanavyuo hao kuwa juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha maendeleo ya watu yanapatikana na kila linalofanywa na Serikali ni kwa manufaa ya watu.
"Ujenzi wa mradi wa Reli ya kisasa, ujenzi na ukarabati wa meli ikiwemo Mv Songea na Mv Njombe katika ziwa nyasa na zingine katika ziwa Victoria na Tanganyika nikwa lengo la kurahisisha usafiri na usafirishaji, mradi wa umeme kinyerezi 1, 2, 3 na Stigler's Gorge ni kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa umeme kwa uhakika na bei nafuu, ujenzi wa mabarabara, dawa hospitalini sasa zinapatikana kwa karibu asilimia 90%, mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu kila mwaka kwa sasa ni zaidi ya Bilion 400 na, yote haya na mengine mengi ni kuhakikisha, kufanikisha na kuhamasisha maendeleo ya watu wa Tanzania, kwa sababu maendeleo ya watu na vitu yanategemeana" amesisitiza Ndg. Polepole
Aidha Ndg. Polepole amesema Chama kitaendelea kuielekeza na kuisimamia Serikali katika suala la ajira ili kuhakikisha kuwa ajira kwa vijana zinaendelea kupatikana.
Wakati huo uo Ndg. Polepole ametumia hadhara hiyo kuwakumbusha wanafunzi kusoma kwa bidii na kuendelea kujibidiisha kutafuta maarifa kwa kujisomea hata watakapo hitimu masomo yao kwa faida ya jamii nzima kama ilivyokwenye ahadi namba (6) ya mwanaCCM
"Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia Elimu yangu kwa faida ya wote".
[HASHTAG]#HapaKaziTu[/HASHTAG]