Kwako Katibu Mwenezi CCM Taifa, ndg Polepole.
Nimesikitishwa kama si kukerwa na kauli yako ya majuzi, ati kushindwa kwa CCM Mbeya ni kutokana na ukabila.
Sisi wana CCM tutokao Mbeya tumekereka sana na kauli hiyo kwani inakosa kukubali madudu makubwa yaliofanywa na CCM Taifa kwa mkoa wa Mbeya miaka kadha iliyopita.
Polepole , jiulize sasa kama ni ukabila, Sugu ambaye wala si Mnyakyusa, Msafwa, Mpangwa au Mkinga, anapata nguvu toka kabila gani?
Kuto analyse na kukubali makosa ni kama mbuni anayeficha kichwa shimoni huku kiwiliwili chake kiko nje na kuendelea kudhuriwa.
Cha msingi CCM Taifa iwe na political scientists, Sugu kawaunganisha VIJANA, kuprotest against in action ya CCM kimaendeleo mkoani Mbeya.
CCM isijitie kutoliona hili, na hii ni pamoja na Sugu kutokuwa na uwezo wowote kuleta maendeleo mkoani Mbeya.
Tukirudi nyuma , ni CCM Taifa iliyopandikiza mbegu ya ufarakano kati ya makundi ya mtandao wa JK huko miaka ya nyuma.
Vinara wa CCM wanaojulikana, wakasema na kusikika , wako wapi?
CCM Taifa devided, but they failed to rule!
Mbona Polepole kijana wa juzi hutaki kuwasikiliza hao wazee waliopigwa mikwara?
Tunakumbuka ugomvi wa kiti cha uNEC mkoa wa Mbeya?
Mpendwa wa wana Mbeya wote kupigwa vita ya waziwazi na CCM Taifa?
Mbaya zaidi kwa karibia miaka 20 mkoa wa Mbeya , CCM Taifa imewaletea miradi gani ya maendeleo?
Miaka 20 ni mingi, sasa kijana wa miaka 20~30 mkoani Mbeya anaielewaje CCM kama chama cha kuleta maendeleo na ajira au ni chama cha maneno matupu?
Vijana haohao wakienda Mwanza na kwingineko si wanaona jinsi CCM inavyowaletea wananchi maendeleo?
Na hata Rais wetu mpendwa Magufuli, alipokuwa waziri wa ujenzi, na sasa Rais, ni miradi ipi ya ujenzi kaleta Mbeya?
Barabara ya kuingia Mbeya mjini ni kero tupu!
Polepole tusitafute wa kulaumu, jilaumuni wenyewe.
Miaka ya nyuma CCM Mbeya was a staunch CCM base.
Mtaji huo mmeupoteza wenyewe.