Polepole, chanzo cha CCM kushindwa Mbeya ni CCM Taifa

Polepole, chanzo cha CCM kushindwa Mbeya ni CCM Taifa

Ukabila on the rise,..sijui mkinga,sijui Myakyusa sinui mnanihii....wazanzibari CCM, si mnaona wakubwa zenu watanganyika wamejaa ukabila,...,achaneni nao hawa wakabila kaane pamoja muendeleze nchi yenu,
Mkuu hicho ndo kimetukera zaidi.
Kijana mdogo Polepole kujaribu kulikuza tatizo la kufikirika!
Mshangao wa wengi ni kwamba ,je kwa mafanikio yao CHADEMA, wao wamefanikiwa kutatua tatizo hilo la kufikirika la ukabila?

Tusijidanganye.

Ni vyema Polepole mwenye nafasi kubwa CCM akatumia hekima na kujua ukweli wa matatizo ya CCM mkoani Mbeya.

CCM Taifa ina mkono wake tatizo la CCM Mbeya, na tuanzie pale alipowekwa ajenti wa CCM Taifa ndg Mwakipesile, Mkuu wa Mkoa wakati huo.
Alitumika na kuharibu kuwaridhisha Team JK na Mtandao.
Mis diagnosis ya tatizo utapata wrong medicine, na tatizo haliponi!
 
Dada dr Tulia kwa sasa yupo kazini mbeya ,majuzi kati hapa kagawa mifuko ya cement kwa SHULE zote jiji mbeya.
Wakati wanachsngishwa au hamlijuihili
IMG_20180314_175834.jpg
 
Mwandosya si alikuwa waziri toka mbeya, Mwakyembe naye si ametokea Mbeya, naibu spika pia si alitokea huko huko na yule aliyekuwa naibu waziri wa elimu ambaye hajui tofauti ya Zimbabwe na zanzibar pia si alitokea huko huko kama hao wote walikuwa jikoni na wameshindwa kuwafanya mpate maendeleo msitafute sababu hata aliyekuwa mkurugenzi usalama wa Taifa Apson pamoja na wakuu wa majeshi wawili wote wametokea huko huko Mboma na Mwamunyange mnahitaji upendeleo upi zaidi ya huo
Walijisahau hao
 
Sahihisha usemi ndugu yangu.
Sugu , Joseph Mbilinyi, Mngoni, ni Form IV failure toka Songea aliyehamia Mbeya baada ya maisha kumwendea kombo kwao.
Kweli ww ndiye failure kabisa,, unaandika vitu ambavyo huvijui kabisa,, Sugu amesoma Mbeya day na Mwalimu wake ni Mpesya na Sugu ni Mkinga siyo Mngoni toka lini jina la Mbilinyi likawa la Kingoni,,, mkuu acha mihemuko
 
Kweli ww ndiye failure kabisa,, unaandika vitu ambavyo huvijui kabisa,, Sugu amesoma Mbeya day na Mwalimu wake ni Mpesya na Sugu ni Mkinga siyo Mngoni toka lini jina la Mbilinyi likawa la Kingoni,,, mkuu acha mihemuko
Mkuu ujibu huu mhemuko.......

Mr. II(Sugu)



Joseph Mbilinyi (born 1 May 1972), known for his stage names Mr. II and Sugu and 2-proud, is one of the founders of the hip hop music scene in
Tanzania. He was also elected to the Tanzanian Parliament in 2010 and then 2015 to 2020.[1]

Honourable Osmund Mbilinyi
MP
Member of Parliament
for Mbeya City


Incumbent


Assumed office
November 2010
Preceded by Benson Mpesya
Personal details
Born (1972-05-01) 1 May 1972 (age 45)
Nationality Tanzanian
Political party
CHADEMA


Mr. II was stems from
Songea in Southern Tanzania, started to rap in 1990, in his youth when he was still in school. His inspirations were Ice Cube, Niggaz With Attitude and above all Tupak Shakur. Mr. II was the first Tanzanian rap artist to have major success with his music. Through his music and language he express and addresses politics, social inequalities and other problems that affected Tanzanians

Source: Wikipedia

Angalizo:
Sio wote tunatoka Mbeya, sahihisha hiyo info iko mtandanoni kama upendavyo
 
RIP JF- Siasa, nyuzi halisia zinafutwa faster! Nadhani wamepata wahariri uhuru na mzalendo.
 
Kwako Katibu Mwenezi CCM Taifa, ndg Polepole.
Nimesikitishwa kama si kukerwa na kauli yako ya majuzi, ati kushindwa kwa CCM Mbeya ni kutokana na ukabila.

Sisi wana CCM tutokao Mbeya tumekereka sana na kauli hiyo kwani inakosa kukubali madudu makubwa yaliofanywa na CCM Taifa kwa mkoa wa Mbeya miaka kadha iliyopita.

Polepole , jiulize sasa kama ni ukabila, Sugu ambaye wala si Mnyakyusa, Msafwa, Mpangwa au Mnyiha Mkinga, anapata nguvu toka kabila gani?

Kuto analyse na kukubali makosa ni kama mbuni anayeficha kichwa shimoni huku kiwiliwili chake kiko nje na kuendelea kudhuriwa.

Cha msingi CCM Taifa lazima iwe na political scientists wenyebuwezo wa ku analyse mspungufu ya chama na kupendekeza marekebisho.
Sugu kawaunganisha VIJANA mkoa wa Mbeya, kawaunganisha kuprotest against in-action ya CCM kimaendeleo mkoani Mbeya.

CCM isijitie kutoliona hili, na hii ni pamoja na Sugu kutokuwa na uwezo wowote kuleta maendeleo mkoani Mbeya.

Tukirudi nyuma , ni CCM Taifa iliyopandikiza mbegu ya ufarakano kati ya makundi ya mtandao wa JK huko miaka ya nyuma.
Vinara wa CCM wanaojulikana, wakasema na kusikika , wako wapi?
CCM Taifa devided, but they failed to rule!
Mbona Polepole kijana wa juzi hutaki kuwasikiliza hao wazee waliopigwa mikwara?

Tunakumbuka ugomvi wa kiti cha uNEC mkoa wa Mbeya?
Mpendwa wa wana Mbeya wote kupigwa vita ya waziwazi na CCM Taifa?

Mbaya zaidi kwa karibia miaka 20 mkoa wa Mbeya , CCM Taifa imewaletea miradi gani ya maendeleo?
Miaka 20 ni mingi, sasa kijana wa miaka 20~30 mkoani Mbeya anaielewaje CCM kama chama cha kuleta maendeleo na ajira au ni chama cha maneno matupu?

Vijana haohao wakienda Mwanza na kwingineko si wanaona jinsi CCM inavyowaletea wananchi maendeleo?
Na hata Rais wetu mpendwa Magufuli, alipokuwa waziri wa ujenzi, na sasa Rais, ni miradi ipi ya ujenzi kaleta Mbeya?
Barabara ya kuingia Mbeya mjini ni kero tupu!

Polepole tusitafute wa kulaumu, jilaumuni wenyewe.
Sehemu kama Iibighi(Rungwe), Tunduma(Songwe) ambazo predominantly ni kabila moja, mbona CCM innaeendelea kuhenyeshhwa?
Ni bora tujiulize tulipo kosea ili kama Mwalimu alivyosemma,Tujisahihishe..
Miaka ya nyuma CCM Mbeya was a staunch CCM base.
Mtaji huo mmeupoteza wenyewe.
SIKWAGHILE MALAFYALE Macho pa Ugali. Wewe ni mfagiliaji mkubwa wa Chama twawala! Lakini jambo moja umeoneshwa jinsi gani watu wa Mbeya tulivyo na misimamo! Bhalinga twangaliligha abho! Asseeeee!!
 
SIKWAGHILE MALAFYALE Macho pa Ugali. Wewe ni mfagiliaji mkubwa wa Chama twawala! Lakini jambo moja umeoneshwa jinsi gani watu wa Mbeya tulivyo na misimamo! Bhalinga twangaliligha abho! Asseeeee!!
Mkuu inakera sana wana CCM Mbeya kwa muda mrefu tumechezewa rafu na CCM Taifa.
Polepole anaongeza chumvi kwenye kidonda, leo anatokea na anatoa sababu ambazo yeye mwenyewe anajua ni za kuwafurahisha wakubwa wake tu.

Sisi watu wa mkoahuo hatunaga aibu ya to call a spade a spade, bila kumung'unya maneno.


Hapa Polepole ametuudhi wana CCM kwa kweli.
 
Back
Top Bottom