Uchaguzi 2020 Polepole: CCM inawataka wagombea wote waliofeli kura za maoni kuwapigia kampeni washindi watakaokaidi kukosa teuzi!

Hiyo ni ngumu sana na asahau hilo jambo.

Yaani Watumishi wa Umma ambao ni makada wa CCM zaidi ya elfu 7 waliojitokeza kukipigania chama huko majimboni - Serikali hii hii ya CCM imewanyima mishahara ya miezi miwili ( mwezi wa saba na huu wa nane), leo hii eti waende wakakipigie kampeni CCM huko majimboni, hao makada anawaona ni wajinga enhee?

Sasa subiri waone kitachotokea. Mtu atoke Dar aende Mbeya kukipigia kampeni CCM wakati Mshahara hana, nguvu hiyo ataitoa wapi?
Mwambie pole pole aache ufala ! Wao wasubiri maana dharau zao sasa zitawatokea puani.
Ukweli watumishi hawa wanaumia sana. Yawezekana waliotoa adhabu wakaona kawaida tena sana lakini kwa kifupi wanyonge hawa na familia zao wanalilia mioyoni.
 
Kumbe ndo maana takukuru iliona iwarejeshee wala/watoa rushwa wao kwa kile ilichodai ccm ina internal mechanism ya ku-deal na rushwa na wala/watoa rushwa. Haya ya polepole nayo ni mwendelezo wa hiyo rushwa.

Tuliambiwa watia nia walikuwa ni zaidi ya 15,000 leo hii namba yote hii iteuliwe ktk nafasi za ulaji mbalimbali naona ccm inakoelekea inataka kufuta nafasi zote za ajira ifanye nafasi zote ziwe za kuteuliwa ili ku-command respect, utii na woga kwa umma huu.

Polepole anawaza 'kitoto' sana! Amekosa sifa za kuwa Mwenezi wa chama chake. Amekosa ushawishi kwa wanachama wenzake hasa nyakati hizi za uchaguzi. Ameanza kutangaza rushwa kwa wapiga debe wa wagombea. Amechoka.

SAD!
 
Back
Top Bottom