Uchaguzi 2020 Polepole: CCM inawataka wagombea wote waliofeli kura za maoni kuwapigia kampeni washindi watakaokaidi kukosa teuzi!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,447
Katibu wa uenezi wa CCM ndugu Polepole amewataka wagombea waliofeli kwenye kura za maoni wawapigie kampeni walioshinda pindi kampeni zitakapofunguliwa.

Polepole amesema CCM ni chama kikubwa tena ni taasisi ya Umma hivyo ina vyeo na fursa nyingi kwahiyo wale watakaokaidi kukampenia wenzao watakosa teuzi siku za usoni.

Chanzo: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
 
Hiyo ni ngumu sana na asahau hilo jambo.

Yaani Watumishi wa Umma ambao ni makada wa CCM zaidi ya elfu 7 waliojitokeza kukipigania chama huko majimboni - Serikali hii hii ya CCM imewanyima mishahara ya miezi miwili ( mwezi wa saba na huu wa nane), leo hii eti waende wakakipigie kampeni CCM huko majimboni, hao makada anawaona ni wajinga enhee?

Sasa subiri waone kitachotokea. Mtu atoke Dar aende Mbeya kukipigia kampeni CCM wakati Mshahara hana, nguvu hiyo ataitoa wapi?
Mwambie pole pole aache ufala ! Wao wasubiri maana dharau zao sasa zitawatokea puani.
 
Wale watoa rushwa walikatwa?!
Nani alisema ni kigezo cha rushwa tu ndicho kilitumika kupata wateuliwa. Kulikuwa na vigezo vingi vya kutumia kumpata anayestahili kuwakilisha wanaCCM kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Kutotumia rushwa kupa kura za wajumbe, kuwa na uwezo wa kuwakilisha vema na kwa umakini wananchi, uzalendo usio tiliwa shaka na mambo mengine kama hayo, ndiyo yalitumika kupata nafasi kuwakilisha CCM katika uchaguzi wa 28.10.2020. Kwa hiyo si kutotumia rushwa pekee kilikuwa kigezo cha kupata nafasi ya uwakilishi kwenye uchaguzi. Upo!?
 
Hii ni kutwika mtu gunia la misumari. Sisi wajumbe tumemchagua mtu kwa kura nyingi, mkatuletea wa kura 5 kisa kaunga juhudi Mkono. Mkaacha anayetekeleza ilani na kusababisha juhudi kuonekana. Wanachama wetu hawamtaki, alitutesa katika uchaguzi uliopita, hatukulala, kutwa kucha tuko kwenye kampeni kumtetea mbunge na Rais wetu, yeye anatukana na kukashifu. Leo kawa mzuri kuliko wafia chama? Wakati huohuo wwapinzani hawamtaki, kasaliti chama Chao. Leo tuambiwe tukapige kampeni la sivo hakuna uteuzi! Hizo teuzi za kutosha waliokatwa wote zitatoka wapi? Au tutaunda taifa jipya? Hiyo siyo rushwa ya teuzi? Hiki Ni chama au kambi ya jeshi, au shule na polepole ni mwalimu Mkuu?
 
Back
Top Bottom