Uchaguzi 2020 Polepole: CCM inawataka wagombea wote waliofeli kura za maoni kuwapigia kampeni washindi watakaokaidi kukosa teuzi!

Hiyo ni ngumu sana na asahau hilo jambo.

Yaani Watumishi wa Umma ambao ni makada wa CCM zaidi ya elfu 7 waliojitokeza kukipigania chama huko majimboni - Serikali hii hii ya CCM imewanyima mishahara ya miezi miwili ( mwezi wa saba na huu wa nane), leo hii eti waende wakakipigie kampeni CCM huko majimboni, hao makada anawaona ni wajinga enhee?

Sasa subiri waone kitachotokea. Mtu atoke Dar aende Mbeya kukipigia kampeni CCM wakati Mshahara hana, nguvu hiyo ataitoa wapi?
Mwambie pole pole aache ufala ! Wao wasubiri maana dharau zao sasa zitawatokea puani.
Sijui amekula nn ? Huyo mtu anaenda kwa miguu kwenye hizo kampeni,yeye anafikiri kukosa mshahara ni jambo dogo
 
Hahaha ccm mijinga sana na itaamini, vyeo vingapi mtapata nyie?! Na waliopo kwenye nafasi hizo mtawaua au mtawapeleka wapi?!
 
Katibu wa uenezi wa CCM ndugu Polepole amewataka wagombea waliofeli kwenye kura za maoni wawapigie kampeni walioshinda pindi kampeni zitakapofunguliwa.

Polepole amesema CCM ni chama kikubwa tena ni taasisi ya Umma hivyo ina vyeo na fursa nyingi kwahiyo wale watakaokaidi kukampenia wenzao watakosa teuzi siku za usoni.

Chanzo: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
Inahitaji kuwa na moyo mkubwa; hasa walioshika nafasi ya kwanza kwenye kura za maoni na wakaenguliwa kugombea. Wao wanaona uwazi uliotawala kura za maoni ilikuwa danganya toto kumbe chama kilikuwa na watu wake - hasa waliohamia kutoka upinzani. Wahanga hawa wanajisikia kutotendewa haki. Vyeo vya kuteuliwa ni bahati na sibu. Probability ya kupata ni ndogo sana.
 
Nchi hii ina wajinga wengi sana
Kweli kabisa lakini wengi zaidi wako CCM kina mvuto sana kwa wajinga. Haitashangaza kumwona Mtemi wa vijisenti wa Harvard University akimfanyia kampeini waliombwaga wakina Musukuma au Kibajaji au hata Yule kijana wa kuunga mkono juhudi aliyembwaga Jimboni. Viongozi Serikalini na Chamani ni vitisho vinatawala na kuimba mafanikio ya Awamu ya Tano kila wakati na kila mahali lakini hakuna kinachoongoka kwa sababu watendaji hawateuliwi kwa uwezo na uzoefu bali kwa kuunga mkono juhudi ambazo hazipo.
 
Bwashee yule Kinanasi amepita kura za maoni?
Ndio mgombea wa ccm Kyela , ukiacha rushwa ya pikipiki aliyowahonga makatibu kata wote wa ccm kyela nzima na kuwapa wajumbe laki tatu tatu , hana ushawishi mbele ya wananchi na wala hana uwezo wa kuomba kura , wengi wanaamini kukosa kwake hata elimu ya sekondari kumemtia zege mdomoni , Mbunge ajaye Kyela ni Alinanuswe Mwalwange kutoka Chadema
 
Katibu wa uenezi wa CCM ndugu Polepole amewataka wagombea waliofeli kwenye kura za maoni wawapigie kampeni walioshinda pindi kampeni zitakapofunguliwa.

Polepole amesema CCM ni chama kikubwa tena ni taasisi ya Umma hivyo ina vyeo na fursa nyingi kwahiyo wale watakaokaidi kukampenia wenzao watakosa teuzi siku za usoni.

Chanzo: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
Ccm sio mama yangu wala baba yangu
Ef7SJLlXoAYKYkX.jpg
 
Polepole sisi wa kampeni mitandaoni hizo teuzi hazi tuhusu sio unaangalia waliokatwa tu.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom