Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,830
- 976
Ndugu zangu, salamu.
Napenda kuchukua fursa hii kukishukuru chama changu kwa kuendesha vizuri mchakato wa kura za maoni kwa ngazi ya majimbo na viti maalumu. Ni imani yangu kuwa michakato mingine itaendelea vyema kwa ngazi zinazofuatia.
Ninajua zipo changamoto ndogondogo za madai ya rushwa, ukiukwaji wa taratibu n.k ila kwa leo sio lengo langu kujadili changamoto hizo. Itoshe kusema kuwa CCM imejiwekea utaratibu mzuri wa kushughulikia changamoto hizo na ndio maana mchakato utaenda mpaka ngazi ya taifa. Hongera sana CCM.
Sisi wote ni mashahidi wa utitiri wa watia nia ya ubunge kwa tiketi ya CCM. Ona mafukara, matajiri, wasanii, wasomi na wasio wasomi ukimiminika majimboni. Wavivu wa kufikiri wanaweza kumchukulia kirahisi, wenyewe wanasema poa hali hi ila kwa watu werevu hili ni jambo fikirishi. Usione vyaelea, vimeundwa.
CCM ipo, itaendelea kuwepo na kushinda chaguzi kwasababu ni chama kilichopo mioyoni mwa watanzania. Hi ni kwasababu moja tuu, CCM ni chama kinachojifanyia tathimini na kukumbatia mabadiliko chanya kutokana na wakati.
Ilikuwa vigumu sana hapa juzi Kati kwa mwanaCCM wa kawaida, asiye na pesa kupata fomu na kutia nia ya ubunge. CCM ikakaa na kutathimini, ikaja na utaratibu wa sasa na motokeo tumeyaona. CCM imeonesha kuwa inapendwa na makundi yote. Wakati Kuna vyama vinatafuta wagombea, hali ni tofauti kwa CCM. Makumi kwa mamia walijitokeza.
Hi sio bahati mbaya, uongozi mzuri umeleta haya. Hongera mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa JMT Dr. ndugu John Magufuli na viongozi wote akiwemo mzee Mangula, komredi Dr Bashiru, ndugu Polepole, ndugu Heri n.k. CCM imeimarika zaidi katika uongozi wenu.
Tunawatakia heri na fanaka katika kazi iliyo mbele yenu. Tutashiriki kwa hali na mali katika kampeni na kuhakikisha CCM sio tuu inapata ushindi bali inapata ushindi wa kishindo kizito.
Vijana, wazee na akina mama ambao sio wanaCCM, karibuni CCM, karibuni sehemu salama
#tukutanekwenyekampeni