Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 2,209
- 4,706
Mkutano na waandishi wa habari utaanza saa 8 mchana kutokea ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba
==========
UPDATES:
Chama cha Mapinduzi kinatoa aarifa rasmi ya kifo cha ndugu yetu na mpendwa wetu, John Pombe Joseph Magufuli, ambaye amekuwa Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
CCM safu yake ya uongozi na wanachama, tumepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha mpendwa wetu Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakuu wa Chama waliopo, Mzee Philip Mangula; Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara na Mzee Ali Mohammed Shein, Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, wameshauriana na kukubaliana kuwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa iketi kwa kikao maalum siku ya Jumamosi ya Tarehe 20 ya Mwezi huu wa Machi 2021, saa 8 mchana, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu, Lumumba, Jijini Dar es Salaam.
Aidha, taarifa inatolewa kwamba Chama kitakuwa na Maombolezo ya Siku 21 sambamba na tangazo la serikali. Wakati wote huo, bendera za Chama cha Mapinduzi zitapepea nusu mlingoti.
Kutakuwa na kitabu cha salamu za rambirambi na maombolezo katika ofisi ya makao makuu ya CCM (White House) hapa jijini Dodoma.
Lakini kitakuwepo pia kitabu cha kupokea rambirambi na maombolezo katika ofisi zetu za Chama, Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi Kisiwandui, Zanzibar
Kitakuwepo pia kitabu cha maombolezo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, Jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Chama unawaomba sana wanachama wote wa CCM, watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu, Watanzania wote kwa ujumla, kuwa na moyo mkuu na kuendelea kuwa watulivu kusimama imara na kuendelea kutafakari mchango wa kipekee na wa kihistoria kwa taifa letu wa ndugu yetu na mpendwa wetu, John Pombe Joseph Magufuli.
==========
UPDATES:
Humphrey Polepole:Chama cha Mapinduzi kinatoa aarifa rasmi ya kifo cha ndugu yetu na mpendwa wetu, John Pombe Joseph Magufuli, ambaye amekuwa Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.