Polepole atoa taarifa rasmi ya CCM kuhusu kifo cha Rais Magufuli. Kamati Kuu ya Chama kufanya kikao maalum Jumamosi, Machi 20, 2021

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,156
4,510
Mkutano na waandishi wa habari utaanza saa 8 mchana kutokea ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba

==========

UPDATES:
Humphrey Polepole:
Chama cha Mapinduzi kinatoa aarifa rasmi ya kifo cha ndugu yetu na mpendwa wetu, John Pombe Joseph Magufuli, ambaye amekuwa Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

CCM safu yake ya uongozi na wanachama, tumepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha mpendwa wetu Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chama cha Mapinduzi kinatoa aarifa rasmi ya kifo cha ndugu yetu na mpendwa wetu, John Pombe Joseph Magufuli, ambaye amekuwa Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

CCM safu yake ya uongozi na wanachama, tumepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha mpendwa wetu Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakuu wa Chama waliopo, Mzee Philip Mangula; Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara na Mzee Ali Mohammed Shein, Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, wameshauriana na kukubaliana kuwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa iketi kwa kikao maalum siku ya Jumamosi ya Tarehe 20 ya Mwezi huu wa Machi 2021, saa 8 mchana, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu, Lumumba, Jijini Dar es Salaam.

Aidha, taarifa inatolewa kwamba Chama kitakuwa na Maombolezo ya Siku 21 sambamba na tangazo la serikali. Wakati wote huo, bendera za Chama cha Mapinduzi zitapepea nusu mlingoti.

Kutakuwa na kitabu cha salamu za rambirambi na maombolezo katika ofisi ya makao makuu ya CCM (White House) hapa jijini Dodoma.

Lakini kitakuwepo pia kitabu cha kupokea rambirambi na maombolezo katika ofisi zetu za Chama, Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi Kisiwandui, Zanzibar

Kitakuwepo pia kitabu cha maombolezo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, Jijini Dar es Salaam.

Uongozi wa Chama unawaomba sana wanachama wote wa CCM, watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu, Watanzania wote kwa ujumla, kuwa na moyo mkuu na kuendelea kuwa watulivu kusimama imara na kuendelea kutafakari mchango wa kipekee na wa kihistoria kwa taifa letu wa ndugu yetu na mpendwa wetu, John Pombe Joseph Magufuli.
 

Attachments

  • IMG-20210318-WA0006.jpg
    IMG-20210318-WA0006.jpg
    30.2 KB · Views: 1
Hii picha aliyoweka haikufaa kwa kipindi hiki tupo katika majonzi makubwa. Mbona anacheka au amefurahi kitu gani. Tafadhali wahusika waibadili inatuletea taharuki.
 
Polepole please toa hiyo picha, nenda na wakati. How stupid are you? You had a lot to thank Magufuli for appointing you to where you are.

What are going to tell us, crap or another vomit from CCM!
 
Mkutano na waandishi wa habari utaanza saa 8 mchana kutokea ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba

View attachment 1728666
1. Mosi; picha haiendani na wakati tulio nao kama Taifa.

2. Pili; afunge mdomo wake maana Taifa hili limefika hapa kutokana na watu wa aina yake. Sikuwaza hata siku moja watu watafurahia kifo cha kiongozi yeyote mkubwa hadharani. Haya ni matokeo ya kupanda bangi na kutegemea kuvuna mahindi.

3. Tatu; nilidhani huu ni muda wa kufanya toba kama Taifa, na siyo wa kiki kwenye vyombo vya habari
 
Hata wale vibaraka wa Lumumba wameshindwa kuweka picha kulingana na muktadha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom