Polepole atangaza moto wa 'mageuzi ya makusudi' CCM

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,615
2,000
Sio mabadiliko pekee, ni mageuzi ya makusudi pia yanayotarajiwa kushuhudiwa kwa kiwango chake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya kufanyika mabadiliko ya uongozi.

Hali hiyo imejidhihirisha kupitia kauli ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho tawala, Humphrey Polepole aliyoitoa hivi karibuni katika mahojiano na kituo cha Uhuru FM kinachomilikiwa na chama hicho.

Alisema chama hicho kinafanya mageuzi ya makusudi, ajenda ambayo alidai ingawa ilikuwapo toka awali haikupata mtu wa kuisimamia kama alivyoonesha nia Mwenyekiti wa sasa wa chama hicho, Dkt. Magufuli.

 

ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,113
2,000
Kwanza yeye si mwanaCCM, amevamia chama chetu nani asiyejua.

Polepole awaeleze wanaCCM ktk ziara zake kabla ya kuingia ccm ametokea wapi na kadi yake ya CCM mbona hailingani na umri wake.

CCM ina wenyewe wasilete ukabila na ukanda ndani ya ccm, kwanza mwenyekiti wa chama ametumia influence yake kuzifanyia mabadilikl jumuiya za chama bila kuwashirikisha wahusika.

Kwa kufuta nafasi za makatibu wa jumuiya za chama wilaya na mikoa ina maana amewafukazi kazi waajiriwa hao zaidi ya 150.

Wasituharibie chama chetu, ambacho kwa kiasi kikubwa kinabebwa na mikoa ya kusini wala sio kanda ziwa , kusini wameingiza mikoa 5 katika mikoa 10 bora iliyoongoza kwa % za CCM kupata % nyingi za ushindi.
 

Kishimbe wa Kishimbe

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
3,161
2,000
Pamoja na mapungufu ya hapa na pale ya Nape Mnauye, lakini bado viatu vyake vitampwaya sana Mr. Polepole!
HP radiates very faint power!
That's my observation! (I'm terribly sorry for whoever inconvenienced!)
NB: A good political analyst is not necessarily a great demagogue!
 

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,154
2,000
Mabadiliko ndani ya ccm ni ndoto za mtu akiwa anatembea. Huyu mjamaa ni kigeugeu wewe muumini wa serikali tatu utasimamia Sera za serikali mbili? Chizi mkubwa
Sijakuelewa! Ina maana wote waliotaka mfumo wa Serikali 3 walikuwa siyo Wana CCM?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom