Vulmeko
JF-Expert Member
- Jul 15, 2025
- 281
- 220
Nimesikiliza mara nyingi hotuba za Mheshimiwa Polepole, na nimejiridhisha pasina shaka kwamba huyu ndugu ni Mkristo, tena aliyebobea katika ujuzi wa Biblia.
Katika hotuba zake anazoziwasilisha kwa weledi wa hali ya juu, mara nyingi akimaliza episode ya kwanza, huwa anaahidi kwamba siku fulani na saa fulani ataongea tena na umma. Hata hivyo, ahadi hiyo huwa haitimii kwa asilimia mia moja. Kuna wakati anaanza kuongea mapema kabla ya muda aliousema, na wakati mwingine anachelewa sana kuanza. Of course, hiyo inaweza kuwa mbinu ya kuwakwepa wakata swichi, lakini sidhani kama jambo hilo linampendeza Mungu anayemuabudu. Mimi sio mjuzi sana wa Biblia, lakini nakumbuka kuna mahali imeandikwa kwamba tusiambiane uongo, kwakuwa tumeuvua utu wa kale; na kwamba waongo watahukumiwa adhabu.
Ndio sababu nauliza: huyu Mheshimiwa amejivua Ukristo? Kama bado, kwanini hayatimizi maagizo ya Bwana Yesu? Na je, kama malengo yake yatafanikiwa, si ataendelea na tabia hiyohiyo ya kuudanganya umma hata katika mambo nyeti?
Kwa unyenyekevu mkubwa, nawasilisha maswali yangu.