Polepole ameishajivua gamba la Ukristo?

Polepole ameishajivua gamba la Ukristo?

Nimesikiliza mara nyingi hotuba za Mheshimiwa Polepole, na nimejiridhisha pasina shaka kwamba huyu ndugu ni Mkristo, tena aliyebobea katika ujuzi wa Biblia.

Katika hotuba zake anazoziwasilisha kwa weledi wa hali ya juu, mara nyingi akimaliza episode ya kwanza, huwa anaahidi kwamba siku fulani na saa fulani ataongea tena na umma. Hata hivyo, ahadi hiyo huwa haitimii kwa asilimia mia moja. Kuna wakati anaanza kuongea mapema kabla ya muda aliousema, na wakati mwingine anachelewa sana kuanza. Of course, hiyo inaweza kuwa mbinu ya kuwakwepa wakata swichi, lakini sidhani kama jambo hilo linampendeza Mungu anayemuabudu. Mimi sio mjuzi sana wa Biblia, lakini nakumbuka kuna mahali imeandikwa kwamba tusiambiane uongo, kwakuwa tumeuvua utu wa kale; na kwamba waongo watahukumiwa adhabu.

Ndio sababu nauliza: huyu Mheshimiwa amejivua Ukristo? Kama bado, kwanini hayatimizi maagizo ya Bwana Yesu? Na je, kama malengo yake yatafanikiwa, si ataendelea na tabia hiyohiyo ya kuudanganya umma hata katika mambo nyeti?

Kwa unyenyekevu mkubwa, nawasilisha maswali yangu.
Basi nenda kamsemelee kwa binamu yako yesu,me nilijua umeandika vya maana kumbe ushuzi tu
 
Basi kama hivyo hata wachezaji wa mpira wana dhambi.

Ukitaka kumpiga mtu chenga, unatishia kama unaenda kushoto lakini unaenda kulia hiyo nayo ni dhambi maana umemdanganya mpinzani wako.

Vipi kuhusu penati zinazopigwa, unaona kabisa kipa karuka kulia na mpira unaenda kushoto.
Kwamba Gaucho motoni moja kwa moja🤣
 
Nimesikiliza mara nyingi hotuba za Mheshimiwa Polepole, na nimejiridhisha pasina shaka kwamba huyu ndugu ni Mkristo, tena aliyebobea katika ujuzi wa Biblia.

Katika hotuba zake anazoziwasilisha kwa weledi wa hali ya juu, mara nyingi akimaliza episode ya kwanza, huwa anaahidi kwamba siku fulani na saa fulani ataongea tena na umma. Hata hivyo, ahadi hiyo huwa haitimii kwa asilimia mia moja. Kuna wakati anaanza kuongea mapema kabla ya muda aliousema, na wakati mwingine anachelewa sana kuanza. Of course, hiyo inaweza kuwa mbinu ya kuwakwepa wakata swichi, lakini sidhani kama jambo hilo linampendeza Mungu anayemuabudu. Mimi sio mjuzi sana wa Biblia, lakini nakumbuka kuna mahali imeandikwa kwamba tusiambiane uongo, kwakuwa tumeuvua utu wa kale; na kwamba waongo watahukumiwa adhabu.

Ndio sababu nauliza: huyu Mheshimiwa amejivua Ukristo? Kama bado, kwanini hayatimizi maagizo ya Bwana Yesu? Na je, kama malengo yake yatafanikiwa, si ataendelea na tabia hiyohiyo ya kuudanganya umma hata katika mambo nyeti?

Kwa unyenyekevu mkubwa, nawasilisha maswali yangu.
Kojoa ulale
 
Back
Top Bottom