Polepole aandika historia ya matusi mazito kwa wanachama wa CCM

Julias Vimvinyira

Senior Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
155
Reaction score
205
KATIKATI ya upepo wa maandalizi ya uchaguzi, sauti ya matusi imeibuka akiwaita wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuwa ni “wahuni”.

Kauli hii imetolewa na mtu aliyewahi kushika nafasi ya heshima ndani ya chama hicho, aliyewekwa juu kama mzigo wa haraka uliotupwa mezani bila kuulizwa mzani wake.

Kauli hiyo haikuwashangaza wengi kwa sababu si mara ya kwanza kuonesha ishara za kujisahau na kutaka sifa kwa njia ya kuropoka.

WanaCCM waliompokea, wakamfundisha, wakamkirimia heshima ya taifa, leo hii wanatupiwa maneno machafu kwa sababu tu hawakumteua mtu anayemtaka. Yeye aliyewahi kusimama majukwaani na kusifia chama kwa kila sentensi, sasa anaona chama hicho hakina maana? Ni wazi kuwa haya si maneno ya hoja bali ni mlipuko wa kinyongo kilichosubiri nafasi ya kulipuka.

Kwa kauli yake, amedhihirisha kuwa dhamira yake haikuwa uaminifu kwa chama bali ni maslahi binafsi. Alipokuwa na nafasi, hakusema chochote kuhusu matukio ya kusikitisha kama kutoweka kwa waandishi wa habari na wanaharakati. Hakulaani, hakushtuka, hakuguswa. Leo anataka aonekane kama mtetezi wa haki na demokrasia ilhali jana alifumbia macho uovu. Ukimya wa wakati ule ni ushahidi wa unafiki wa kisiasa.

Uamuzi wa wajumbe kumpitisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa urais ulifanyika kwa njia halali na kwa maridhiano ya wazi. Kumdharau mgombea huyo ni kuwadhalilisha wajumbe wote waliotimiza wajibu wao kwa mujibu wa Katiba ya chama. Na zaidi, ni jaribio la kutikisa imani ya wanachama kwa chama chao, kwa maslahi ya mtu mmoja mwenye kiu ya umaarufu wa haraka.

Watanzania wanatambua tofauti ya mwanasiasa anayepigania hoja na yule anayepiga kelele baada ya kukosa nafasi. Kauli hii haijengi hoja yoyote, bali inabomoa hadhi ya aliyekuwa nayo. Ukweli unabaki palepale: chama hiki hakisimamishwi na jazba ya mtu mmoja, bali na misingi thabiti ya nidhamu, heshima na umoja.
 
KATIKATI ya upepo wa maandalizi ya uchaguzi, sauti ya matusi imeibuka akiwaita wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kuwa ni “wahuni”.

Kauli hii imetolewa na mtu aliyewahi kushika nafasi ya heshima ndani ya chama hicho, mtu aliyepanda juu kupitia migongo ya wanachama hao hao anaowadharau leo. Kauli hiyo haikuwashangaza wengi kwa sababu si mara ya kwanza kuonesha ishara za kujisahau na kutaka sifa kwa njia ya kuropoka.

Attachments

  • cf0ea736521de32f5d65e1a6b7fd56a4_1747824734726.mp4
    579.6 KB

Ate wewe muhuni
 
Back
Top Bottom