Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,875
Hadi muda huu ninaongea,
kuna wanafunzi wengi sana wenye vigezo hawajapata vyuo.Wana one ,two na three. Mwezi Juni 2017 ,pale UDSM Mh.Rais aliagiza wanafunzi waombe vyuo kupitia chuo chenyewe na sio TCU (Central Admission System).
Alitoa sababu kadhaa kuwa vyuo baadhi vina honga staffs kadhaa wa TCU ili wapate wanafunzi.
Kipindi hicho nilikuwa Naibu waziri wa mikopo DARUSO,hata nilipokuja kuwa Mwenyekiti-TSNP nimekuwa na msimamo wangu hadi sasa kuwa mfumo wa CAS-TCU ulikuwa imara.
Ni wazi kabisa,sababu za Mh.Rais zilikuwa za msingi sana ,watendaji wake wangemshauri kuzifanyia kazi changamoto alizozitaja kuliko kubadilisha mfumo wote.Na mimi simlaumu sababu yeye alikuwa na lengo la utatuzi wa tatizo.
Nchi yetu ina vyuo vingi sana ,vyenye majina,visivyo na majina ila pia wanafunzi au waombaji wameongezeka sana.Kinachopelekea wanafunzi kukosa vyuo ni kwamba wengi wamejikita kuomba vyuo pendwa,vikubwa na vyenye majina na kwasababu hawapo centralized katika mfumo mmoja ina kuwa ningumu sana kwao,sio rahisi wote kuchaguliwa katika vyuo hivyo hata awamu zote huku vyuo vingine visivyo na majina vikikosa wanafunzi.Kulipaswa kuwe na utoaji wa elimu na ufahamu wa kutosha kwa wanafunzi, ukizingatia mfumo wa kuomba kupitia chuo upo tofauti na ule wa CAS-TCU.
CAS (Central Admission system) ya TCU ilikuwa na uwezo kupeleka wanafunzi katika vyuo walivyoomba na kama hawana vigezo au Admission capacity ipo limited vyuo alivyoomba walikuwa wanasaidia kumpeleka mwanafunzi chuo kingine ,hata kama hajakiomba kuliko kukosa chuo.
Shida ilianzia hapo kuwa wanafunzi wanapelekwa vyuo ambavyo hawakuomba ,ni kwasababu sio wote walioomba UDSM wataenda UDSM ,au Mzumbe,au UDOM nafasi zipo limited na wanafunzi wengine huomba bila ufahamu wa vigezo (Cut point ya faculty huzika/Admission capacity ya faculty).
Hivyo CAS-TCU ikawa inawapeleka katika vyuo ambavyo ,vina nafasi ya udahili ila ambavyo wanafunzi hawakuviomba.
Sasa hivi wanafunzi wanaomba chuo moja kwa moja,wanaomba UDSM ,MZUMBE,UDOM,ARDH na NIT unakuta vyuo hivi vimeombwa na wengi ,hivyo havichukui wote hata kama wanavigezo au hawana ,wanatemwa na awamu ya pili wanaomba programs zingine katika aina ya vyuo hivi wanatemwa .Hatimaye anakosa chuo.CAS-TCU ilikuwa inaweza kumpatia chuo mwanafunzi hata kama hakukiomba kuliko kukosa kama wanavyokosa sasa.
Pia wanafunzi wengi wa Diploma waliokosa AVN hawajaomba chuo hadi sasa ,suala la AVN ni pana mno ,ni shida kubwa .NACTE inapaswa iwajibike kabisa kabisa imeshindwa kusimamia vyuo hivi vinavyotoa diploma , kupeleka matokeo kwa wakati.
Ombi langu kwa TCU,Mimi najua kuna vyuo bado vina nafasi ya udahili ,naomba dirisha lingine lifunguliwe kwa hawa wanafunzi waliokosa vyuo.Vyuo hivyo viruhusiwe kufungua dirisha .
Vijana wana shida mno ,kubwa mno kuanzia katika mfumo wa udahili upo hovyo,mfumo wa kupata AVN upo hovyo, penalty ya 10% bodi ya mikopo baada ya miaka tangu kuhitimu chuo ina umiza watu ,mfumo wa ajira upo hovyo.
Mambo yote kwa vijana yapo hovyo ,mabaraza ya vijana ya vyama (Youth wings) wapo kimya ,kila mtu yupo kimya.
Mungu azidi kutubariki .
Abdul Nondo.
abdulnondo10@gmail.com