Poleni watz wenzetu kwa kutiwa majaribuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Poleni watz wenzetu kwa kutiwa majaribuni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ze burner, Oct 20, 2011.

 1. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  habari wana jf.

  nikiwa home nimeketi kwa umakini mkubwa nikisikiliza taarifa ya habari kutoka tbc1 nikasikia habari ya chanjo mpya ya maleria ambayo kwa maelezo ya watafiti wanasema inaweza kuzuia mtu aliyechanjwa kutopata malaria kwa muda wa miaka miwili. uhakika wa chanjo hiyo ni wa asilimia hamsini. watafiti bado wanaendelea kusema kuwa licha ya chanjo hiyo kuonekana inafaa bado inabidi itumike katika hali ya majaribio kwa kwa miaka miwili zaidi kabla ya kutumika rasmi.

  Kilichonishtua zaidi ni kwamba majaribio ya chanjo hiyo yamefanyika katika nchi saba tu zote za afrika ikiwemo nchi yetu ya Tanzania. mikoa iliyotumika kwa majaribio ya chanjo iyo ni mkoa wa tanga (wilaya ya korogwe) na mkoa wa pwani ( wilaya ya bagamoyo).

  hivi wana jf kweli serikali yetu inatutakia mema kwa kutufanya sisi ndo chambo kwa chanjo hiyo, hivi serikali haikujiuliza ni kwanini chanjo hiyo haifanyiwa majaribio pia katika nchi za wanaojiita watu weupe? ninachokiona mimi ni kwamba serikali kwa kweli imetuchoka raia wake kwa kiasi kikubwa. mimi sifahamu zaidi ila kwa suala la kujaribiwa sumu hii imeniuma sana maana ki kawaida wanyama wenye mifumo sawa na wanadamu ndio hujaribiwa kwa dawa fulani na siyo mwanadamu.

  Poleni sana ndugu zetu wa maeneo mliolishwa sumu hiyo. ni Mungu tu awanusuru waja wake ila serikali yenu kamwe haijawatendea haki.
  Ndugu wana Jf wenzangu. dua zetu ni muhimu sana ili kunusuru janga lolote kwa majaribu hayo. tena siju kama hao wanaojaribiwa wanafahamu kuwa wanajaribiwa... na hii ndiyo sirikali yetu.

  wenye uelewa zaidi watutoe hofu. karibuni sana
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wanasayans
  Eeeh! Mje mseme hapa
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,409
  Trophy Points: 280
  300600_10150419320033792_211320898791_10299918_126266094_n.jpg [​IMG]

  huyu ndio MISS MTWARA 2011 Rahma SWAI! alifariki dunia juzi baada ya kushikwa na HOMA kali, inayoaminika kuwa MALARIA, akapelekwa zahati sa5 usiku, daktari hayupo mpaka asubuhi, ilipofika saa9 usiku ikabidi rafiki yake ampeleke kwenye hospitali ya mkoa ambapo mwendo mfupi kabla ya kufika, akafariki dunia! R.I.P Rahma!

  MY TAKE: maleria huua ..acha watu wafanye tafiti usileta fikra za kiujima hapa
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  saint ivuga umekuwa dokta siku hizi
  magazeti yaliandika alifariki kwa shinikizo la damu ww unasema malaria anyway cha muhimu tumwombee apunzike kwa amani
  utakubali ww ufanyiwe majaribio???? kama ndio ujitokeze.
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,409
  Trophy Points: 280
  mkuu nitafanyiwaje majaribio wakati siumwi malaria? na hizo dawa amabazo tunaziumia sasa hivi ni kina nani walifanyiwa majaribio? wao sio watu?
   
 6. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Tuachane na dhana potofu maana ni mauti kwetu. Hakuna chanjo inayoweza kufanyiwa majaribio ktk mwili wa binadamu moja kwa moja, mtoa mada amechanganya neno majaribio na anatakiwa ajue kuwa sio dawa ndio inafanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza bali ni mradi ndio unafanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza ktk maeneo yaliyotajwa ili kujua matokeo yake kabla yakuusambaza nchi nzima. Hakuna Dawa inayojaribiwa kwa idadi kubwa ya watu namna hiyo hivyo tuhasishane watu wakapate chanjo maana malaria inakatisha maisha yetu kwa wingi sana.
   
 7. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  nadhani wewe liikwanda ndo umejichanganya. nilivyosema ndiyo nilivyosikia. wanafanyia majaribio dawa na siyo mradi. na kwa maneno yao ni kwamba walichogundua mpaka hivi sasa chanjo hiyo mafanikio yake mpaka hivi sasa ni asilimia hamsini tu ndiyo imebidi waendelee kujaribu kwa miaka miwili zaidi i li kuwa na uhakiika zaidi na chanjo hiyo...
   
Loading...