Ntate Mogolo
JF-Expert Member
- Jun 5, 2016
- 410
- 711
Polo kwa wahanga wa bomoa bomoa! Kweli ni majonzi kupoteza makazi yako, na hasa ukiwa na umri mkubwa, ni shida kweli kweli.
Ukiangalia mtazamo wa jamii iliyokumbwa na kadhia hii ya bomoa bomoa, lawama zinaiangukia serikali kwa kuongezea vipimo vya upana wa hifadhi ya barabara, lakini pia kwa kutokutoa fidia kwa wahanga wa bomoa bomoa hii!
Lakini kwa upande mwingine, jamii inapaswa kuwajibika kubeba sehemu kubwa ya lawama za bomoa bomoa inayoendeshwa na Tanroads. Yapo makosa mengi ya makusudi na pengine kwa kutokujua au kupuuzia tu ambayo wanajamii wa maeneo husika wameyafanya hapo kabla, matokeo yake wanakumbana nayo hii leo. Bomoa bomoa!
Watanzania walio wengi ni watu wa ajabu sana! Na hasa akipata pesa ya kujenga! Wengi hupata ujasiri wa kutaka kutumia njia ya mkato kutimiza adhima yao! Kwa kuwa anapesa, hutaka kujenga pahala popote pale anapotaka bila kufanya upembuzi yakinifu. Hadi hii leo, ukitembea sehemu mbali mbali katika miji yetu, utaona bado kuna maeneo ambayo ni hifadhi ya barabara kwa kuangalia hata kwa macho! Watanzania wenye pesa wanazidi kujenga mijengo ya bei kubwa! Lakini miaka ijayo bomoa bomoa ikija, hawa nao watakuwa wa kwanza kuona kuwa serikali imewaonea.
Hivyo basi, pamoja na kuitupia lawama serikali kwa zoezi la bomoa bomoa linaloendelea katika maeneo mbali mbali, kila mwana jamii anayeguswa na hili anawajibika kwa namna moja ama nyingine! Uwekezaji katika ujenzi wa NYUMBA ni uwekezaji wa muda mrefu! Hii ni tofauti na ununuzi wa gari, ambalo unaweza kuhamia mji mwingine ukabeba gari lako. Lakini nyumba hai hamishiki!
Haiingii akilini mtu anawekeza kiasi kikubwa cha pesa katika ujenzi wa nyumba katika eneo, bila kufanya utafiti wa kina kwenye mamlaka zote zinazo husika! Huo ni uzembe mkubwa, na matokeo yake ndo haya. Utaishia kuwa huna tofauti na mtu anaye anzisha ujenzi wa nyumba kwenye bonde la mto wakati wa kiangazi, siku masika yakianza na mvua zikaja, atapoteza nyumba yake.
Watanzania, tujifunze kufanya utafiti wakutosha katika mamlaka husika kabla ya kufanya ujenzi. Pia tupunguze kiburi cha pesa, tupokee ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali tunapotaka kujenga, itatusaidia kukwepa bomoa bomoa. Lakini mwisho, kiwanja cha barabarani siku zote kina athari kubwa sana usipokuwa makini.