Poleni Tanga, Wabunge wenu ni Mizigo

Riziki Magembe

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
886
206
Wana jamvi katika tathmini yangu mkoa wa tanga ni miongoni mwa mikoa yenye rasilimali na mazao mengi ya biashara ikiwemo ukanda mrefu wa kibiasha wa bahari ya hindi laki wabunge wake ni mizigo,naombeni tuwatathmini wabunge wa majimbo 11 ya mkoa wa tanga lakini pengine kuna mikoa mengine ina wabunge mizigo ungeni hapa ili tuwajadili kwa pamoja,pia majina yao mnaweza kuyataja ili tuwajadili vizuri
 
Tanga imejaliwa kila kitu kuanzia bahari, mbuga za wanyama za Saadani na Mkomazi, matunda ya kila aina, madini, Nyanda za juu kule Lushoto, wana reli na barabara kuu pamoja na ardhi nzuri ya kilimo na mifugo.

Wabunge wanaangalia zaidi maslahi yao kwa sababu vyote vilivyotajwa hapo juu havijapewa kipau mbele cha kutosha. Viwanda vya mbolea, chuma na chumvi vyote vimekufa! Viwanda vya simenti tu ndio naona vinaongezeka kwani kinajengwa cha tatu sasa.

Sijue sera za vyama zikoje kwani sioni mikakati yeyote mikubwa ya kuleta maendeleo mkoani hapa. Wawekeze hoteli Lushoto. wajenge viwanda vidogo vidogo vya kusindika matunda na mboga. Wafufue viwanda vya chumvi na mbolea, wavune mazao ya baharini na waendeleze wachimbaji wadogo wa madini. Vilevile wahamasishe wananchi walime, mkoa uwe mmoja wa wazalishaji wakubwa wa chakula hapa nchini.
 
Huku mwingine hata hajajua kulea familia eti anataka kugombea urais! hii nchi ina laana ukiwa unatembea unajikwaa na kiungo cha binadamu eti hospitali vifaa vya ku- dispose mabaki vimeharibika wakati pesa za viongozi kuzunguka watakako zipo!
 
Back
Top Bottom