Pole sana rafiki yangu. Ndoa hizi!

Pole sana rafiki yangu. Ndoa hizi!

ThaGreatman

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2018
Posts
708
Reaction score
1,466
Bila kupoteza muda, naomba kushea nanyi mkasa mzito ulomfika rafiki yangu.

Jamaa yangu anayeishi mkoani alifunga ndoa miaka kadhaa iliyopita, (jamaa alimuoa bibie akiwa na mahaba mazito sana na jamaa mmoja ambaye walisoma pamoja).

Baada ya miaka kadhaa kwenye ndoa na kubarikiwa watoto wawili, mke akakumbuka penzi la mpenzi wake wa zamani, akaanza kumbembeleza sana mpenzi wake wa kale waendelee na mahusiano huku akieleza magumu anayokutana nayo kwenye ndoa yake, jamaa alikataa. (Mke wa mtu hakukata tamaa, akaendelea kumuomba sana jamaa waendelee na mahusiano yao).

Baada ya mvutano wa muda mrefu, mke wa jamaa akaomba ruhusa kwa mumewe kwenda jijini Dar kusabahi ndugu zake. Jamaa akamruhusu, lakini kwa kuwa alikuwa na mashaka na mwenendo wa mkewe, alipanda ndege kwenda Dar wakati mke alipanda bus (mume akawahi kufika kabla ya mke,bna hivyo kusubiri uelekeo wa mke).

Mke amefika Dar, akapokelewa na mpenzi wake wa kale. Wakaenda hotel fulani karibu Ubungo, wakavunja amri ya sita mpaka asubuhi, wakati wote huo mume anamuuliza mkewe amefikia kwa ndugu yupi mke anamdanganya mumewe pasipo kujua jamaa yupo jijini tayari.

Asubuhi ya jana tarehe 20/10/2019 wameachana (wapenzi wa zamani) na kuahidiana kukutana siku itakayofuata kuendeleza usaliti wao. Mke anakwenda mchana kwa nduguye, akamkuta mumewe![emoji44][emoji44][emoji44][emoji44]

Mume kwa hasira kaanza kumpiga mkewe. Kampiga sana na kuondoka naye kurejea mkoani, (usiku wa kuamkia leo). Jamaa (mpenzi wa chuo) nipo naye hapa anajutia sana kukubali kulala na mke wa mtu, analia wakati wote tangu asubuhi, sasa sijui analia mpenzi wake kupigwa au analia kujutia kumkosea Mungu wake.

Wakati wengine wanakesha kuomba wapate waume hata waletwao na upepo wa kisulisuli, wengine walio ndoani wanasaliti ndoa zao na kufanya mambo ya kipuuzi kabisa (hapa justifications za kufanya usaliti sijazingatia).

Sijui huko mkoani kama huyu mwanamke yupo salama, mioyo imejaa hofu sana tukifikiria hasira za jamaa!

Wanawake kwa wanaume, mkiamua kuingia kwenye ndoa basi mjitahidi kuheshimu ndoa zenu (na kama mkishindwana basi achaneni kwa amani na maisha yaendelee). Lakini hii habari ya kusalitiana inaleta madhara makubwa sana, na wakati fulani inakatisha maisha ya watu kabisa!

Mungu aturehemu, pole sana dada kwa kipigo lakini pia pole sana brother kwa msukosuko huu mzito, kikubwa usimuue mkeo, unaweza kumuacha kwa kosa la kukusaliti au unaweza kumsamehe maisha yaendelee!
 
Mkaa gunia mbili
Usiseme hivyo ndugu unaumiza nafsi zetu...

Maana jamaa mwenye mke na mwizi wa mke pia wanafahamiana Ila mwenye mke hajui kuwa msaliti anayetoka na mkewe Ni mtu anaye mjua kabisaa
 
Wakuu mimi ni mtata sana ila amini siwezi kumpiga mwanamke nikifumania akiliwa na mwanaume mwingine..

Ningekuwa mimi hapo, kiroho safi kama nimethibitisha kwamba amechepuka
namruhusu tangu siku hiyo akaishi na huyo bwana mimi narudi kufanya mambo yangu.

Yawezekana dudu langu halimkidhi so alikuwa kwangu tu kwa sababu ya ndoa, hivyo nampa uhuru aende kwa huyo anaekimdhi na mimi kiroho naenda kutafuta mwingine wa kuendeleza gurudumu.
 
Huyo mwenye mke alichokosea ni kitu kimoja.

Kama ningekuwa mimi baada ya kupanda pipa na kufika mapema Dar, ningevuta muda kidogo halafu ningeenda moja kwa moja kituo cha basi kumsubiria mke wangu huku nikiendelea kuwasiliana nae.

Yani picha lote ningelimalizia hapo hapo Ubungo maana ningewabamba wote na ningeamua cha kuwafanya kutokana na makosa yao.
 
Mkwaha,

Alichofanya sahihi, alichokosea ni kumdunda tu. Alitakiwa amuache, yaani anaoa mke wa pili, mke akiuliza anampa talaka rasmi.
 
Write your reply...Amalia uyo mwanamke ataachika alafu hawezi mtunza
 
Nadumbukia muda si mrefu nitayaona yaliyomo.

Daaahh, mambo ya kupasha viporo haya.....
usiweke hisia huko,ingia kama unafanya biashara ya kufuga mbuzi,yaani mwanamke kama jike la mbuzi,ukiwa na mentality kwamba wewe ni mfugaji wa binaadam haitokusumbua,akizingua unafurusha unaleta mwingine,mtindo uwe huo hadi pale dushe litapoacha kusimama
 
Back
Top Bottom