MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,643
- 33,427
Wanabodi,
Nimesoma habari kupitia gazeti la Championi kuhusu hali mbaya ya kiafya ya mchezaji mkongwe aliyewahi kuchezea Simba kwa mafanikio makubwa na pia kucheza Taifa Stars kwa kipindi kirefu sana tena kwa kiwango cha juu Alphonce Modest.
Mchezaji huyu kwa mujibu wa Championi la leo anasumbuliwa na figo amelazwa Bugando Mwanza na hali yake kimaisha ni mbaya kumudu matibabu yake.Alphonce Modest amewataja Juma Kaseja na Mrisho Ngassa kama wachezaji pekee wanaomsaidia.
Namkumbuka mchezaji huyu alivyokuwa na nidhamu kubwa,mpole na mtu wa dini na hasa soka lake akiwa moja ya beki namba tatu bora kuwahi kutokea Tanzania.
Hali ya soka huko nyuma kifedha ilikuwa mbaya zaidi ya sasa na wachezaji wengi wamebaki maskini.
Naomba nitoe wito kwa TFF lifanye juhudi za kumsaidia Alphonce Modest ikibidi uwekwe utaratibu wananchi tumsaidie kuchangia tulicho nacho ili Modest ajue tunathamini mchango wake ktk Taifa hili na iwe motisha kwa vijana tunaowahimiza washiriki michezo.
Pole sana Alphonce Modest,Mungu mwenye huruma akupe nafuu ya haraka ili uendelee kujenga Taifa letu.
Mods habari hii ni zaidi ya sports!