Fikra tunduizi toka kwa Nyangeta Olomide Mwita

Motowntzjpm

Senior Member
Jun 16, 2023
118
191
Hili linatuhusu sote kama nchi, tumejenga utamaduni mbaya wa kuiga mambo ya kipumbavu badala ya kuiga mambo mazuri yenye faida. Tatizo hili lipo katika nyanja zetu zote za maisha iwe ni katika siasa, utawala wa nchi, utumishi wa umma, sanaa na michezo nk.

Hebu tuangalie hii picha vizuri, mchezaji wa timu yetu ya Taifa anaonekana akiwa katika mzozo na mchezaji wa timu ya Taifa ya Morocco. Kwa waliotazama mechi hii watakumbuka kuwa mchezaji wetu wa timu ya Taifa ndiye alianzisha mgogoro huo na baadaye alitolewa nje ya uwanja na mwamuzi. Timu yetu ya Taifa ilicheza rafu nyingi na kusababisha adhabu zilizosababisha tukafungwa magoli 3 kwa sifuri.

Kiwango chetu cha soka ni cha chini mno ukilinganisha na kiwango cha timu ya Taifa ya Morocco. Ni fursa adimu kwa timu changa kama yetu kupata bahati ya kucheza na timu kubwa kama Morocco katika michuano mikubwa kama ya AFCON. Bila kujali matokeo ya mchezo, wachezaji wetu wangecheza kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu huku wakijifunza mbinu, ujanja, na nidhamu ya soka kutoka kwa wachezaji wenzao wa Morocco badala ya kuonyesha ubabe wa kijinga wa kucheza rafu nyingi na kuishia kupoteza mchezo.

Tukiendelea na utamaduni huu wa kijinga hatutatoka hapa tulipo, iwe ni katika siasa zetu, chaguzi zetu, utawala wetu, elimu yetu nk.
 
Tatizo CCM usitafute mchawi
 
Back
Top Bottom