Mtoa mada ni muongo na amebainisha jinsi gani yeye ni pandikizi aliye kazini kumchafua January kwa manufaa ya watu anaowajua yeye. Huyu hawezi kuwa ni mtu wa Mungu aliyeandika haya. Kama alikuwapo kwenye kikao hicho, basi anadanganya kwa makusudi au hakuhudhuria kabisa kwahiyo ametunga ya kwake baada ya kuhadithiwa machache.
Mimi nilikuwapo katika mkutano huo na naweza hata kukuleteeni sauti ya hotuba yenyewe ili msikilize uwongo uliomwagwa hapa. Kimsingi maaskofu walimualika kuwahutubia kuhusu changamoto za Kitaifa na juu ya uongozi unaohitajika kupambana na changamoto hizo. Hakuna yoyote aliyepewa pesa na January katika mkutano huo. Hakuna.
Hakuna sehemu ambapo January aliwaomba maaskofu wamuunge mkono kugombea urais. Mambo aliyozungumzia ni kuhusu "inequality" katika jamii (yaani tofauti kati ya maskini na matajiri), kuhusu nyufa za kitaifa alizoongelea Nyerere miaka 20 iliyopita, kama rushwa, udini, uzanzibari na uzanzibara. Alizungumzia pia kuhusu kumomonyoka kwa maadili na kushamiri kwa uwongo, utapeli, ubakaji, wizi na mauaji katika jamii yetu, na jinsi gani viongozi wa dini wanavyofanya kazi kubwa kupambana na haya, na jinsi gani wanahitaji kusaidiwa na viongozi wa serikali.
Alisema kwamba kama Taifa tunahitaji uponyaji. Akasema katika uponyaji huo viongozi wa dini wana nafasi kubwa, kama viongozi wa kisiasa, hivyo lazima washirikiane. Akasema ili nchi ipone, lazima viongozi wa dini na wa kisiasa wawe wasafi na "wasipende kulamba sukari". Asema uongozi wa nchi hauna umri, alipotumia mfano wa Yeremia kwamba aliaminiwa na Mungu katika umri mdogo kuwa kiongozi. Haina maana kwamba alijifananisha naye. Alimaanisha tu kwamba hata vijana wanauwezo wa kuongoza na waaminiwe. Alimaliza kwa kusema japo tumefikisha miaka 50 ya Tanzania, safari yetu ya kujenga nchi ndio kwanza imeanza, lakini ili kupambana na changamoto zilizopo, nchi inahitaji kufanyiwa "reset" ili kujengwa upya na kizazi kipya.
Maneno yake yote yalikuwa na ushawishi mkubwa, hasa pale alipotumia mistari ya Biblia kujenga hoja zake. Imemuonyesha mbele ya viongozi hawa wa dini jinsi gani January ni kiongozi ambaye ni mcha Mungu, asiye mdini, anayekubalika na dini zote na aliyetayari kushirikiana na viongozi wa ngazi zote za jamii ili kupata majawabu ya changamoto zinazotukabili.